kovai tamil taiga
JF-Expert Member
- Sep 28, 2013
- 1,571
- 2,192
FC Lupopo yadai Yanga imewadhulumu fedha kwa usajili wa Twite.Yanga walitakiwa kulipa dola 15, 000 kama wamemuongezea mkataba Twite lakini hawakufanya hivyo!
"Tutasonga mbele hadi FIFA".
Dawa ya deni ni kulipa tu!!
"Tutasonga mbele hadi FIFA".
Dawa ya deni ni kulipa tu!!
UONGOZI wa Timu ya FC Lupopo ya Congo, umewasilisha malalamiko yake, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuwa wanaidai Yanga Dola 15,000 za mauzo ya mchezaji Mbuyu Twite.
Katibu Mkuu wa FC Lupopo, Constantine Kabika, alisema jana jijini Dar es Salaam, kuwa madai yaliyowasilisha TFF ni ya fedha za mauzo ya mchezaji Mbuyu Twite, ambaye alisajiliwa na Yanga mwaka 2012 akitokea timu yao.
Alisema, katika usajili wa awali, walikubaliana na Yanga kupata asilimia kadhaa ya kila wanapoingia mkataba na mchezaji huyo au kumuuza timu nyingine, kwa kuwa wao wana mkataba wa maisha na mchezaji huyo.
Alisema, awali Yanga walipomsajili mchezaji huyo, klabu hiyo ilipata Dola 20,000 na kusainiwa na rais wa klabu hiyo Victor Kasongo Agosti 5, 2012.
Alisema, hivi karibuni klabu hiyo imeingia mkataba mwingine wa mwaka mmoja na mchezaji huyo na wao katika mgao huo walitakiwa kupewa dola 15,000.
Tulipowafuata Yanga kuwadai fedha hizo wamekuwa wakitusumbua, juzi Seif Magari alituambia twende ofisini kwake matokeo yake ametugandisha pale baadaye tunaambiwa alikuwa safarini Zanzibar, alisema Kabika.
Alisema, Katibu wa Yanga, Beno Njovu, juzi aliwaambia watapewa dola 5,000 kwa mujibu wa Abdallah Bin Kleb, lakini wao wamekataa.
Alisema, endapo hawatafikia mwafaka na TFF, watapeleka suala lao katika Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), kuomba mchezaji huyo afungiwe.
Uongozi wa Yanga kupitia Ofisa Habari wake, Baraka Kizuguto, ulisema kuwa hauna taarifa za madai hayo.
Chanzo: RaiaTanzania