Fatma Karume: Dk Shein Siyo Rais wa Zanzibar

Ukurunzinza UPI nakosa lipi kwan muda washrin kugombea kikatiba uliisha?na uchaguzi siumefanyka na cuf pia wameambulia kura zao 600 hujamskia bibi YAKE huyo fatma akisema .acheni unyumbu wafikra
 
uyo nae anatafuta kick za kijinga tu akae kmy maigizo yamrisha saiv tunataka maendeleo kwan shein amepindua au amepigiwa kura na wananchi
mkuu wangu ebu msome vizuri kuna mahala kasema"ccm ya Tanganyika ndo inaleta matatizo Zanzibar kwa kuwachagulia viongozi wasiowataka"si ajabu pengine anamaanisha hata hilo unalolisema wewe?
 
Anapata wapi nguvu zakusema? Lazima kuna kitu nyuma ya pazia. Familia yao inakula na kunywa kwa pesa ya serikali sasa mtu kama huyu kuna haja kumchunguza anapat wapi hizo nguvu? Na nikwamasilah yanan anasema hayo?
Kwani uhuru wa kusema kanyang'anywa na chombo gani? Kwanza huyu mama hali pesa yoyote ya serikali amejiajiri. Anayekula pesa ya serikali kwa mgongo wa Karume senior ni yule kokoo aliyesema CUF walipiga kura na mwanaye Karume Rais mstaafu.
 
Babake pia mbona inasemekana nae alicheza faulo? Nidhaniacho mimi ni dadaa katolewa ktk mfumo bila kupenda! Kurithishana kumepitwa na wakati.
Watu kama nyie ni hasara kwa Taifa hili. Ikiwa baba yako alifanya makosa ukae kimya milele ?! Usomi gani huu?
 
Mbona hakupinga Baba yake kuwa Rais,kura za maoni zanzibar Karume alikua wa 5 ikabidi NEC dodoma impitishe kwa kulazimisha kura zipigwe tena na kuachana matokeo ya Zanzibar
kuna mahala anasema ccm ya Tanganyika ndo tatizo ,
 
Wa
na ndio maana wanataka wajitoe icc kwa upuuz huu huu wa kubaka demokrasia
Waache wajitoe ila wasubiri mbabe Fulani uko USA akitoboa na kuingia white house watataman hata case zao zipelekwa huko, michezo hii itaisha tu ya kubaka demokrasia
 
mkuu wangu ebu msome vizuri kuna mahala kasema"ccm ya Tanganyika ndo inaleta matatizo Zanzibar kwa kuwachagulia viongozi wasiowataka"si ajabu pengine anamaanisha hata hilo unalolisema wewe?

SI uongo Shein awamu ya kwanza hakuchukua hata form ya kuomba kugombea urais. Form zilijazwa na wengine yeye akiwa makamu wa Kikwete na akiwa hana hofu na nafasi yake.

Dodoma alikabidhiwa nafasi bila mapenzi na matakwa ya wazanzibari na leo hata wakimchagua mwingine Lumumba hawawezi kuelelewa
 
MJUKUU wa rais wa kwanza wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, Abeid Amani Karume, amepinga hatua ya kumtangaza Dk. Alli Mohammed Shein, kuwa rais Visiwani, anaandika Pendo Omary.

Fatma Amani Abeid Karume, mtoto wa kwanza wa rais mstaafu, Amani Abeid Karume amesema, “Dk. Shein, siyo kiongozi halali wa Zanzibar. Amewekwa madarakani na jeshi na kinyume na Katiba na taratibu za nchi.”

Amesema, “Rais aliyewekwa madarakani na vyombo vya dola, siyo rais wa wananchi. Rais anayewekwa madarakani kwa nguvu za kijeshi na vitisho, hawezi kuwa rais wa wananchi. Anakuwa rais wa majeshi.”

Akiongea kwa sauti ya uchungu na MwanaHALISI Online, Jumatano wiki hii, ofisini kwake, jijini Dar es Salaam, Fatma amesema, “Chama Cha Mapinduzi, kisijidanganye. Zanzibar siyo shwari. Kinachotengenezwa sasa, siyo utawala. Ni muendelezo wa chuki, visasi na uhasama.”

Amesema, “CCM ya Tanganyika, ndiyo inayoiharibu Zanzibar. Wanalazimisha viongozi wasiokubalika na wananchi Visiwani kutawala kwa manufaa yao binafsi.”

Soma mahojiano kamili na mwanasheria huyo mashuhuri nchini, katika gazeti la MwanaHALISI Jumatatu wiki ijayo.

Mwanahabari Huru

Hivi kwani kavile kasema sasa siyo? Rais wa Zanzibar ni Dr. Shein hili mjadala wake ni wa kupotezea muda. Bi. Karume na wengine wenye mawazo kama ya kwake inabidi wajipange na kujiuliza ni vipi walipotea na kusababisha Shein arudi madarakani ili wajipange tena kwa 2020.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom