Fatma Karume: Kwa mujibu wa Katiba, ibara ya 138(1),Rais hana mamlaka ya kutuamlia kodi hata kama anaipunguza

Magufuli ana nia njema kabisa , kafanya haya kwa dhumuni la kuwaletea watu maendeleo na kuinua vipato vya wananchi. hata mlalamike kiasi gani, Magufuli katatua tatizo ambalo kimsingi lilikuwa kubwa. nyie mnaosema Magufuli kavunja sheria, hivi mnadhani Rais Magufuli akipeleka muswada huo wa marekebisho wa sheria bungeni , hautapita kuwa sheria? ?magufuli alichofanya ni kupunguza mchakato wa mabadiliko hayo ambayo ungegubikwa na rushwa na ufisadi
Hawa watu ni wapuuzi sana.Sielewi kama kuna kitu serikali inaweza amua ikashindwa. Huyo anayelilia iende bungeni hana lolote la maana anaweza badilisha huko bungeni. Kama sheria ya mafao imepita huko bungeni na ni unyonyaji kwa wananchi hii ingeshindwa nini kupita?Kama kila sheria inayopelekwa huko bungeni ni lzm ipite kuna umuhim gani wa kujadl kitu ambacho tayar kina majibu?
 
Huyu mwanamke tayari amekosa uhalali wa kiweledi wa kuhoji mamlaka, taasisi, mtu/watu wanapokwenda kinyume na katiba na sheria za nchi kutokana na mwenendo wake ambao haueleweki siku za hivi karibuni kwa kutetea mambo ya kiboya.

Uchaguzi uitishwe haraka tu, atafutwe mtu mwingine apewe hiyo nafasi aweze kuitumikia kwa busara na hekima....

Huyu mama ni msomi but kichwani hayupo sawa kulingana na sheria, tamaduni mila na desturi zetu watanzania
 
Huyu dada kuna kitu hakipo sawasawa kichwani. Fatilieni maisha yake mtanielewa. Hapa yeye haoni kuwa jambo hili ni kwa maslahi mapana ya nchi yetu.

Hata kama mtu humpendi hekima yako itapimwa pale utakapoona jambo lina manufaa kwa Tz ukapongeza au kama kiburi ni kikubwa kaa kimya.

Walamba viatu vya mabeberu tunawajua hamtaikwamisha Tanzania Mpya. Mwacheni Rais Magufuli afanye kazi. Wanyonge tunamuelewa. Wewe umekulia Ikulu Znz umesoma shule za nje kwa mabeberu; hujui shida yoyote ya mtu mnyonge leo utamteteaje?. Hebu tupishe ukooo..!
Kuna taratibu za kuendesha nchi na ndio maana kuna katiba na Legislative Acts, kanuni nk. Hivyo vyote haviwezi kuwa compromised tukatumia hizo mnazoita busara za mtu mmoja na ndio maana kunakuwa na Checks and Balances.

Hii tabia ya kumuachia mtu kuvunja katiba ndio matokeo yake tunatengeneza akina Mobutu wengine wa kutuibia na kuiacha nchi ktk ufukara wa kutupwa.

Maamuzi yoyote yanayoathiri maslahi mapana ya nchi lazima yaamuliwe na bunge hata kama ni Rubber Stamp kama hili la kwetu hivyo kwa hili Shangazi yuko sahihi kabisa na wanaompinga ni wale walamba buti wa sasa ambao hawana maana kabisa.
 
hujanielewa vizuri niliposema serikali si mtu namaanisha kuwa serikali ni uwakilishi wa kundi la watu na si mtu kama fatuma karume mwenyewe ila mtu ni serikali kama alivyofanya Lugola. lugola kasimama kwa niaba ya serikali ila fatuma kasimama yeye mwenyewe.
"kwa niaba ya" ndio cha maana!
Nways Fatma ana point,nchi lazima iongozwe kwa mujibu wa sheria na taratibu tulizojiwekea!
 
Huyu dada kuna kitu hakipo sawasawa kichwani. Fatilieni maisha yake mtanielewa. Hapa yeye haoni kuwa jambo hili ni kwa maslahi mapana ya nchi yetu.

Hata kama mtu humpendi hekima yako itapimwa pale utakapoona jambo lina manufaa kwa Tz ukapongeza au kama kiburi ni kikubwa kaa kimya.

Walamba viatu vya mabeberu tunawajua hamtaikwamisha Tanzania Mpya. Mwacheni Rais Magufuli afanye kazi. Wanyonge tunamuelewa. Wewe umekulia Ikulu Znz umesoma shule za nje kwa mabeberu; hujui shida yoyote ya mtu mnyonge leo utamteteaje?. Hebu tupishe ukooo..!
Mods tunaomba muweke kitufe cha dislike nilikua nataka nidslike nimeshindwa
 
Huyu dada kuna kitu hakipo sawasawa kichwani. Fatilieni maisha yake mtanielewa. Hapa yeye haoni kuwa jambo hili ni kwa maslahi mapana ya nchi yetu.

Hata kama mtu humpendi hekima yako itapimwa pale utakapoona jambo lina manufaa kwa Tz ukapongeza au kama kiburi ni kikubwa kaa kimya.

Walamba viatu vya mabeberu tunawajua hamtaikwamisha Tanzania Mpya. Mwacheni Rais Magufuli afanye kazi. Wanyonge tunamuelewa. Wewe umekulia Ikulu Znz umesoma shule za nje kwa mabeberu; hujui shida yoyote ya mtu mnyonge leo utamteteaje?. Hebu tupishe ukooo..!
Acha mihemuko mkuu.Jibu hoja.Kwanini Jiwe na serikali yake wasiandae mswada wa mabadiliko wa hiyo sheria na kuipeleka bungeni badala yake anatafuta shortcuts?
 
Hayo ni maelezo ya Raisi wa TLS kupitia mtandao wa twitter ambapo ameweka/ameambatanisha na kifungu husika cha katika ku-support maelezo yake.

Tweet yake inasomeka hivi:

Ibara 138(1) ya Katiba inasema hakuna kodi yeyote itayetozwa bila ya kupitishwa kwa mujib wa sheria iliopitishwa na Bunge au kwa mujib wa taratibu ya ya sheria iliyopitishwa na Bunge. Rais hana mamlaka kutuamulia kodi yetu hata kama anaipunguzi
@MagufuliJP . Linda Katiba please.
Mimi nilisikiliza rais vizuri kwenye ufunguzi wa mkutano wa jana na sikuona wala kusikia mahala popote pale ambapo rais amesema au ku-mply kuwa anataka kutoza kodi.
Tuache kudhalilisha hadhi zetu kwa chuki za kitoto.
 
Katiba halali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iko likizo hadi Jiwe atapoondoka madarakani.

Tuko kwenye kipindi cha mpito kwa miaka 2 hadi 7 ijayo....tujifunze kuishi bila katiba kwa kipindi hiki.
Tuishi kama tumetoka vitan au tumepata uhuru 2015?
 
Hayo ni maelezo ya Raisi wa TLS kupitia mtandao wa twitter ambapo ameweka/ameambatanisha na kifungu husika cha katika ku-support maelezo yake.

Tweet yake inasomeka hivi:

Ibara 138(1) ya Katiba inasema hakuna kodi yeyote itayetozwa bila ya kupitishwa kwa mujib wa sheria iliopitishwa na Bunge au kwa mujib wa taratibu ya ya sheria iliyopitishwa na Bunge. Rais hana mamlaka kutuamulia kodi yetu hata kama anaipunguzi
@MagufuliJP . Linda Katiba please.
Ngoja niigeuze upside down, halafu niisome!
 
atueleze mabadiko ya katiba ya zanzibar yaliyofanywa na baba kama yalikuwa sahihi kikatiba au la maana naona sasa hivi ndio anajitia kukosoa wakati uvunjaji wa katiba uliokuwa ukifanywa nyuma aliunyamazia
 
Kama akipunguza na kutoa ahueni kwa wananchi tutamshukuru na kumuunga mkono, tunachohitaji ni maisha nafuu, tunamruhusu aamue tu.

Bunge lenyewe ndo hili lililopitisha 25% mafao kwa waastafu, si afadhali aamue tu mwennyewe, kama wabunge hawapo kutetea wananchi kwa nn tuwaamini?

Tuacheni propaganda watanzania tunahitaji kupata maisha nafuu, hatuhitaji kufahamu nani kaamua so far wananchi wanafaidi.

Ukisharuhusu hiyo loophole na ikatumika pia kukandamiza maisha ya watanzania, hautakuwa na uhalali wa kulalamika.. Nadhani umenielewa (kama akili zimo).
 
Ndo tatizo la Watanzania badala ya kujibu hoja wanakuja na CHARACTER ASSASSINATION, mpingeni Madam Fatuma Kwa hoja ili kudhihirisha usahihi wa KODI inayotaka kutozwa na Rais
 
Mwambien atulie,rais anajua anachokifanya
Hapo sivyo mkuu, mtu akienda kinyume na katiba ni dalili mbaya kwa mustakabari wa taifa.
Punguzo nimelifurahia sana tena sana na bado nitaendelea kulifurahia, ila sasa wachukue hatua ya kupeleka bungeni marekebisho ya sharia husika ili iwe sheria na isiwe ni hisani ya mtu kujisiskia apendavyo. Vile vile TRA akitupeleka mahakamani tutashindwa kulindwa kisheria.
 
Back
Top Bottom