Fast track diploma ya Nurse-( sasa miaka 2) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fast track diploma ya Nurse-( sasa miaka 2)

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by saitama_kein, May 11, 2011.

 1. saitama_kein

  saitama_kein JF-Expert Member

  #1
  May 11, 2011
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Jamani taifa linakwenda wapi??
  Diploma ya Nurse ilikuwa miaka minne (4) lakini serikali yetu ya awamu ya nne ikapunguza na kuwa miatatu (3) na benchi ya kwanza watamaliza hivi karibuni.
  Kama hiyo haitoshi, sasa wanapunguza mpaka miaka 2??? Kweli afya bora kwa kila Mtanganyika itapatikana hapo??
  (source taarifa ya habari ITV leo tarehe 11.05.2011 saa 2 usiku)
   
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  May 11, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145

  Elimu ya UPE, Vodafasta, na sasa sekta ya Afya! sad!
   
 3. Nicky82

  Nicky82 JF-Expert Member

  #3
  May 11, 2011
  Joined: Mar 14, 2009
  Messages: 939
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wanataka waende sambamba ba ule mpango wao wa kuanzisha zahanati za kata! Baada ya kufanikiwa kuua kiwango cha elimu sasa ni wakati wa kuwaua watu...sidhani kama hawa jamaa wanatumia vichwa kufikiri.
   
 4. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #4
  May 11, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kama wale tu wanaosoma kwa miaka mitano wanakata kichwa badala ya mguu and vice versa is true, hawa wa miaka miwili watakuja ku-prescribe chaki kama panadol! [FONT=&quot]Changing the rules of the forest without changing the monkeys is like painting a cat![/FONT]
   
 5. c

  chetuntu R I P

  #5
  May 11, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 954
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ni upupu mtupu hata hao ma nursing officers wa siku hizi mmmhh. Serikali inaharibu kila sekta, bdo police tu.
   
 6. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #6
  May 12, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Naandika kwa masikitiko kwa uwazi kwa rais wangu mpendwa Jk,jk umefanikiwa kuua elimu kwa uwezo wako wote,umezalisha waalimu mbumbumbu kwa kuwaomba waliofeli form 4 kwa grade ya div4 ndo wawe walimu na mapolisi,matokeo yake walimu wameanza kuleta std wasiojua kusoma wala kuandika/rejea takwimu za Haki Elimu,waliofeli f6 wakafundishe sekondari,na ma polisi waende wa div4 walau pt28 na leo tunaona wasivotumia akili na utashi ktk kutii amri za kuzuia au kuua waandamanaji wa kidemokrasia. Mh.jk leo umeingilia sekta ya afya kwa kupunguza muda wa kutafuta ujuzi wa wauguzi badala yake ufyatue wauguzi nusu watalaamu! Aya mambo hasara yake haionekani wazi kama kwa walimu kupata failed nyingi bali ktk sekta ya afya matokeo yake ni kuongezeka kwa maiti muchwari na kuongezeka kwa wajane na yatima ambapo baadae tutatengeza maombaomba wa kutosha. Mkakati wako labda ni kuona Tanzania imevurugika ukishatoka madarakani! Mh.JK nakuhakikishia kuwa kwa heshima kubwa ya maneno ni kuwa baadhi ya mashirika ya kidini hayotokubali mpango huo wa kuua sekta ya uuguzi.
   
 7. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #7
  May 12, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  <br />
  <br />
  Jamani hebu tuwe realistic kidogo. Hivi ni diploma gani hiyo hapa duniani inayosomwa miaka minne? Mambo mengine ni kupotezeana muda tu. Cha msingi ni kuupanga mtaala vyema na watu wasome muda mfupi. Huu ni urasimu tu. Yaani anayesoma diploma anafanana na mtu wa degree ya engineering! Ah wapi! Labda mtu aje na mawazo ya kwamba kusoma diploma kutafanya wanafunzi wamiss hiki na si kuangalia urasimu wa muda tu!
   
 8. saitama_kein

  saitama_kein JF-Expert Member

  #8
  May 12, 2011
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Diploma ya nurse inatolewa kwa wanafunzi waliomaliza fomu 4 na kufanya vizuri katika mchepuo wa masomo ya sayansi na huwezi kuilinganisha na digrii ya engineering ni kwa aliyemaliza fomu 6...........hapo utaona ni tofauti ya miaka 2!!
  Muda kwa mafunzo ya nurse ni muhimu sana ndugu yangu...wanahitaji muda wa kusoma na kufanya pratical ili siku utakapokwenda kupigwa shindano usije pigwa vibaya na kuishia ku paralysis.....katika hili tuondoe utani..Haya ni maisha na afya za watu!!
   
 9. itnojec

  itnojec JF-Expert Member

  #9
  May 12, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 2,191
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  dunia nzima sijaona nursing diploma ya miaka minne.
   
 10. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #10
  May 12, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  <br />
  <br />
  oh kumbe hapo inakosekana tu certifate ya nursing sijui kama ipo ili mtu aweze kufanya diploma. Hivi kuna form 4 yoyote anayeweza kuwa amefanya vizuri akaenda kusoma diploma ya nursing? Au kufanya vizuri kunaanzia wapi na kuishia wapi? Labda tusome kuanzia sasa diploma ifanywe na form 6 na hao form 4 waanze na certificate kwanza. Jamani tunatatizo kubwa saana la mitaala kuna haja ya kuirekebisha na kuangalia uhalali wa diploma ya miaka minne km kweli kuna hii kitu.
   
 11. mwanaone

  mwanaone JF-Expert Member

  #11
  May 12, 2011
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 635
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 180
  Ndugu zanguni ulimwengu mzima nchi zote zilizoendelea hakuna Diploma inayozidi miaka miwili. Sio Diploma tu hata Advance Diploma inayozidi miaka minne. Hiyo uingereza ambayo ndugu zetu wengi wanakimbilia huko kufata elimu bora wana mpango wakupunguza miaka ya degree exclude medicine kutoka miaka 3 mpaka miwili ili kuwapunguzia wanafunzi gharama.

  Yaani kwa mahesabu miezi ambayo mwanafunzi anasoma kwa kipindi cha miaka 3 ni miezi 15 muda mwingi wanakuwa likizo. Mfumo wa elimu wa Tanzania kuna urasimu wa hali ya juu na nashukuru SERIKALI YA AWAMU YA NNE IMELIONA HILI.

  NURSING DIPLOMA 4 YEARS ULIKUWA NI UPUMBAVU WA HALI YA JUU. JAPO SIJAWAHI WALA SITOUNGA MKONO FORM SIX LEAVER KUWA WALIMU KAMA HAWAJAENDA VYUO VYA UWALIMU.
   
 12. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #12
  May 12, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Sasa tutachomwa sindano machoni.......subirini
   
 13. saitama_kein

  saitama_kein JF-Expert Member

  #13
  May 12, 2011
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Wala si utani ndugu yangu na waathirika wakuu ni mama/ dada zetu na watoto zetu haswa huko pembezoni mwa Tanzania....
   
 14. NgumiJiwe

  NgumiJiwe JF-Expert Member

  #14
  May 14, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Nadhani watakuwa wale waliopata D kwenye Biology,Chemistry na Physics/Maths,manake juu ya hapo na combi ikakubali basi majority wataenda form 5.Kama haya ninayosema ni kweli,basi ilikuwa sawa kabisa kwa diploma ya nursing kuchukua miaka 4.Ukisema waanze na certificate,ndipo wasome diploma nadhani itawachukua muda uleule au hata zaidi.Lakini kikubwa ni kupata wahitimu ambao watakidhi mahitaji yetu na siyo kuiga mifumo ya nchi nyingine ambazo inawezekana tunatofautiana kimahitaji
   
 15. Nditu

  Nditu Member

  #15
  May 16, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 84
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Asante sana Saitama. Mimi pia nasikitika mno kwa kitendo cha serikali kuchakachua kila idara mpaka hii moja iliyokuwa imebaki ya Afya! Kwa kadiri ninavyofahamu Diploma ya Uuguzi kwa miaka miwili haiwezekani na kama tutalazimisha tutazalisha mbumbumbu wasioweza kuhimili Challenges zilizo mbele yao.

  Hapo awali Tanzania ilisifika kwa kutoa wahitimu bora kabisa katika fani hii lakini sasa tunakoelekea kina Kikwete wanatupeleka shimoni kwa sababu za kisiasa. Mimi mwenyewe ni Daktari na mkufunzi wa siku nyingi (Mstaafu) niliyefanya kazi ndani na nje ya nchi hii. Naelewa faida ya kuwaweka wanafunzi chuoni kwa miaka minne kwani mwanafunzi husoma bila presha, hupata muda wa kukielewa na kukifanyia mazoezi anachofundishwa, na anatoka akiwa ameiva.

  Kufananisha elimu inayotolewa na nchi "zilizoendelea" ni kupotosha mada kwani wenzetu wana vitendea kazi bora vya kufundishia na hata wauguzi wao huenda kupambana na changamoto tofauti kabisa na za hapa kwetu ambapo hapa muuguzi ni sharti awe mwelewa, mzoefu na mwenye uamuzi wa haraka na kuchukua hatua.

  Kwa hiyo mimi sikubaliani hata chembe hii ya Form 4 au hata 6 kusoma na kuchukua Diploma ya Uuguzi kwa miaka miwili!
   
 16. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #16
  May 16, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mzee Nditu, Asante saana kwa hoja zako. Mie sina hakika km kukaa na kurudiarudia vitu kwa muda wa miaka minne ndio kunaonyesha competency. vitu vinabadilika ikiwa ni pamoja na maradhi kutokana na mabadiliko ya kimazingira, tiba zinabadilika na mahitaji pia yanabadilika. Kwahiyo kuendelea kupingana na wakati eti sisi wakati ule ilikuwa hivi, ni kuogopa tu changamoto. Unaweza kuniambia hawa wanafunzi wa miaka miwili watakosa nini walichofanya wanafunzi wa miaka minne. Hawa walisoma miaka 4 lakini discpline yao kwa wagonjwa ikoje?
  Kusoma miaka mingi si kuelewa kama unavyotaka kusema ni zaidi ya kupoteza muda tu. Cha msingi ni continous development hasa kwenye fani za uguuzi, personal initiative, vitendea kazi bora, motisha, kutrain watu wenye uwezo nk.
   
 17. mchillo

  mchillo JF-Expert Member

  #17
  May 17, 2011
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 430
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Mwanaone, maelezo yako yanadokeza wewe nimmoja wa wadau watakaonufaika na hiyo training ya Fast Track ambayo kwa kweli si lolote ni uchakachuaji tu. Unasema Diploma ya UUguzi miaka 4 ni upuuzi? Unataka kutushawishi kwamba wahitimu wa miaka 2 unayotaka watakuwa competent sawa na wa miaka 4? Kwa msingi upi wa elimu kama sote tunafahamu jinsi viwango vya elimu vilivyoshuka nchini? zaidi ya nusu ya wahitimu wa vidato vya nne na sita na hata baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu siku hizi hawawezi kujieleza kwa lugha ya kiingereza kwa ufasaha, je, hujui kwamba hiyo ndiyo lugha rasmi kwa kufundishia Uuguzi na Uganga?
  Uuguzi na uganga una terminologies ngumu kufahamika hata kwa wanaoifahamu vema lugha hiyo na zamani wanafunzi waliandaliwa kwa mwaka mzima wakifundishwa pamoja na mengineyo lugha ambayo baadae itakuwa lugha yao rasmi ya kikazi, sasa kwa hii lipualipua ya kina Kikwete unadhani wataupata kweli muda huo? Kisha kulikuwa na mwaka mzima wa Ukunga (Midwifery) ambapo wanafunzi walijifunza kwa vitendo wakikaguliwa kwa karibu kabisa na wakuu wa idara husika na waalimu wao; jambo lililosababisha wauguzi wetu kuonekana competent hata nje ya mipaka yetu, leo hii taifa letu linajivunia wauguzi tele walioajiriwa na kuaminika Afrika Kusini, Botswana, Swaziland na mpaka Canada, Uingereza na Marekani, unadhani hali itakuwa hivyo baada ya zoezi hili? Mnalinganisha eti na nchi zilizoendelea, sisi tumeendelea? tuna zana za kufundishia zilizo sawa na wanazotumia wanafunzi wa Uingereza, Uholanzi n.k.? na tumeangalia vema background ya wanafunzi watarajiwa wetu?
  Vyovyote ilivyo huu ni uchakachuaji na inabidi ulaaniwe kwa nguvu zote. Wamechakachua shule za msingi tukanyamaza, shule za sekondari tumenyamaza, na sasa kwenye sekta nyeti ya afya tunyamaze? Hapana. Nasikia sasa wanachakachua hata kwenye majeshi maana nasikia kuna maofisa wanaoitwa Voda Fasta yaani watoto wa vigogo wanaosukumwa tu mradi wahitimu mafunzo! Nauliza tunakwenda wapi?
  Mungu ibariki Tanzania.
   
 18. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #18
  May 17, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kaka/dada kweli nyie ni wadau katika sekta. Hivi mtu katoka form 6, mnasukuma akasoma diploma ya miaka 4 na mwingine wa hiyo form 6 akasome Degree kuna nini hapo? Unless utuambie kwamba kuwe na specialisation kwenye nurses na I hope zipo midwives etc. Tusiogope mabadiliko labda tuseme syllabus ndio hiyo hapa na kwa miaka 2 hawatasoma vitu hivi hapa ndio mtaeleweka vinginevyo ni mlolongo na likizo ndefu zisizi na tija. Nchi yetu watu wanahitimu umri umekwenda saana na si kwasababu ya ubora wa Wahitimu bali ni complications ya Mtaala. Tukubali mfumo wetu wa Elimu unahitaji mabadiliko kuanzia kwenye contents ya vinafundishwa, walimu wanaofundisha, muda na entry qualifications. Sio fair kabisa kwa mtu kuhangaika diploma 4 years unless iwe part time.
   
Loading...