McLaren
JF-Expert Member
- Feb 19, 2025
- 889
- 2,863
Wakuu,
Kwa aliyeelewa maelezo ya shahid naomba anieleweshe. Kajikanyaga mno
Lissu alimtaka shahidi aonyeshe kama baadhi ya kauli alizodai zilisemwa kijiweni kwao ikiwemo madai kuhusu Chadema kuzuia uchaguzi, polisi kuiba kura na majaji kuwa vibaraka wa CCM zilikuwa zimeandikwa kwenye maelezo yake ya polisi, shahidi alikiri mara kadhaa kuwa maneno hayo hayapo kwenye maelezo yake.
=================
Mhe. Lissu: Naomba sasa shahidi apatiwe kielelezo D10.
Mhe. Lissu: Umeieleza Mahakama kuwa pale kijiweni kuna watu wengi ikiwemo madereva bajaji na wenye maduka ya vitu vya nyumbani
Shahidi wa kificho P7 : Kweli
Mhe. Lissu: Sasa tuoneshe kwenye hicho kielelezo hayo maneno yapo?
Shahidi wa kificho P7 : Hayapo.
Mhe. Lissu: tar. 03/04 mlikuwa mnazungumza mazungumzo ya kawaida na kuna mtu akaibua mazungumzo mengine kuhusu Chadema kuzuia Uchaguzi.
Shahidi wa kificho P7 : ndio
Mhe. Lissu: haya nioneshe yapo wapi?
Shahidi wa kificho P7 : hapa imesema alianzisha lakini mtu yani
Mhe. Lissu: Maneno yapo au hayapo?
Shahidi wa kificho P7 : Hayapo.
Mhe. Lissu: Tena watakinukisha mbaya. Yapo au hayapo kwenye maelezo yako.
Shahidi wa kificho P7 : Watakinukisha.
Mhe. Lissu: swali langu umesema hayo maneno yalisemwa na mtu mmoja?
Shahidi wa kificho P7 : Hapana.
Mhe. Lissu: Ahsante. Sasa umesema pia huyo mtu mmoja akasema Polisi wanaiba kura hata ukienda mahakamani majaji ni vibaraka wa CCM
Shahidi wa kificho P7 : Ni kweli
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kama hayo maneno kuhusu majaji yapo?
Shahidi wa kificho P7 : hayapo.
Mhe. Lissu: Je kwenye maelezo yako polisi uliandika kuhusu polisi nao kuiba kura
Shahidi wa kificho P7 : Hayapo.
Mhe. Lissu: Je umetaja tume ya uchaguzi hata mara moja kwenye maelezo yako Polisi?
Shahidi wa kificho P7 : Sijataja.
Mhe. Lissu: Je kwenye maelezo yako umetaja uchaguzi wa mwaka 2024 hata mara moja?
Shahidi wa kificho P7 : Hamna.
Mhe. Lissu: Ulisahau ulichoandika polisi?
Shahidi wa kificho P7 : Nilikuwa naandika maelezo sio kitabu.
Mhe. Lissu: Umesema tukiwa tunaendelea na mabishano nilipata hamasa sasa hayo maneno kuwa ulipata hamasa kama yapo kwenye maelezo yako Polisi.
Shahidi wa kificho P7 : hayapo.
Mhe. Lissu: Unasema uliingia youtube kwa kutumia simu janja. Yako wapi kwenye maelezo yako ya polisi hayo nayo?
Shahidi wa kificho P7 : Niliingia youtube maana yake nilikuwa na simu
Mhe. Lissu: huwezi kuingia kwa kutumia Computer?
Shahidi wa kificho P7 : Mimi sina Computer
Mhe. Lissu: Sasa ndio ujibu swali langu kuwa ulisema uliingia kwa kutumia simu?
Shahidi wa kificho P7 : Sijataja.
Mhe. Lissu: Umesema uliingia kupitia Channel ya Jambo sasa tuoneshe hayo kwenye maelezo yako.
Shahidi wa kificho P7 : Hayapo.
Mhe. Lissu: unasema ulishitakiwa kwa kufanya fujo. Tuoneshe hilo nalo kama lipo?