FASTJET: My first and last experience

Mbona wengine wanasema hawa jamaa wako poa. Au uko kikazi zaidi???????????????
 

Kaka acha kulinganisha international flight na local.. Mfundishe huyu Tiba ajue kwamba international wanasaidia wanaochelewa but local airline haiwezekani maana wanakodisha madirisha ya check in

Binafsi ni mteja mzuri sana wa fast jet na nitaendelea kuwa mteja wao kwa sababu nimeyakubali mapungufu yao.. Na ukilinganisha Fast jet na precision fast jet wana mapungufu machache kuliko precision.. Muhimu ni kuelewa terms and condition zao vizuri...

Terms za fast jet reporting time ni 3 hours before departure na ukichelewa sana watakusaidia lakini mwisho wa kufanya check in ni 40 minutes before departure.. So kwa kigezo hicho mtoa mada alichelewa check in..

Na wanafanya hivyo sababu Fast jet hawana dirisha la check in kama qatar au emirates. Wao wanachofanya wanaazima dirisha kwa ajili ya check in na ndio maana wanasema dakika 40 before safari hawawezi kusaidia wacherewaji sababu muda wa kukodisha dirisha unakuwa umeshaisha...

Binafsi nilishachelewa Qatar airways nakumbuka ilikuwa tarehe 24/6/2012 pale JNIA na tulifika saa sita kama na nusu hivi wakati ndege inaondoka saa 7 lakini kwa huruma walikuja wafanyakazi wao wakawasha computer za check in, wakatuprintia sticker za bags.. Tukachekiwa airport fasta na tukaingia kwenye ndege na kuondoka na hii iliwezekana sababu wao wana dirisha lao maalumu pale airport hawakodishi na wana haki ya kuwasha computer muda wowote tofauti na fast jet wanaotegemea Swissport..

Ukichelewa local airline imekula kwako lakini ukichelewa international airline unaweza ukaeleweka na kuwashiwa computer for check in maana wanajua wao wanatembea kwa Connections kwenye hubs zao so wakikuacha wanajua utateseka sana kwenye connection maana kuna miji mingine hazina connection flights za kila siku so lazima upandishwe ndege tu ili wakuokoe ukaiwahi connection yako
 
Last edited by a moderator:
Sisi wa mabasi hata getini unafunguliwa mlango unarukia na safari inaunga, huko angani mtanisimulia tuuuuuuuuuuu
 
Sisi wa mabasi hata getini unafunguliwa mlango unarukia na safari inaunga, huko angani mtanisimulia tuuuuuuuuuuu
Umeona eeeh!!!!
Hadi raha. Sisi watanzania tuliochoka tutaendelea na usafiri wetu wa Analogia(Bus) mpaka hapo Digitali(Ndege) watakapokuwa wamejipanga(Ustaarabu) na pia sisi tukiwa tumeandaliwa vema(Kipato).

Na ole wake serikali kama itajaribu kufuta usafiri wa Analogia(Bus) ili tuhamie Digital(Ndege) kilazima.
Patachimbika!!!
 
pole sana inasaidia lakini haina tofauti na daladala
 
Pamoja na hayo yote, bado inavyoonekana wewe sio wa status ya kusafiri kwa Bus.

Nimekusoma kwenye maelezo yako hapo juu, sioni mahali popote ambapo wazo la kusafiri kwa Bus linaweza kujitokeza. Ninaona kabisa ni lazima ungesafiri na Ndege ama Private Car lakini sio Bus kwa namna yoyote ile.

Usafiri wa jamii(Daladala, Bus, Treni, Bodaboda, Baiskeli Mtumbwi, Malori) inaonekana ulishaachana nao zamani sana. Uko juu ndugu na usirudi nyuma.
Hongera ndugu!!!
 
Mkuu inawezekana wewe sio mzoefu wa usafiri wa anga hapa Tanzania. Hao Precision unaowasifia ipo siku utakuja hapa kuwaanzishia uzi wa kuwaponda. Kifupi inategemea tu bahati ya safari ya siku hiyo.

Ni kweli kabisa. Mimi katika maisha yangu sitakaa niwasahau hao Precision ambao niliapa mwaka 2002 kuwa sitapanda ndege zao tena lakini kama walivyosema "Never say Never" siku hizi napanda , kuna siku niitwa kwenye interview Mwanza kutoka Dar Es Salaam ilitakiwa iwe siku ya ijumaa. Kwa kuwa sikutaka mwajiri wangu wa wakati huo ajue nikazusha kuumwa nikaondoka ijumaa asubuhi na kufika mwanza mapema na kuwahi interview saa nne. Nilipanga nirudi jumapili ndege ya jioni. Niliambiwa niwe pale saa moja kabla.

Basi siku ya kurudi Dar niliwahi vizuri kabla hata ndege hiyo toka Dar haijafika. Nilimkuta mzee pale counter ya Mwanza pamoja na binti mmoja na jamaa mwingine ambaye alikuwa kwenye ofisi akicheza Karata kwenye Kompyuta. Nikawapa tiketi wakaniambia nisubiri, basi nikawa sina shaka nikanunua gazetu nikaanza lakini nikashangaa watu wengine wana-check in. Mimi nikaenda tena kuulizia wakaniambia niendelee kusubiri. Baadaye nikaona watu wengi wanaingia nikaenda tena kuulizia wakasema nisubiri kunaofisa anakuja kuongea nami.

Nikasubiri baada ya dk 5 hivi ndege toka Dar ikafika nikaulizia tena ndipo yule dada akaondoka akabaki yule mzee ambaye kazi yake ilikuwa kupima mizigo, ghafla akaja huyo ofisa ambaye alinitaarifu kuwa ndege imejaa kwa kuwa nilichelewa. Kwa kweli nilichanganyikiwa. nikasema nilejeshee fedha zangu nikapande basi. Wakasema eti watakata asilimia 20 nikasema sawa. Wakaniambia nisubiri baadaye wakaja kusema eti nije kesho yake saa nne, ndipo mhasibu atakapokuwa amefika. Kwa kweli nilichukia na kuchanganyikiwa. Baadaye walimwita askari mmoja ambaye alianza kunitishia kuwa angeniweka ndani, nilikuwa na simu (Mshindi) nikajaribu kupigia simu za mamaeneja zilizokuwa kwenye nembo yao ama zilikuwa hazipokelewi ama hazipatikani.

Mama mmoja alinionea huruma ndipo akaja akaniambia kuwa wakati ule ile ilikuwa kawaida. aakaniambia kuwa kuna binti wa mkubwa alipata safari ya ghafla ndiye aliyepewa nafasi yangu, na wakati nasubiri walikuwa wanaangalia kma kuna abiria ataahirisha safari lakini hakupatikana. kwa kuwa usafiori wa basi ulikuwa mgumu wakati huo, na kwakuwa ingebidi nianze safari siku ya jumanne na kufika jumatano (kwani pesa ningepewa saa nne) nilisafiri na dege yao ya jumatatu asubuhi na kufika Dar saa 5 hivi.

Kuna matukio related na hilo yalifuata ambayo yaliniathiri maishani mwangu, yaani kutosafiri kurudi Dar jumapili kama nilivyopanga. Yule binti sikuwahi kumwona tena ila yule mzee (alikuwa na jicho moja bovu akipendelea kuvaa T-shirt nyeupe) aliendelea kuwepo pale mpaka kwenye miaka ya 2006 hivi kwani nilikuwa nikipita pale na kumwona roho yangu ilikuwa inastuka sana.

Hivyo nakubaliana nawe huku Afrika wasafiri hawana haki kabisa.
 
du pole sana mkuu hayo kweli ni majanga ya hatariiiiiii........
 

Japo sishabikii maandamano ila kwa hili hata waje na maji ya kuchubua ngozi lazima niwahi kutetea CHA WOTE.
 
Herg, am I wrong?, ndivyo ilivyo mkuu kwa ufahamu wangu na hii si story ni utaratibu wao.

Tiba

Kwa domestic flight hii ni sawa kwani counter inatakiwa kufungwa 30min kabla ya ndege kuruka. Useme tu ukweli ni kwamba walishauza nafasi yako ndio maana hata ndege ilipozuiwa kuruka hawakukupa nafasi.
 
pole mkuu, siwapendi watu wa rahisi.... maranyingi wanamatatizo
 

Mkuu LUmumbaDAR,

Sina uhakika ni wapi nimesema siwezi kusafiri na bus. Hilo linawezekana na uwa ninafanya hivyo kulingana na mazingira ya safari yenyewe.

Tiba
 
pole mkuu, siwapendi watu wa rahisi.... maranyingi wanamatatizo

Mkuu Elia, na hicho ndicho nimejifunza hasa, rahisi ni ghali!!!!

Tiba
 
Kwa domestic flight hii ni sawa kwani counter inatakiwa kufungwa 30min kabla ya ndege kuruka. Useme tu ukweli ni kwamba walishauza nafasi yako ndio maana hata ndege ilipozuiwa kuruka hawakukupa nafasi.

Mkuu MpangoA, ninaweza kukubaliana na wewe kwamba uenda nafasi yangu iliuzwa na fasta fasta wakafunga counter ili wawe na kisingizio cha kuniacha. Halafu wanakuwa na majibu ya @##$$.

Tiba
 

Mkuu Nyati,

Pole kwa yaliyokupata siku hiyo na asante kwa kutushirikisha bad experience ya Precision Air. Naomba nikubaliane na wewe kwamba wakati mwingine usafiri wa ndege unaweza kuwa kero na hasa wanapoamua kufanya uhuni kama huo waliokufanyia wewe. Kwa bahati nzuri, sijawahi kupata usumbufu wowote kila mara ninaposafiri na Precision. Tatizo langu na Fastjet nimekuwa nikisikia watu wanalalamika na ilikuwa ni bahati mbaya sana kwamba nilipoamua kusafiri nao kwa mara ya kwanza, yakanikuta yaliyonikuta.

Sina hamu nao.

Tiba
 
[
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…