Fedha chafu sasa basiiiiii?


mkerwaji

mkerwaji

Member
Joined
Feb 9, 2010
Messages
27
Likes
1
Points
5
mkerwaji

mkerwaji

Member
Joined Feb 9, 2010
27 1 5
“Sheria inalenga katika kuweka utaratibu wa kudhibiti matumizi ya fedha wakati wa kampeni za uchaguzi na kuweka mfumo wa kisheria wa uwajibikaji katika matumizi ya fedha za umma na vile vile kuanisha adhabu kwa watakaokiuka masharti,” inaeleza sehemu ya madhumuni ya muswada huo.Sheria mpya imeelezwa kulenga kupunguza matumizi mabaya ya fedha wakati wa kampeni na uchaguzi ikiwa ni pamoja na moja ya njia ya kudhibiti vitendo vya rushwa ndani ya vyama vya siasa wakati wa mchakato wa uteuzi na wakati wa uchaguzi.Kwa mujibu wa maelezo ya muswada huo, kutakuwapo na utaratibu wa kisheria utakaowezesha kuwapo haki na usawa katika matumizi ya vyombo vya habari vya umma na ulinzi kutoka kwa vyombo vya dola wakati wa kampeni hadi uchaguzi wenyewe.Hatua kadhaa zimependekezwa katika muswada huo ikiwa ni pamoja na kufutwa kwa mgombea atakayejihusisha na vitendo vya rushwa wakati wa kampeni na uchaguzi na kuwapo kwa vipengele vya faini ya hadi shilingi milioni kumi.Mbali ya vitendo vya rushwa, sheria mpya itawalazimisha wagombea na vyama vya siasa kutoa taarifa ya vyanzo vya mapato nje ya ruzuku itakayokuwa inatolewa na Serikali, hatua ambayo imeelezwa inalenga kupunguza kuingia kwa fedha haramu katika siasa.Kumekuwapo na vilio vya matumizi makubwa ya fedha katika siasa kiasi cha kuwafanya watu wenye uwezo wa kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kukata tamaa kujihusisha katika siasa na hivyo kugeuza siasa kuwa mikononi mwa wenye fedha pekee.Hatua ya sasa ya Serikali kuandaa sheria ya udhibiti wa matumizi ya ovyo ya fedha itaibua changamoto jipya kwa watu wenye uwezo mkubwa kisiasa ambao walikwisha kukata tamaa kujihusisha na siasa kwa kuchelea kutumia rushwa.ANGALIZO!JE HIKI NDICHO TUTARAJIE KWA SHERIA HII? AU NI MWANZO WA MBINYO WA DEMOCRASIA NA WANA DEMOCRASIA?
 

Forum statistics

Threads 1,235,149
Members 474,353
Posts 29,213,291