Kozo Okamoto
JF-Expert Member
- Oct 14, 2013
- 3,391
- 1,546
Da! hakuna usafiri na uogopa kama ndege, ktk maisha yangu ndege nimepanda mara 2 tena kwa matatizotu sivinginevyo, pole sana
Hapo kwenye red, uwe makini na uandishi wako. Natumaini ulikuwa wataka kuandika take-off. Katika wakati ambapo rubani anatakiwa kuchukua maamuzi magumu ni kuahirisha kupaa huku tairi ya mbele imeshanyanyuka, kuahirisha kutua huku umeshakaribia gusa chini na kufanya crash landing.
Kwa hy mkuu haikukaguliwa kabla ya safari??
uje na sato
Mkuu ajali za ndege zinatokea mara ngapi Tanzania ukilinganisha na ajali za magari? ndege ni usafiri ulio salama!
Wakuu,
Naandika hapa huku mapigo ya moyo yapo juu sana. Natokea Mwanza muda huu na flight ya saa8:25 fastjet kurudi Dar. Tumefika kwenye run-way na mbio zikaanza za kutafuta speed ya kupaa, wallahiiii ndege si wakakatiza ghafla juu na si tayari Kasuku (fastjet) yupp kibati... Aiseee zimefungwa break mpaka tumehama ndani pamoja na mikanda kufungwa.
Nashukuru tuko salama na imebidi turudi tutoke nje ya ndege. Tumerudi terminal ndege inakaguliwa
Ilikuwa imekaguliwa lakini kwakuwa imegonga ndege hai wakati inatake off,lazima ifanyiwe ukaguzi mwingine ili kuangalia km haikupata madhara makubwa iweze kuendelea na safari.
Mchawi aliyetuloga watanzania alishakufa...yaani huwa hatujishughulishi na chanzo cha tatizo hadi tatizo litokee. Hapo airport Mianza kuna kundi kubwa la ng'ombe wanalishwa hapo uwanjani, nasikia ni wa meneja wa uwanja,kuna aina flani za ndege viumbe ambao upenda sana kuwa karibu na malisho ya mifugo:nyangenyange,nk pia pamoja na kuzuia kilimo cha mpunga jirani na uwanja kumbe zoezi hilo lililenga hasa kutoa nafasi ya malisho ya mifugo na sasa kuna kilimo cha mbogamboga jirani kabisa na uwanja yote hayo ni kivutio cha ndege pori kuwepo hapo muda mwingi.Uwanja wa ndege Mwanza kuna tatizo la (ndege hai) wengi maana hata ile ndege ya jeshi ilipata ajari kisa ndege hai kaingia kwenye injini ya ndege