Fedha za maafa Kagera zakarabati shule ya CCM

Fedha za maafa Kagera zakarabati shule ya CCM

Papushikashi

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2016
Posts
11,354
Reaction score
13,884
Bukoba. Wakati baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Kagera wakilalamikia kukosa misaada iliyotolewa na wahisani kwa wathirika wa tetemeko la ardhi, imedaiwa kuwa Shule ya Sekondari ya Omumwani inayomilikiwa na Jumuiya ya Wazazi ya CCM imekarabatiwa kwa fedha hizo.

Madai hayo yalitolewa na Meya wa Manispaa ya Bukoba, Adronikus Karumuna kuwa sehemu ya miundombinu ya shule hiyo yakiwamo mabweni yalikarabatiwa ili kupokea baadhi ya wanafunzi waliohamishwa kutoka sekondari za Ihungo na Nyakato ambazo zinajengwa upya.

Akichangia taarifa ya tetemeko la ardhi iliyowasilishwa jana katika Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera (RCC), Meya huyo alishutumu matumizi mabaya ya fedha hizo. Alisema haikuwa haki kutoa kipaumbele cha ukarabati wa shule inayomilikiwa na CCM badala ya sekondari za Serikali.

Meya huyo alisema kamati ya maafa kushindwa kuzishirikisha kamati za mitaa na kata kumesababisha malalamiko mengi.


Chanzo: Muungwana
 
Naumia sana kuona mamb bado yako ovyo............

Kweli ubaguzi hauwez kuisha kama bado mtu anachagua kufua nguo nyeupe kabla ya nyeusi.......

Hapa naona wamechagua kujenga shule ya chama kabla ya shule za serikal......

[HASHTAG]#StepByStep[/HASHTAG]
 
Naumia sana kuona mamb bado yako ovyo............

Kweli ubaguzi hauwez kuisha kama bado mtu anachagua kufua nguo nyeupe kabla ya nyeusi.......

Hapa naona wamechagua kujenga shule ya chama kabla ya shule za serikal......

[HASHTAG]#StepByStep[/HASHTAG]
Mtu ukioji unaitwa mchochezi
Ila mambo haya yanauma sana
 
Nakubali kuna baadhi ya mambo ambayo yamefanyika ya ndiyo sivyo, lakini hili la shule ya Omumwani naona RC na uongozi wake wamefanya uhamuzi sahihi kabisa - sasa mlitaka wanafunzi wa Ihungo na Nyakato walale wapi - Mahotelini?

Haya mambo ya kusema ni Shule ya Chama mnataka kuleta mambo ya siasa tu, ukweli wa Mambo Shule ya Omumwani ilijengwa miaka ya 1968/69 majengo yake bado ni imara kuliko majengo mengine ya Sekondari za zamani save Rugambwa, hivyo Uongozi wa Mkoa kupanua mabweni na classrooms ku accomodate wanafunzi kutoka Ihungo na Nyakato sioni uhamuzi huo una walakini gani, hata mimi nilikuwa nalifikiria sana hilo.

Binafsi naona madai ya kusema eti Serikali imetumia fedha za michango kukarabati Shule ya Chama - madai hayo hayana mshiko wowote - mambo mengine tusijaribu kuweka chumvi mno.
 
Zilianza zikakarabati shule ili kuondoa Aibu na kuzidi kushikilia akili Zetu Kwa sasa Shule imerudishwa Serikalini. Maana yake sasa inaenda kujengwa Shule ya Kimataifa.
 
Back
Top Bottom