Ryzen
JF-Expert Member
- Dec 6, 2012
- 7,301
- 8,693
HIZI NDIO CLUB ZENYE MAKOMBE MENGI ULAYA.
5.Juventus. Msimu huu walionekana bora sana na walitabiriwa na wengi kwamba huenda wangeweza kuchukua ubingwa wa Champions League lakini wakafungwa na Real Madrid. Juventus ndio klabu inayoongoza kwa mafanikio nchini Italia kwani wameshashinda Serie A mara 33 wakashinda Italian Cup mara 12 na Italia Super Cup mara 7,Champions League mara 2,Europa League mara 3 na kombe la washindi mara moja,Uefa super cup mara mbili,klabu bingwa dunia mara mbili na kuwafanya jumla kuwa na makombe 62.
4.Manchester United. Hii ndio klabu inayoongoza kwa mafanikio nchini Uingereza ikiwa imeshashinda vikombe 20 vya ligi kuu nchini Uingereza huku wakiwa wamebeba Fa mara mara 12, vikombe vya ligi mara 5 na mara 21 wakibeba ngao ya hisani,kombe la washindi mara moja,super cup mara 1,intercontinental cup mara 1,klabu bingwa dunia 1 na makombe makubwa ya Ulaya wameshashinda mara 4 huku mwaka huu wakibeba kombe la Europa ambalo walikuwa hawajalibeba kwa siku nyingi na jumla pamoja na makombe ya vilabu vya dunia na mabara United wameshinda vikombe 66.
3.Bayern Munich.Wana vikombe vya Bundesliga mara 27 huku wakiwa na vikombe vya ligi ya Ujerumani mara mara 6,German Cup mara 18, German Super Cup mara 5, nje ya Ujerumani klabu hii imeshashinda makombe ya Ulaya mara 5,Intercontinental cup mara 2 huku wakiwa wameshinda kombe klabu bingwa dunia mara moja, kiujumla klabu hiyo ya Ujerumani imechukua jumla ya makombe 67 hadi sasa.
2.Real Madrid. Wamefanikiwa kutetea kombe la Champions League na hiyo ikawapa kombe hilo kwa mara ya 12 ya makombe ya ya Uefa, Uefa super cup mara 3,klabu bingwa dunia mara 2, La Liga mara 33, Copa Del Rey mara 19, 9 Spanish super cup,intercontinental cup mara 3,Spanish League Cup 1 na Europa 2 hii ikiwapa jumla ya makombe 84.
1.Kama mpira ni makombe baasi Barcelona ndio klabu bora barani Ulaya kwa sasa kwani ndio klabu inayoongoza kuchukua makombe mengi ulimwenguni kuliko klabu nyingine yoyote, wameshashinda ubingwa wa La Liga mara 24,Spanish Cup 29,Spanish Super Cup mara 12,Spanish League Cup mara 2,klabu bingwa dunia mara 3, na mwaka 2009 walishinda makombe 6,makombe 5 ya Ulaya,kombe la washindi mara 4,Uefa super cup mara 5 lakini jumla Barcelona wana makombe 87.