Idd Ninga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 5,208
- 4,406
FARASI FUNGUA KAMBA.
1)Hauna kichwa farasi,vipi ikutese kamba.
hujatafuta nafasi,mbona kichwa umefumba.
Wa waza chanya na hasi,ama wacheza marimba.
Farasi fungua kamba,hicho kiti karatasi.
2)japo mchana mweupe,vipi kwako kuna giza.
Ulalapo japo lepe,wenzako wakuchunguza.
Tuvuke haya matope,shida tuanze punguza.

3)ukionapo kizito,wenzio wakutawala.
Wakwona kama kitoto,kidogo kilo cha swala.
Wanakupa mkong'oto,kichwani wawa hewala.

4)uifungapo akili,chako kichwa kitalala.
Haimuliki akili,kwanza anza fanya sala.
Hata mkiwa wawili,hata kundi ni mashala.

5)uwayazapo ya nyuma,fikiri sana ya mbele.
Ni wakati kusimama,tuache kuwa kambale.
muda ni sana mapema,twaweza panda kilele.

6)mtaji mbona tunao,tena ndie vichwa vyetu.
Tuje washinda na wao,hii sasa zamu yetu.
Tuwatawale na wao,yawe marifa ya kwetu.

7)kamba hiyo ikatike,sasa muda kuamua.
Na uvivu ufutike,mbele tuanze sogea.
Kesho ije na nicheke,kuona najikwamua.

Shairi:FARASI FUNGUA KAMBA.
Mtunzo:Idd Ninga wa Tengeru
+255624010160.
iddyallyninga@gmail.com