Features za kuvutia kwenye simu za Xiaomi

Features za kuvutia kwenye simu za Xiaomi

View attachment 2526578
Simu za Xiaomi zina features nyingi za kuvutia bila kupoteza muda naanza direct kuonesha features hizo

1. Hypercharging Ability
Xiaomi anatumia technology yake ya Xiaomi Hypercharging technology inayokuwezesha kuchaji simu yako kutoka asilimia 0 Hadi 100 kwa dakika 15 hadi 20 tu.
ili kufanya hypercharging isiharibu betri Xiaomi ameinclude features 34 kwenye battery, circuit na charger ili kuendelea kuwekea betri katika hali ya usalamaView attachment 2526550

2. App Lock
Simu za Xiaomi zinakuja na feature ya App Lock inayokuwezesha kulock apps unazozitaka kwa kutumia fingerprint scanner au face unlock.
View attachment 2526552

3. Horizontal/ Vertical Recent Apps
Tofauti na ilivyo kwa simu nyingi ambazo Recent apps zimekuwa arranged horizontally simu za Xiaomi zinakiwezesha kuarrange apps zako kwa njia zote mbili vertically au horizontally View attachment 2526555View attachment 2526556

4. Back tap
Feature hii inakuwezesha kuaccess tools kama Camera, torch, calculator, Google Assistant na Silent Mode kwa kubonyeza nyuma ya simu yako mara mbili au mara tatu.View attachment 2526558

5. App Volume control
Hii feature inakuwezesha kuwa na volume tofauti kwenye application tofauti tofauti. Kwa mfano unaweza kuset sauti kubwa YouTube, sauti ndogo Instagram na sauti ya wastani TikTok badala ya kuwa na sauti standard kwa apps zote.View attachment 2526560

6. Super Macro shots
Feature hii inasaidia kuboost uwezo wa kamera kupiga Macro shots na kufanya macro shots ziwe na ubora wa hali ya juu.View attachment 2526561

7. Clone Mode on Camera
Hii ni mode inayokuwezesha kuongeza clones za object unazozipiga picha. Kwa mfano ukimpiga picha mtu mmoja unaweza ku-multiply wakatokea wawili au zaidi.View attachment 2526562

8. Three-finger slide screenshots
Hii ni feature inayokuwezesha kupiga screenshots kwa kuslide down vidole vyako vitatu kutoka juu ya display hadi chini. Hii ni rahisi zaidi kuliko kutumia volume down and power button kupiga screenshots.

9. Second Space
Hii ni feature inayokuongezea phone layout nyingine kwenye simu yako. Feature hii ni nzuri sana, ni kama unatumia simu mbili tofauti ndani ya simu moja. Unaweza kuitumia kutenganisha apps zako za ofisini, au za entertainment na kuzitumia kupitia Second Space ambayo itahitaji password yako ili kuingia Second space.
View attachment 2526567

10. Tones of Animated Wallpapers
Simu za Xiaomi zinakuja na live wallpapers nyingi tena ni za bure. Zipo nyingi yaani kuchagua ushindwe wewe tuView attachment 2526571

Hapa nimeanza na features kumi tu lakini features zipo nyingi sana. Nitaendelea nazo hapo chini kwenye hiihii thread.
Je zina support Google Camera?
 
Hivi hii picha ya simu uliyotumia kwny maelezo yako ni simu gani? Nmeipenda hyo display yake!
Nimepost simu nyingi sijajua ni ipi unaiulizia
Ila kama ni hizi simu mbili basi
Hii ya kushoto ni "Xiaomi 12 Pro"
Hii ya kulia ni "Xiaomi 12"
JamiiForums-1493441962.jpg
 
Natumia redmi note 10 pro
Hivi inakuwaje unapiga picha inatoa quality nzuri
Unataka ku upload mfano whatsap status inaonyesha iko low quality iko na blur!?
Nadhani hiyo ni shida ya WhatsApp, sio simu. Ukipost picha kwenye WhatsApp status inapungua quality
Kama tu humu JF ukipost picha inapungua quality
 
Sasa ni mwaka wa tano nilisha mkimbia Mkorea. Nipo huku kwa hisani ya CHIEF MKWAWA
Alinifungua akili. Sijawahi kujuta nilianza na Redmi Note 7 Pro na sasa nipo na Redmi Note 10 Pro
Vp ukaaji wa betri wa hyo smu? Ikiwa data on inaweza kumaliza saa 24? Na camera yake vp iko vzuri?

NB; Huyo uliem-quote sio chif mkwawa wa tech forum. Huyu chif mkwawa wa tech forum anaandikwa hivi Chief-Mkwawa
 
Vp ukaaji wa betri wa hyo smu? Ikiwa data on inaweza kumaliza saa 24? Na camera yake vp iko vzuri?

NB; Huyo uliem-quote sio chif mkwawa wa tech forum. Huyu chif mkwawa wa tech forum anaandikwa hivi Chief-Mkwawa
Ina kaa na charge masaa ya kutosha. Pia hata hiyo Redmi Note 7 Pro hadi leo nipo nayo. Nisipo washa data inakaa na charge zaidi ya siku 5. Hawa jamaa wapo vizuri. Pia kuisha kwa charge kunategemea matumizi.
 
Hiyo option namba 27 & 28 kwenye Redmi Note 10 Pro sijaiona.
 
Hiyo option namba 27 & 28 kwenye Redmi Note 10 Pro sijaiona.
Kuna baadhi ya features zipo kwenye flagship zao au kwenye latest MIUI mfano MIUI 13 na MIUI 14
 
Wadau ntapata wap battery original za redmi note 8 , nilinunua moja juzi kat kariakoo halinA ata siku tatu linazima likifika 30%
 
Back
Top Bottom