February:kwa nini kuna mwaka una siku 28 na mingine 29

Da vinci jr

JF-Expert Member
Mar 12, 2012
202
34
Soma Hapa
Kalenda tunayo tumia leo imetokana na kalenda ya Juliani ya kirumi. Hapo zamani kalenda hii ilikuwa na miezi kumi tu katika mwaka. Ndio maana Desemba tafsiri yake kwa lugha ni mwezi wa kumi. Baada ya mwezi wa kumi zilibaki siku nyingi za majira ambazo warumi hawakuzijali. Mwezi wa kwanza(machi) ulianza mara baada ya majira mengine kuanza. Miezi yote 10 ilikuwa na siku 29 kulingana na mzunguko wa mwezi.

Mfalme wa pili wa roma Numa Pompilius aliamua kubadilisha kalenda hii kwa kuongeza miezi miwili, Januari na Februari baada ya Desemba ili kumalizia zile siku za majira ambazo hazikuwekwa kwenye kalenda. (Januari ulikuwa mwezi wa 11 na Februari wa 12). Miezi hii miwili iliyo ongezwa ilikuwa na siku 29 kama miezi mingine.

Baada ya kipindi kirefu miezi iliongezwa siku hadi 30 kwa sababu alizo zijua mfalme wa kipindi hicho. Kama hiyo haikutosha baadhi ya miezi iliongezwa siku moja, hivyo kufikia siku 31. mwezi wa siku 31 ulifuatiwa na mwezi wenye siku 30.

Machi 31, Aprili 30 ,may 31, juni 30, julai 31, Agusti 30 na kuendelea.

Baada ya kipindi kingine kirefu, mfalme aliamua kuongeza siku moja katika mwezi Agusti ili kumuenzi Kaisari Agustus, siku hiyo aliitoa katika mwezi wa februari ili asibadilisha urefu wa mwaka. na hiyo ndiyo sababu mwezi huu wa Februari unakuwa na siku 28/29. na pia ndio sababu miezi Julai na Agusti inayo fuatana yote ina siku 31.

Chanzo:
tinomasayansi
 
Nina kukubalia tu kwa sababu mmetengeneza kastori kazuri na mmeipanga bila kukosea naona unatupeleka unaturudisha

tu kuchezea akiri zetu ili mradi stori tamu. basi sawa umejitahidi kufikisha tu ilimradi basi.
 
mmmh hapa ni sharow reasoning.... lakini sawa!!!!

Nadhani swala hilo ni la kisayansi na linaelezeka vizuri.Tungoje wataalam watujuze,sıdhani kama ni swala la kuongeza au kupunguzwa sıku na mtu bali kutokana pengne na motion za dunia na satelite zake kwa mahusiano baina yao kadhalika jua.
 
Kwa sababu Joshua alisimamisha jua .Soma kwenye biblia Yoshua 10:13 "ndipo jua likasimama na mwezi ukatulia...."
So ndio maana februari una siku mbili pungufu
 
History of calendars
From Wikipedia, the free encyclopedia
The history of calendars spans several thousand years. In many early civilizations, calendar systems were developed. For example, in Sumer, the birthplace of the modern sexagesimal system, there were 12 months of 29 or 30 days apiece, much like the modern Gregorian calendar. Mesoamerican cultures also developed their own intricate calendars; the ancient Maya had two separate years-the 260-day Sacred Round, and the 365-day Vague Year. Classical Greek and Roman cultures also developed calendars; the ancient Athenians, for one, had a lunisolar calendar that lasted 364 days, with an intercalary month added every other year. The Romans used two different year lengths; the older one had 304 days divided into 10 months; the newer 365 days divided into 12 months, very much like the modern calendar. They counted years from the founding of Rome, or, sometimes, from the reign of the current consul. The Hindu calendar is known from texts from about 1000 BC and divides an approximate solar year of 360 days into 12 lunar months of 27 or 28 days. The resulting discrepancy was resolved by the intercalation of a leap month every 60 months (Hindu calendar - Wikipedia, the free encyclopedia). The Islamic civilization also developed their own calendar based on the moon (see Islamic calendar - Wikipedia, the free encyclopedia).

The oldest known Calendar is a Lunar Calendar in Aberdeenshire, Scotland, which was constructed around 8,000 BCE.[1]
 
Angalau nimepata cha kujibu endapo m2 ataniuliza,,,bt am nt sure if tz true o not,.
 
Haruni au Joshua wa wana wa Israel kuna kipindi alisimamisha jua lisizame kwa muda ili apate wasaa wa kuwatandika Wafilisti. Source Biblia Agano la Kale
 
Kwa sababu Joshua alisimamisha jua .Soma kwenye biblia Yoshua 10:13 "ndipo jua likasimama na mwezi ukatulia...."
So ndio maana februari una siku mbili pungufu

Hiki kitu hua kinanichanganya mkuu.....kwa nn alisimamishe jua wakati jua halizunguki?? Msaada kaka
 
Habarini za muda huu wana jamii wenzangu........kuna kitu tangu ningali mdogo najiulizaga alafu sipati majibu kuhusu mfumo uliotumika kuundia kalenda,,Hivi kwanini kila mwaka mwezi wa pili(february) unakuwaga ni mfupi???
 
Habari

Nilipokuwa nasoma shule ya upili tulifundishwa long year na leap year. Ule mwaka unaogawanyika kwa nne(4) unakuwa long year yaani mwaka mrefu ambapo mwezi february unakuwa na siku 29.

Mwaka usiogawanyika kwa nne huu tunauita leap year yaani mwezi february unakuwa na siku 28.

Mwaka jana nilisoma makala moja iliyokuwa inaeleza hapo ilikuwaje. Katika kalenda ya julian ilikuwa ina shida ya kimahesabu. Kama tunavyojua dunia huzunguka siku 365 na robo. Sasa kila mwaka kwenye kalenda ya juliani ilikuwa zinaongezeka (sina uhakika) dakika moja.

Sasa kwa mahesabu iyo dakika moja inayoongezeka ikipita miaka na miaka inakuwa saa. Na saa zikiwa zinaongezeka inatokea siku. Sasa maana ya siku 365 na robo inapoteza maana.

Alipokuwa papa Gregorian alibadilisha huu mfumo na kuunda Gregorian kalenda ambayo tunatumia hii leo.

Nachotaka kukijua ni namna gani walitumia hesabu zao ili kuweza kuweka mlinganyo ambapo ulisaidia siku zibaki pale pale yaani siku 365 na robo. Walitumia kanuni gani kuisaidia dunia isipotee na upumbafu

Asante
 
Kumbuka Moses wakati wanapigana vita kuelekea Nchi ya ahadi, Kuna wakti vita ilikuwa kali na Mungu aliamua kusimamisha jua lisizame, na ndipo mwaka mmoja ukawa mfupi na mwingine mrefu.
 
Back
Top Bottom