FC Barcelona wanaanza kazi leo!

FC Barcelona wanaanza kazi leo!

Nipo Mkuu,nimeloa ndembendembe.Lakini,Barcelona wameonesha kiwango kizuri. Na 'wamenyimwa' penati

Aaah Mkuu! Nakuheshimu sana ila hizi comments zako zinanipa wasiwasi, kiwango gani wameonesha pamoja na kupangiwa kikosi cha pili?
 
Leo mnamo tarehe 2/3/2013 saa kumi na mbili jioni,FC Barcelona wataanza kazi yao.Baada ya kubezwa,kudharauliwa,kuonekana hawafai,kuonekana kiwango kimeporomoka na mambo yafananayo na hayo,Barcelona wataanza kuwaonesha kiwango chao halisi Real Madrid watakapopambana nao uwanjani Santiago Bernabeu.

Wakisheheni kila aina ya kipaji cha soka,Barcelona walipokea kebehi za kutosha baada ya kupigwa kumbo mara mbili na AC Milan kwa kuzabwa mabao 2-0 na baadaye kuonja shubiri ya mabao 3-1 kutoka kwa Real Madrid siku chache zilizopita. Leo wataanza kazi rasmi ya kuziba midomo ya wakejeli wao kwenye mechi ya La Liga.

Wataonesha kuwa wana plan B na hata C ya ushindi. Kila atakayekuja mbele yao,kuanzia na Real Madrid,atakumbana na kiwango cha hali ya juu cha Barcelona. Wapo watakaoishinda Barcelona na kuifurusha kwenye michuano mbalimbali.Lakini,wataishinda Barcelona ya kweli.

Muda wa kazi ni sasa!

NB: Mimi ni shabiki wa Yanga na AC Milan lakini ninayependezwa na kiwango cha Barcelona.

Real Madrid watakuwa uwanjani bila Ike Casias pamoja na Angel Di Maria wakati Barcelona watamkosa Xavi Hernandes

cc Gang Chomba Mourinho na wengineo

haaaahaaaahaaaa shem n u kamsabikie lulu atuna mashabikli wa YANGA KAMA WEWE
 
Aaah Mkuu! Nakuheshimu sana ila hizi comments zako zinanipa wasiwasi, kiwango gani wameonesha pamoja na kupangiwa kikosi cha pili?
Lakini hata Barcelona si walianzisha kikosi cha pili Mkuu?
 
Kuna watu walidai kuwa Pep Guardiola hakuwa na kazi yeyote pale na kwamba Barcelona ilitengenezwa na Ridjkaard kiasi kwamba hata Julio wa Coastal Union akipewa Barcelona itashinda tu.

Haya tunayoyaona sasa yakitokea ni matokeo ya timu kukosa kocha. Kama Tito Villanova ataendelea kukosekana miezi mingine miwili hata ubingwa wa ligi uko mashakani.

Anayeifunga Barcelona kwa sasa hana sababu ya kujisifu saaana, HAINA COACH
 
Umenena vyema sana Mkuu
 
Sisi Yanga FC ya Jangwani tunaomba mechi na Barcelona
 
Kuna watu walidai kuwa Pep Guardiola hakuwa na kazi yeyote pale na kwamba Barcelona ilitengenezwa na Ridjkaard kiasi kwamba hata Julio wa Coastal Union akipewa Barcelona itashinda tu.

Haya tunayoyaona sasa yakitokea ni matokeo ya timu kukosa kocha. Kama Tito Villanova ataendelea kukosekana miezi mingine miwili hata ubingwa wa ligi uko mashakani.

Anayeifunga Barcelona kwa sasa hana sababu ya kujisifu saaana, HAINA COACH

Pole Mkuu, msije tu mkasema Mourinho kamroga Villanova, Juventus imecheza muda gani without Conte?
 
Back
Top Bottom