Fatma Karume: Kwa mujibu wa Katiba, ibara ya 138(1),Rais hana mamlaka ya kutuamlia kodi hata kama anaipunguza

Magufuli ana nia njema kabisa , kafanya haya kwa dhumuni la kuwaletea watu maendeleo na kuinua vipato vya wananchi. hata mlalamike kiasi gani, Magufuli katatua tatizo ambalo kimsingi lilikuwa kubwa. nyie mnaosema Magufuli kavunja sheria, hivi mnadhani Rais Magufuli akipeleka muswada huo wa marekebisho wa sheria bungeni , hautapita kuwa sheria? ?magufuli alichofanya ni kupunguza mchakato wa mabadiliko hayo ambayo ungegubikwa na rushwa na ufisadi
Kumbe lazima atoe rushwa kwa wabunge ili apitishe sheria anazotaka!!!
 
Wizara ya mambo ya nje iliwatetea mashoga pia,na kwa niaba ya serikali ikasema itaheshimu mikataba ya kuwalinda waliyoingia!

jifunze kutofautisha kati ya serikali na mtu. serikali si mtu bali mtu ni serikali nadhani umenielewa kwa hili.
 
Huyu dada kuna kitu hakipo sawasawa kichwani. Fatilieni maisha yake mtanielewa. Hapa yeye haoni kuwa jambo hili ni kwa maslahi mapana ya nchi yetu.

Hata kama mtu humpendi hekima yako itapimwa pale utakapoona jambo lina manufaa kwa Tz ukapongeza au kama kiburi ni kikubwa kaa kimya.

Walamba viatu vya mabeberu tunawajua hamtaikwamisha Tanzania Mpya. Mwacheni Rais Magufuli afanye kazi. Wanyonge tunamuelewa. Wewe umekulia Ikulu Znz umesoma shule za nje kwa mabeberu; hujui shida yoyote ya mtu mnyonge leo utamteteaje?. Hebu tupishe ukooo..!
Wenyewe kila kitu ni kupinga tu hata kama kinamnufaisha mnyonge...tumewachoka na siasa zenu na kama kuna mtu hajafurahishwa na kauli ya Rais anaweza akahama nchi sio lazima aishi Tanzania
 
Mwambien atulie,rais anajua anachokifanya
Rais anaongoza kwa mujibu wa katiba na sheria sio kwa mujibu wa anavyojua yeye vinginevyo itakuwa vurugu kama kila rais atataka kuongoza kwa jinsi anavyotaka yeye. Vinginevyo hakuna haja ya kuwa na katiba na sheria za nchi kama rais ndiye atakuwa ni katiba na sheria.

Na hili ndilo tatizo kubwa la rais wetu. Ameapa kuilinda na kuiheshimu katiba lakini baada ya hapo anafanya na kuamua jinsi anavyotaka yeye matokeo yake anajikuta kwenye misuguano mikubwa na wapinzani na taasisi za kimataifa. Acheni kutetea uvunjaji wa sheria na katiba
 
jifunze kutofautisha kati ya serikali na mtu. serikali si mtu bali mtu ni serikali nadhani umenielewa kwa hili.
Mtu hawezi kuwa serikali,watu ndio serikali!Huwezi kuwa na serikali bila watu,kwahiyo hauko sahihi unaposema mtu ni serikali!
 
Kama akipunguza na kutoa ahueni kwa wananchi tutamshukuru na kumuunga mkono, tunachohitaji ni maisha nafuu, tunamruhusu aamue tu.

Bunge lenyewe ndo hili lililopitisha 25% mafao kwa waastafu, si afadhali aamue tu mwennyewe, kama wabunge hawapo kutetea wananchi kwa nn tuwaamini?

Tuacheni propaganda watanzania tunahitaji kupata maisha nafuu, hatuhitaji kufahamu nani kaamua so far wananchi wanafaidi.
Sasa aliyeleta mswada wa hiyo sheria si serikali ya magufuli
 
Hayo ni maelezo ya Raisi wa TLS kupitia mtandao wa twitter ambapo ameweka/ameambatanisha na kifungu husika cha katika ku-support maelezo yake.

Tweet yake inasomeka hivi:

Ibara 138(1) ya Katiba inasema hakuna kodi yeyote itayetozwa bila ya kupitishwa kwa mujib wa sheria iliopitishwa na Bunge au kwa mujib wa taratibu ya ya sheria iliyopitishwa na Bunge. Rais hana mamlaka kutuamulia kodi yetu hata kama anaipunguzi
@MagufuliJP . Linda Katiba please.
Mungu mbariki Fatuma Karume .
 
Tatizo kajigeuza kuwa ndie katiba ya nchi.

Na ndo maana hataki kusikia MCHAKATO WA KATIBA PENDEKEZWA iliyokuwa imepitishwa na BMK 2014!!
Wakti swala la Katiba mpya liko kwene ILANI ya CCM inashangaza Mwenyekiti Magufuli hataki kusikia habari hiyo!!!Kweli yeye ndo amejigeuza KATIBA MPYA...!!!Huyu Rais ni janga kwa Tanzania.
 
Hayo ni maelezo ya Raisi wa TLS kupitia mtandao wa twitter ambapo ameweka/ameambatanisha na kifungu husika cha katika ku-support maelezo yake.

Tweet yake inasomeka hivi:

Ibara 138(1) ya Katiba inasema hakuna kodi yeyote itayetozwa bila ya kupitishwa kwa mujib wa sheria iliopitishwa na Bunge au kwa mujib wa taratibu ya ya sheria iliyopitishwa na Bunge. Rais hana mamlaka kutuamulia kodi yetu hata kama anaipunguzi
@MagufuliJP . Linda Katiba please.
Bunge gani hilo la kupitisha Sheria zenye kumjali Mwananchi !!! Afadhali Rais awe anaamua Mwenyewe kuliko kutegemea chombo kibogoyo.
 
Huyu dada kuna kitu hakipo sawasawa kichwani. Fatilieni maisha yake mtanielewa. Hapa yeye haoni kuwa jambo hili ni kwa maslahi mapana ya nchi yetu.

Hata kama mtu humpendi hekima yako itapimwa pale utakapoona jambo lina manufaa kwa Tz ukapongeza au kama kiburi ni kikubwa kaa kimya.

Walamba viatu vya mabeberu tunawajua hamtaikwamisha Tanzania Mpya. Mwacheni Rais Magufuli afanye kazi. Wanyonge tunamuelewa. Wewe umekulia Ikulu Znz umesoma shule za nje kwa mabeberu; hujui shida yoyote ya mtu mnyonge leo utamteteaje?. Hebu tupishe ukooo..!
Fatma karum si kuwa anakataa swala la kupunguza kodi, na mi sijaona kmpopote kodi ilipopunguzwa. Anajaribu kuelezea kuwa kodi inapangwa na bunge. Aki anachofqnya magufuli ni danganya toto. Hawa machinga kwanza watalia very soon.
 
Hayo ni maelezo ya Raisi wa TLS kupitia mtandao wa twitter ambapo ameweka/ameambatanisha na kifungu husika cha katika ku-support maelezo yake.

Tweet yake inasomeka hivi:

Ibara 138(1) ya Katiba inasema hakuna kodi yeyote itayetozwa bila ya kupitishwa kwa mujib wa sheria iliopitishwa na Bunge au kwa mujib wa taratibu ya ya sheria iliyopitishwa na Bunge. Rais hana mamlaka kutuamulia kodi yetu hata kama anaipunguzi
@MagufuliJP . Linda Katiba please.
Rais Macrons wa Ufaransa mbona kafanya hivyo, najua unaweza sema ni kwa mjibu wa katiba ya ufaransa, ila sijasikia mh. rais Magufuli akiamua kodi ya kulipa alichofanya ni kupendekeza.

Mkumbuke alichofanya angeweza kukifanya gizani pia msione sasa kaleta huku sebuleni tuone wote mnaanza kulalamika.

Kulipa kodi ni uzalendo ila mifumo ya utozaji hizo kodi ni kandamizi lazima ziwe na madaraja.
 
Mtu hawezi kuwa serikali,watu ndio serikali!Huwezi kuwa na serikali bila watu,kwahiyo hauko sahihi unaposema mtu ni serikali!
hujanielewa vizuri niliposema serikali si mtu namaanisha kuwa serikali ni uwakilishi wa kundi la watu na si mtu kama fatuma karume mwenyewe ila mtu ni serikali kama alivyofanya Lugola. lugola kasimama kwa niaba ya serikali ila fatuma kasimama yeye mwenyewe.
 
Kwa maoni yako, Kama sio Mh Rais anajaribu kujikosha kwa wananchi aliowaumiza kwa muda mrefu tangu aingie madarakani ni nn?? Alishindwa nn kulishauri Bunge kupitia upya sheria ya kodi??? Au ndio kusema kwakuwa hakuna chombo chochote chenye mamlaka ya kuhoji tamko au maamuzi ya Mh Rais?? Kama ndivyo alipaswa kuonyesha mfano kwa kufuata sheria na katiba ya nchi.

Hapa Mh Rais kateleza tuache unafiki wa kumshambulia Fatma kwa kuweka wazi Katiba inavyosema. Hapa hatumsaidii kwani kuna siku ataamka na kutenda makubwa zaidi.
Kwahiyo roho zinawauma Rais kushusha kodi?
 
Hayo ni maelezo ya Raisi wa TLS kupitia mtandao wa twitter ambapo ameweka/ameambatanisha na kifungu husika cha katika ku-support maelezo yake.

Tweet yake inasomeka hivi:

Ibara 138(1) ya Katiba inasema hakuna kodi yeyote itayetozwa bila ya kupitishwa kwa mujib wa sheria iliopitishwa na Bunge au kwa mujib wa taratibu ya ya sheria iliyopitishwa na Bunge. Rais hana mamlaka kutuamulia kodi yetu hata kama anaipunguzi
@MagufuliJP . Linda Katiba please.

bado ninasubiri sehemu ambayo atamuunga mkono rais.
 
Kama akipunguza na kutoa ahueni kwa wananchi tutamshukuru na kumuunga mkono, tunachohitaji ni maisha nafuu, tunamruhusu aamue tu.

Bunge lenyewe ndo hili lililopitisha 25% mafao kwa waastafu, si afadhali aamue tu mwennyewe, kama wabunge hawapo kutetea wananchi kwa nn tuwaamini?

Tuacheni propaganda watanzania tunahitaji kupata maisha nafuu, hatuhitaji kufahamu nani kaamua so far wananchi wanafaidi.
Unafahamu sheria mpaka inapelekwa bungeni kupitishwa huwa inaanzia wapi?.Hyo sheria ya mafao ilitokea kwa Rais ndo ikaenda bungeni,huwezi kuwalaumu wabunge pekee kwa kuipitisha alafu ukamwacha yule aliyewapelekea huo mswasa waupitishe.
 
Alichofanya raisi ni kwa manufaa ya taifa tena sana lakini alitakiwa akipeleke Bungeni ili kipitishwe kama njia mojawapo ya mapato sasa mfano kama mtu akikamatwa amekataa kutoa hiyo 20,000 kwa ajili ya kitambulisho cha raisi atahukumiwa kwa sheria ipi? (wapo ambaoa watashindwa kukilipia) dada wa TLS ameangalia mbele zaidi maana kitu kama hicho kinatakiwa kiwe cha kudumu na siyo cha mpito maana akiondoka Jiwe ina maana nacho kinakufa
 
Huyu dada kuna kitu hakipo sawasawa kichwani. Fatilieni maisha yake mtanielewa. Hapa yeye haoni kuwa jambo hili ni kwa maslahi mapana ya nchi yetu.

Hata kama mtu humpendi hekima yako itapimwa pale utakapoona jambo lina manufaa kwa Tz ukapongeza au kama kiburi ni kikubwa kaa kimya.

Walamba viatu vya mabeberu tunawajua hamtaikwamisha Tanzania Mpya. Mwacheni Rais Magufuli afanye kazi. Wanyonge tunamuelewa. Wewe umekulia Ikulu Znz umesoma shule za nje kwa mabeberu; hujui shida yoyote ya mtu mnyonge leo utamteteaje?. Hebu tupishe ukooo..!
Kila kitu kinaenda kwa utaratibu uliowekwa,na utaratibu wenyewe ndio katiba,sasa hata kama anania nzuri alitakiwa afanye mchakato wa kurekebisha hizo sheria na sio kutoa matamko.
 
Back
Top Bottom