Dark City
JF-Expert Member
- Oct 18, 2008
- 16,253
- 11,598
Mara nyingi nimekuwa nikisikia viongozi wengi wakisema serikali haiwezi kutumia pesa zake kwa hili au lile. Hivi karibuni, Naibu waziri wa Elimu G Kabaka akaririwa akisema kuwa pesa za serikali haziwezi kutumika kumlipia kila mwanafunzi wa elimu ya juu. Mimi ninavyojua serikali imepewa jukumu na wananchi kukusanya kodi kwa niaba yao na kusimamia matumizi ya pesa hizo baada ya wananchi wenyewe (kupitia kwa wabunge wao) kuiambia jinsi ya kuzitumia. Sasa naomba nieleweshwe, hizi ni pesa za serikali au za umma? Maana huu mkanganyiko ndio unaosababisha pesa za umma (kama ninavyoamini mimi) zionekane kama hazina mwenye nazo na ni halali ya kila kibaka anayeweza kupata upenyo wa kuzikaribia. I think we need to be clear on this.