MwanaHaki
R I P
- Oct 17, 2006
- 2,401
- 707
Wakati shirika la ndege la fastjet lilipoanza shughuli zake hapa nchini takriban miaka 5 iliyopita, lilikabiliwa na changamoto nyingi, mojawapo ikiwa kuzushiwa tuhuma nzito, haswa kuhusu usalama wa ndege zake hizo.
Nakumbuka, siku ya kwanza nilipopanda ndege ya fastjet, tarehe 23 Agosti 2013, nilikutana na watu wakarimu sana. Safari kutoka JNIA kwenda KIA ilikuwa nzuri na salama.
Tangu siku hiyo nikawa Mtetezi Namba 1 wa fastjet, niliandika pia tweet nyingi kuisifia fastjet, hata kubuni msamiati wa "fastjetting" na "fastjetter". Mojawapo ya akaunti zangu za Twitter ni @fastjetter1.
Lakini leo nasikitika kusema fastjet " wamebugi", wamechemka vibaya mno.
Wiki iliyopita Mama yangu alinunua tiketi ya fastjet ya kwenda Dar na kurudi akitokea KIA, safari ikiwa Jumamosi, 12 Machi. Leo, Ijumaa, Machi 11, tumejaribu kubadili safari hiyo ili aondoke tarehe 27 Machi na kurudi tarehe 3 Aprili. Tiketi ilinunuliwa kwa gharama ya TZS 213,000, lakini gharama ya kuibadilisha tiketi ikawa TZS 220,000! Hii ni sawa na kununua tiketi nyingine mpya, wala si kubadilisha safari!!!
Nachelea kusema kuna sintofahamu kubwa sana kwa namna fastjet inavyotoa huduma zake. Ilianza vizuri lakini sasa inaharibu. Kama kuna mtu amewadanganya wamiliki wa fastjet kwamba Watanzania wataendelea kuvumilia tabia hii ya kunyanyaswa, amewapoteza njia. Mojawapo ya sababu ya wajasiriamali kuanguka kimafanikio ni kudhani kwamba wateja watanunua huduma au bidhaa kwa bei yoyote ile. Si kweli.
Fastjet sasa mnaelekea kuwa slowjet. Siku zenu zinahesabika.