Fedha za rambirambi zaivuruga familia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fedha za rambirambi zaivuruga familia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Apr 20, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Imeandikwa na Mwandishi Wetu, Arusha; Tarehe: 19th April 2011
  Habari Leo

  FEDHA za ubani kutokana na kifo cha aliyakuwa mfuasi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Ismail Omari, aliyeuawa Januari 5, zinaonekana kuivuruga familia hiyo ya marehemu.

  Fedha hizo ni zilizochangwa Januari 12 chama hicho kilipokusanya maelfu ya wafuasi wake kwenye uwanja wa NMC kwa lengo la kuomboleza vifo vya Ismail na Denis Shirima na kukusanywa kiasi kikubwa cha fedha zikiwa ni rambirambi kwa ajili ya familia zao.

  Mbali na mchango uliochangwa siku hiyo kabla ya miili kuzikwa, pia wanachama na wapenzi wa chama hicho nchini walichangia familia hizo, ambapo mfanyabiashara maarufu nchini, Mustafa Sabodo, alitoa Sh. milioni 10 kwa familia hizo.

  Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa bado fedha hizo hazijaifikiwa familia ya Ismail, licha ya jitihada kubwa zilizofanywa nayo kuhakikisha inapata fedha hizo, lakini hadi leo bado inasota bila mafanikio.

  Kutokana na hali hiyo, mjane wa Ismail, Asia Mussa (26), amelazimika kuondoka Arusha na kurudi kwao Lushoto, Tanga, baada ya kudai fedha hizo tangu mumewe alipoagwa uwanjani hapo.

  Akithibitisha hilo kabla ya kuondoka hivi karibuni, Asia alisema asingeweza kuendelea kusubiri malipo hayo yanayoonekana kama yameyeyuka, hivyo ni bora akamshitakie Mwenyezi Mungu, kwani ndiye mtoa riziki na kama ni riziki ya watoto wa marehemu, ni wazi itawafuata watakakokuwa wakiishi.

  “Nilikwenda ofisi ya Munge, nilijibiwa majibu ya kejeli, siwezi kusahau katika maisha yangu … eti si lazima watoto wa marehemu wakapewa rambirambi zao. Nikaona ni vizuri nijiondokee…tumevumilia vya kutosha, tumefuatilia vya kutosha, sina hamu na ofisi ile ya Munge tena,” alisema Asia kwa masikitiko makubwa.

  Msemaji wa familia, Nyerere Kamili, alisema kitendo walichofanyiwa na Chadema hakiwezi kuvumiliwa na hakifai katika jamii ya kitanzania yenye kuheshimu amani na utulivu, kwani wametembea kufuatilia ahadi za chama hicho bila mafanikio, hivyo kuamua kushitaki kwa Mungu.

  Alisema walifuatilia fedha hizo kwa Mbunge, Godbless Lema, akawa hapokei simu, katika ofisi yake walikwenda hadi wakaonekana wasumbufu, huku wahusika wakitoa kauli za kashfa dhidi yao, hivyo wamechoka.

  “Baada ya kufuatilia kwa muda mrefu, baba wa marehemu alilazimika kurudi nyumbani Kondoa, lakini mwishoni mwa Februari walimwita kupokea fedha hizo, mzee aliendelea kusumbuka hadi Machi 17 walipotakiwa kufungua akaunti ya pamoja benki, baba wa marehemu na mke wa marehemu, na hata walipofungua hakuna kilichoingizwa hadi leo,” alisema Kamili.

  Aliongeza kuwa chama hicho kilimwandikia barua yenye kumbukumbu namba CDM/AR/J.02/14.11 ya Februari 14 iliyosainiwa na Katibu wa Chadema wa Mkoa, Amani Golugwa, ikiwataka kutoa taarifa ya mpango wa mirathi na miniti za kikao cha familia na kutekeleza maelekezo hayo mara moja, walitekeleza, lakini hakuna malipo yaliyofanywa.

  Baba wa marehemu, Omari Juma, akizungumza kwa masikitiko, alisema kitendo cha vingozi wa chama hicho kuwasumbua kiasi hicho ni kielelezo cha wazi kuwa hawakuwa na nia ya kumsaidia mtoto wa marehemu, bali walichokuwa wakitaka wanakijua wenyewe.

  “Hivi karibuni walituita, tukaenda mimi na Nyerere, jambo la kushangaza walitukalisha ofisini hadi saa 9 alasiri, tangu asubuhi na baadaye wakatuonesha hundi tupu isiyo na maandishi yoyote na kutueleza kuwa hawawezi kuitoa hadi mjane awepo … kwa nini hadi mke wa marehemu awepo, wakati tulifungua akaunti ya pamoja?” alihoji Juma.

  Baada ya kukumbwa na ukata kimaisha, familia hiyo ililazimika kwenda kumwona Meya wa Jiji, Gaudance Lyimo na kuelezea kilichowakuta pamoja na ukata unaowasakama na Meya kuwasaidia Sh 200,000 ili kupunguza ugumu wa maisha, huku akiwasisitiza kusubiri kwani ipo siku watalipwa.

  Lyimo alithibitisha kwa njia ya simu juzi kutoa msaada huo akieleza kuwa wakazi wa Arusha ni watu wake na hana sababu ya kubagua familia hiyo licha ya wao hususan yeye (Meya) kuonekana kuwa ndiye chanzo cha yote yaliyotokea kinyume na ukweli halisi wa jambo hilo.

  “Ni kweli walifika ofisini kwangu kunishitakia masuala yao na Chadema na ukata unaowakabili hasa mjane, nilishindwa kuwasaidia madai yao kwa viongozi wa chama hicho, lakini nilipunguza ukata wao kwa kuwapa pesa kidogo kutoka mfukoni mwangu na nipo tayari kutoa msaada pale hali itakavyoruhusu,” alisema Lyimo.

  Chama hicho kilifanya maandamano hayo wakidai kubatilishwa kwa uchaguzi wa Meya wa Jiji hili, Lyimo (CCM) na Naibu wake, Michael Kivuyo (TLP) kwa madai ya kukiukwa kwa kanuni na taratibu katika kuwachagua viongozi hao.

  Akizungumzia tuhuma hizo, Mbunge Lema alisema ni kweli familia ya marehemu Omari haijalipwa fedha hizo kutokana na familia hiyo kutojipanga na kufuata taratibu za nani apewe fedha hizo, kwani kuna mgongano kati ya wazazi wa marehemu na mjane mwenye mtoto wa mwaka mmoja.

  Mbunge huyo aliishauri familia hiyo kwenda mahakamani kufungua mirathi ili iamue ni nani mwenye haki ya kuchukua fedha hizo, kwani mjane Asia hufuatilia fedha hizo akifuatana na baba mkwe wake waliyefahamiana wakati wa msiba.

  Alisema marehemu alilelewa na mama yake ambaye ndiye alimzika, huku baba yake akifahamiana na marehemu miaka mitatu tu kabla ya kifo, hivyo kinachotakiwa ni wote watatu kukubaliana, kwani kila mmoja anastahili kupata.

  Alisema fedha hizo ambazo ni Sh. milioni tano zilishindwa kuingizwa kwenye akaunti ya pamoja waliyofungua mjane na mkwewe, kutokana na mke kulalamika kuwa yeye na mkwewe wanaishi mikoa tofauti hivyo haitawezekana kimatumizi.

  Lema alisema hawawezi kutoa fedha hizo kiholela mpaka utaratibu ufuatwe, ili anayestahili aweze kulipwa na kusisitiza kuwa ikiwa wataendelea kutoelewana, yeye mbunge atabeba mzigo huo na kumpa mjane fedha hizo, zimsaidie matunzo ya mtoto.

  Alisema baada ya kufungua akaunti na kupeleka barua za vikao vya familia, waliwaita ili kujadiliana kabla ya kuwapa fedha hizo, lakini cha kushangaza alifika baba wa marehemu na Kamili ambaye si ndugu wa familia.

  Baada ya utafiti alisema waligundua walimsafirisha kwa makusudi mke wa marehemu, ili akachukue fedha hizo lakini walikataliwa hadi awepo mjane huyo.

  Alisema hawana sababu ya kusita au kuidhulumu familia hiyo ya Ismail kwani majeruhi wote waliwatibu mpaka wakatoka hosptalini na hakuna waliyemdhulumu kwani tayari familia ya marehemu Shirima imelipwa kutokana na wao kutokuwa na matatizo.

   
 2. A

  Adili JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2011
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 1,997
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Marehemu alikuwa na mke (mjane) na mtoto/watoto. Chadema inaona ugumu gani kumpatia mjane pamoja na watoto wake hela hizo. Kama marehemu alikuwa hakuandika wosia basi kisheria warithi wake ni mjane na watoto wake. Au bado tuko kwa zile imani kuwa mwananamke anarithiwa na ndugu za marehemu? Hili linatia dosari sana kwa Chadema.
   
 3. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #3
  Apr 20, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Na hayo ni Matatizo ya Nchi yetu... Katiba mpya lazima iwe na kifungu cha Urithi ni bora ufuate Mswada wa Serikali; Serikali inatakiwa isiwe na dini; Mila zetu na Ukabila na dini zetu mara nyingi zinagombania mali za wafiwa;

  "Mimi nilikuwa mtoto wa pili wa kiume baba yangu alipofariki sikurithisha Mashamba na Mali alizokuwa nazo walimpa Kaka yangu; good enough Kaka ananigawia lakini wazee wa kimila hawanitambui kwenye huo Uridhi"
   
 4. Diehard

  Diehard JF-Expert Member

  #4
  Apr 20, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 370
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Tatizo Gazeti Habari Leo lingekuwa Mwananchi Nipashe kwa mbali ningeamini lakini sio hili ambalo ndugu wa Ismail walikanusha nja klulipinga vikali kuwa linapotosha jamii kuhusu ile habari za kulazimishwa kuupe;leka mwili wa marehemu viwanjani kuagwa.,

  More likely the news have been cooked
   
 5. p

  politiki JF-Expert Member

  #5
  Apr 20, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Jamani hili liwe somo kwenu wenye familia,
  kila mwenye familia get a will today ama sivyo utaipitisha familia yako
  kwenye matatizo ambayo yanaepukika.
  Ushauri wangu wa haraka haraka kwa chadema mpeni pesa mke wa marehemu kwa niaba ya mwanaye full stop.
   
 6. Khakha

  Khakha JF-Expert Member

  #6
  Apr 20, 2011
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 2,983
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  habari leo ni gazeti la kipuuzi. Cjawahi kuliona kwenye newsstands likiuzwa.
   
Loading...