Fedha za safari za rais zapigwa panga

"Nyie mnataka nikialikwa niseme siji kwa sababu wananchi wangu hawapendi!, acheni hizo bwana"
 
Usanii tu aliweza kuchota mabilion 26 hazina atashindwa kuongeza

Umenena kweli mkuu!Hadi hapo Bunge liwe na nguvu kudhibiti hela HAZINA ndiyo uchotaji utakoma!

Rais wa TZ ni Mungu-Mtu ana nguvu kisheria kuchukua hela yyt BOT na huwa inafanywa hivyo!
 
Kamati ya bajeti ambayo inayongozwa na mwanasheria mkuu mstaafu Andrew Chenge imepunguza bilioni 11 kutoka kwenye bajeti za safari za Rais kwa mwaka wa fedha ujao.Fedha hizo zitatumika kwenye miradi ya maendeleo.

Mwaka wa fedha ambao unaelekea kuisha Rais alitengewa bilioni 50 kwa ajili ya safari japo ndani ya miezi 2 zilikuwa tayari zimeshatumika.

Kwa hiyo mwaka ujao wa fedha ametengewa bilioni 39 kutoka bilioni 50
==========================================




Chanzo: Nipashe
Rais anaongoza kwa kuwa na safari zisizo na tija kwa nchi.Watumishi wengine itakuaje?na pesa nyingi zinaibiwa ofisi ya membe tiketi bei mara 6 ya bei halisi
 
Msidanganyike na maneno yao hawapigi panga wa shoka wanawadanganya hao zipo palepale haipunguzwi hata sent moja
 
Umenena kweli mkuu!Hadi hapo Bunge liwe na nguvu kudhibiti hela HAZINA ndiyo uchotaji utakoma!

Rais wa TZ ni Mungu-Mtu ana nguvu kisheria kuchukua hela yyt BOT na huwa inafanywa hivyo!

Nahisi kuna mbunge mmoja aliomba serikali ilete mswada bungeni wa bunge kusimamia bajeti.Wenye kumbukumbu nzuri mnaweza nisaidia kuhusu la huyo mbunge kuomba huo mswada.
 
Chama Chakavu (CCM) tatizo mmechelewa sana kufanya huu usanii kiasi kwamba watanzania wameshawagundua ninyi ni wezi tu na hata mfanye kitu kizuri namna gani hakuna atakayewaamini tena. hebu fanya ka research kadogo sana hata kwa kuangalia maoni ya watu waliochangia hii thread then utagundua watanzania wanafikiria nini kuhusu CCM!!!!!!...
 
Usanii tu aliweza kuchota mabilion 26 hazina atashindwa kuongeza

Kweli huu ni usanii , hizo bajeti zao ni kiini macho tu. Wanasema huyo mkweree alipangiwa bajeti ya 15 bill mwaka jana kwa ajili ya safari zake na akatumia 50 bill. sasa kitu gani kitamzuia kutumia zaidi mwaka huu ambacho hakikumzuia mwaka wa fedha uliopita? Safari hizi za mara kwa mara umekuwa ni mradi kwa hawa viongozi kwani wapambe wao [MTAWA] wanabeba viroba vya dollar kwenda kuficha huko ughaibuni!!!
 
..wabunge wajinga sana nchi hii.....hili la rais kuongeza umaskini kwa safari zake wameligundua leo!! ...its too late for them....sasa wakati rais anakaribia kuondoka madarakani ndo eti wamegundua safari zake zinatafuna nchi!!..wamesahau kwamba raia tunapiga kelele tangu huyu mtembezi alipoingia madarakani....Wabunge warudi nyuma wapige hesabu ya gharama ya safari za JK tangu aingie madarakani...ndo watajua ikulu imeshirikije kuongeza umaskini kwa raia....
 
Bajeti ya safari za Rais yafyekwa
Jakaya-June11-2014.jpg

Rais Jakaya Kikwete

Wajumbe wa Kamati ya Bajeti wameibana serikali na kufanikiwa kupunguza zaidi ya Sh. bilioni 200 katika Bajeti Kuu ikiwamo matumizi ya anasa.
Katika kikao hicho kilichoanza tangu juzi, wajumbe hao wamepunguza maeneo ya anasa na safari za Rais zaidi ya Sh. bilioni 15 kwa mwaka 20/14/15.
Vyanzo vyetu vya habari vya kuaminika vilisema kuwa Rais mwaka huu (2013/14), alipangiwa bajeti ya Sh. bilioni 15, lakini ametumia karibu Sh. bilioni 50.
Chanzo hicho pia kilisema wajumbe wamepambana na kuipunguzia Ikulu Sh. bilioni 11.
Kilisema matumizi ya anasa kama kununua samani za ofisi na safari za mara kwa mara zisizo za lazima, ndizo zinazosababisha matumizi kuongezeka.
¡°Tumechoka kuona matumizi ya anasa huku wizara muhimu zinazogusa maisha ya wananchi zikikosa pesa,¡± kilisema chanzo hicho.
Aidha, alisema mwaka huu wa fedha Rais alitengewa Sh. bilioni 50, lakini wajumbe walichachamaa na kuondoa Sh. bilioni 11.
¡°Fedha zilizoondolewa zinapelekwa kwenye kilimo, afya na hasa suala la MSD,¡± kilisema chanzo hicho.
Alisema Wizara ya Afya iliomba Sh. bilioni 145, lakini serikali ikaitengea Sh. bilioni 45 tu.
¡°Sisi tumepambana mpaka zifike Sh. bilioni 95,¡± alisema.
Aidha, chanzo hicho kilisema wajumbe wamepambana ili kuongeza posho za madiwani zifikie zaidi ya Sh. bilioni tano na mifuko ya maendeleo ya vijana ifikie zaidi ya Sh. bilioni 10.
¡°Serikali walikuwa hoi na usiku huu wanakwenda kukutana kwenye kikao na JK,¡± kilisema chanzo hicho.
Hadi tunakwenda mitamboni wajumbe hao walikuwa bado wakiendelea na kikao hicho.


CHANZO: NIPASHE
 
jk.gif

Wajumbe wa Kamati ya Bajeti wameibana serikali na kufanikiwa kupunguza zaidi ya Sh. bilioni 200 katika Bajeti Kuu ikiwamo matumizi ya anasa.

Katika kikao hicho kilichoanza tangu juzi, wajumbe hao wamepunguza maeneo ya anasa na safari za Rais zaidi ya Sh. bilioni 15 kwa mwaka 20/14/15.

Vyanzo vyetu vya habari vya kuaminika vilisema kuwa Rais mwaka huu (2013/14), alipangiwa bajeti ya Sh. bilioni 15, lakini ametumia karibu Sh. bilioni 50.

Chanzo hicho pia kilisema wajumbe wamepambana na kuipunguzia Ikulu Sh. bilioni 11.

Kilisema matumizi ya anasa kama kununua samani za ofisi na safari za mara kwa mara zisizo za lazima, ndizo zinazosababisha matumizi kuongezeka.

"Tumechoka kuona matumizi ya anasa huku wizara muhimu zinazogusa maisha ya wananchi zikikosa pesa," kilisema chanzo hicho.

Aidha, alisema mwaka huu wa fedha Rais alitengewa Sh. bilioni 50, lakini wajumbe walichachamaa na kuondoa Sh. bilioni 11.

"Fedha zilizoondolewa zinapelekwa kwenye kilimo, afya na hasa suala la MSD," kilisema chanzo hicho.

Alisema Wizara ya Afya iliomba Sh. bilioni 145, lakini serikali ikaitengea Sh. bilioni 45 tu.

"Sisi tumepambana mpaka zifike Sh. bilioni 95," alisema.

Aidha, chanzo hicho kilisema wajumbe wamepambana ili kuongeza posho za madiwani zifikie zaidi ya Sh. bilioni tano na mifuko ya maendeleo ya vijana ifikie zaidi ya Sh. bilioni 10.

"Serikali walikuwa hoi na usiku huu wanakwenda kukutana kwenye kikao na JK," kilisema chanzo hicho.

Hadi tunakwenda mitamboni wajumbe hao walikuwa bado wakiendelea na kikao hicho.

Source, nipashe
 
Candid Scope billion 50 kwa ajili ya safari tuu na anasa huku budget za wizara zikiwa hata nusu yake hazikufikiwa ila fungu lake la safari hazikupungua hata shs moja
 
Last edited by a moderator:
Bajeti ya Sh50 bilioni zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya safari za Rais Jakaya Kikwete katika mwaka ujao wa fedha ni miongoni mwa mafungu ya fedha ‘yaliyopigwa panga' ili kuwezesha kupatikana kwa fedha za kugharimia miradi ya maendeleo.

Habari kutoka ndani ya kikao cha majadiliano baina ya Serikali na Kamati ya Bunge ya Bajeti zinasema, Sh11 bilioni zimepunguzwa katika fungu hilo na kubakiza Sh39 bilioni.

Hata hivyo, kiasi kilichobakishwa ni ongezeko la asilimia 260 la Sh15 bilioni zilizopitishwa na Bunge mwaka jana kwa ajili ya safari za Rais katika mwaka wa fedha unaomalizika Juni 30 mwaka huu.

"Katika bajeti ya 2013/14 safari za Rais zilitengewa Sh15 bilioni lakini inaonekana fedha zilizotumika ni nyingi zaidi maana ndani ya miezi miwili tu zote zilikuwa zimemalizika," kilisema chanzo chetu na kuongeza:

"Kwa hiyo kwa mwaka 2014/15 Serikali ilimtengea Rais Sh50 bilioni za safari, ila tumekata Sh11bilioni ili kupelekwa katika shughuli nyingine za maendeleo. Kwa hiyo kwa mwaka ujao wa fedha, safari za Rais zitatengewa Sh39 bilioni".

Awali, ilielezwa kuwapo kwa mvutano mkali baina ya Serikali na Kamati ya Bunge ya Bajeti, lakini jana mchana pande hizo zilikubaliana kukata asilimia 7.5 ya fedha katika baadhi ya mafungu ya matumizi mengineyo (OC) kutoka katika wizara zote ili kuwezesha kupatikana kwa Sh230 bilioni ambazo zinahitajika kwa ajili ya maendeleo hasa katika sekta tatu; afya, miundombinu na kilimo.

"Bado kikao kinaendelea na tangu asubuhi tumekata fedha katika fungu la matumizi mengineyo, mfano chai katika ofisi za wizara pamoja na ununuzi wa magazeti, ununuzi wa magari ya kifahari, mafuta, viburudisho, semina na makongamano pamoja na safari za ndani," kilieleza chanzo chetu.

Chanzo kingine kutoka Serikalini kilisema: "Katika siku ambazo tumevutana kwenye kikao cha kamati ni leo (jana), lakini mwishoni tulifikia mwafaka wa kukata kati ya asilimia saba na nane ya fedha za matumizi mengineyo katika wizara zote, ili kupata fedha za maendeleo."

Juzi, Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba alisema wizara yake inakusudia kupitia bajeti za wizara zote ili kuhamisha fedha kutoka katika matumizi yasiyo ya lazima ili zielekezwe katika mahitaji muhimu.

"Kama wananchi wanakula mlo mmoja kwa siku, waliopo wizarani hawawezi kufa kwa kukosa chai asubuhi. Tutafanya hivyo ili fedha hizo zipelekwe katika shughuli za maendeleo.

Kesho (jana) katika kikao cha mashauriano tutakwenda kuweka msimamo wa pamoja katika jambo hilo. Wizara zisielekeze macho Wizara ya Fedha pekee, nazo zinatakiwa kuwa na mikakati ya kubana matumizi yake."

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Andrew Chenge alipoulizwa kuhusu hatua iliyofikiwa katika majadiliano alisema: "Subirini itakaposomwa bajeti mtajua kilichoamuliwa." Vyanzo vya mapato
Licha ya kuwapo kwa makubaliano kuhusu suala la matumizi, vyanzo vya mapato vimeendelea kuwa siri hata kwa wajumbe wa Kamati ya Bajeti.

Usiri wa vyanzo hivyo ni moja ya mambo ambayo yalizua mvutano kutokana na wabunge kutaka kufahamu ni kwa vipi Serikali itamudu kupata kiasi cha Sh19 trilioni kugharimia Bajeti ya 2014/15, wakati imeshindwa kutimiza malengo ya kukusanya Sh18.2 trilioni kwa mwaka huu wa fedha.

Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya bajeti, Hamad Rashid Mohamed alisema Serikali imekuwa ikishindwa kukusanya mapato ya kutosha kutokana na kung'ang'ania kutekeleza miradi ambayo ingeweza kufanywa na sekta binafsi.

Mbunge huyo wa Wawi (CUF), alitoa mfano wa miradi mikubwa ya kujenga reli, bandari na barabara kwamba inaweza kutekelezwa na sekta binafsi kwa ubia na Serikali.

Alisema kutokana na mahitaji makubwa ya kifedha, Serikali imekuwa ikikisia makusanyo makubwa ambayo haiwezi kufikia malengo yake, hivyo kuathiri miradi mingi ya maendeleo.

"Sisi tumekuwa tukiwaambia kama fedha za ziada zinapatikana, Bunge lipo walete supplementy budget (Bajeti ya nyongeza) kuliko huu utaratibu wa sasa wa kupitisha bajeti ya mapesa mengi ambayo hatuna uwezo wa kuyapata," alisema.

Alisema tatizo lingine ni kukosekana kwa nidhamu ya ukusanyaji na matumizi ya fedha... "Kuna miradi hewa na mingine fedha zinaonekana kwenda lakini haijatekelezwa, haya ni mambo ambayo yanaifanya bajeti yetu kutotekelezeka."

Jana, Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum alisema Serikali itatangaza vyanzo vyake vipya wakati wa kusoma bajeti yake bungeni... "Huo ndiyo utaratibu wa kawaida kabisa miaka yote."

Akizungumzia suala hilo, Nchemba alisema: "Hatuwezi kuweka wazi vyanzo vya mapato hivi sasa, kwa sababu tulichonacho ni mapendekezo tu."

Alisema mapendekezo hayo yatapelekwa Baraza la Mawaziri ambalo litaongozwa na Rais Jakaya Kikwete ambaye anatarajiwa kuwasili Dodoma leo.

 
Candid Scope billion 50 kwa ajili ya safari tuu na anasa huku budget za wizara zikiwa hata nusu yake hazikufikiwa ila fungu lake la safari hazikupungua hata shs moja

Mbaya zaidi mwaka huu alitengewa bilioni 15, lakini yeye katumia zaidi billion 50, hizi ametichukua toka wapi bila idhini bunge?
 
Mbaya zaidi mwaka huu alitengewa bilioni 15, lakini yeye katumia zaidi billion 50, hizi ametichukua toka wapi bila idhini bunge?

Ndio maana wasaidizi wake kila mara wanampangia safari fungu kubwa sana hilo aise na posho ziko nje nje kutokana na safari hizi
 
Mbona wamechelewa sana, Ila wasiishie tu kwa safari za Rais tu, wapunguze mpaka kwenye safari za mawaziri.

Hapa hakuna kitu ni usanii tu. Nani au chombo gani nchi hii kinaweza kumzuia rais afanye atakavyoo? Hata kama bunge litapunguze, yeye atatumia mara dufu na hakuna wa kumwuliza. Yote hii ni gia ya uchaguzi ujao ili ccm waseme wanawajali wananchi. Hizi safari za rais zimepigiwa kelele na wananchi tangu aingie madarakani, eti sasa ndio wabunge wa ccm wanaona safari za rais ni mzigo wakati walikuwa wanasema zina manufaa makubwa kwa nchi.
 
Mimi siamini kama kweli zimepunguzwa.Hilo ni changa la macho kwa walipa kodi.

Kwanza tujiulize kama alipangiwa bil 50 na alizimaliza ndani ya miezi 2 je zilipoisha aliacha kusafiri kwa sababu budget yake imeisha?Who is fooling who? Ukweli ni kwamba wamepunguza tu kwenye makarakasi lakini mkuu ataendelea kuchanja anga as usual. Au mmesahau kuwa mkuu hakuachiaga uwaziri wa mambo ya nje japo ni presideee (asikiaye na afahamu).
 
Wanaudanganya umma hao, nani utakuwa na jeuri hiyo.Kwani zilipozidi bajeti hawakuona
 
Back
Top Bottom