Mdakuzi mkuu
JF-Expert Member
- Dec 27, 2016
- 212
- 719
BAADHI YA MASWALI YALIYOULIZWA
Nimewaza tu hapa. Kumekuwa na fedha nyingi sana inayotolewa mahakamani na watuhumiwa mbalimbali kuhusu kesi kadhaa ili wapewe dhamana.
Utasikia "ameachiwa kwa dhamana ya TZS 10 Millioni, ameachiwa baada ya kutoa TZS 2 Million, wamekamilisha masharti ya dhamana wakatoa TZS 5 Million kila mmoja, nk".Mfano Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, kila siku iendayo kwa Mungu, mamilioni yanaingia pale kama benki vile.Na mahakama zinginezo huko mikoani nako watu wanatoka kwa dhamana ya hela nyingi sana.
Je,fedha hii itolewayo mahakamani kama dhamana, huenda wapi au hufanya kazi zipi?Hazina wanazichukua au ni mapato ya ndani ya Halmashauri husika?
Asanteni
---
Salaam,
Nimekuwa nikisikia mara kadhaa watuhumiwa hutakiwa kutoa kiasi fulani cha fedha kama dhamana dhidi ya mashtaka yanayowakabili ili waachiwe kutoka mahabusu.
Je, fedha hizi huwa zinarudi?
Asante.
BAADHI YA MAONI YALIYOTOLEWA NA WADAU
---Dhamana sio mapato mkuu, dhamana (kama ni fedha taslimu) hurudishwa kwa mhusika (mdhamini) baada ya kuisha kesi au muda wowote atakapoamua kujitoa kama mdhamini wa mtuhumiwa, itaingizwa kama mapato pale tu mtuhumiwa atakapokiuka masharti ya dhamana kwa kutoroka na mdhamini ashindwe kumfikisha mahakamani au kueleza mahali alipo ili asaidiwe kumpata.
Hata hivyo mahakama itampa muda mtu huyu amtafute huyo mtuhumiwa na atakaposhindwa kumfikisha mahakamani mpaka muda aliopewa kuisha..basi ndio watakapoichukua hiyo pesa (kutaifisha) na kama dhamana ni mali (nyumba au kiwanja) watavutaifisha na kuvipiga mnada
Dhamana nyingi ambazo hazihusishi kesi za wizi wa pesa, ambapo dhamana inahusisha kuweka hati zisizohamishika zenye thamani ya nusu ya pesa unayodaiwa kuiba.
Dhamana zingine una sign hati (bond) sio cash!!! Mnadhimi anakuja na vitambulisho na barua zake za ofisini au mtendaji wa mtaa na ku sign hizo bond sio cash.