Hadithi ya "Biashara chafu": Na Ntalanda

JosephNyaga

JF-Expert Member
Apr 28, 2014
291
232
BIASHARA CHAFU

Sehemu ya 01

Mwanzo

Nimajira ya jioni ivi, gari aina ya benz nyeusi, inaonekana ikilandalanda maeneo jirani na Benki Kuu ya Taifa hapa nchini (BOT), ndani ya gari hio wanaoneka akina Jonathan, Kenn, Joven, Isack, Paul, Kizito na Mamba, wote wakiwa na karatasi zilizo na ramani ya benki hio. Mida ya saa moja hivi, Jonathan akachukua simu yake ya mkononi alafu akabonyeza namba kadha, kisha akaiweka simu Sikioni
"Jonathan, sasa mnaweza ingia ndani ila hakisheni kila mmoja wenu anavaa kifaa chake cha mawasiliano" aliongea jamaa niliyempigia, nakunifanya nami nitoe amri hio haraka kwa wenzangu "Jamani twenzetuni, kila mmoja ahakikishe amevaa mawasiliano yake" nilizungumza kwa sauti ya juu kidogo.

"Johnathan, wamesema wameshaseti kila kitu tiyari" alizungumza Kenn, huku uso wake ukionyesha wasiwasi sana katika tukio tunalokwenda kulifanya muda mfupi ujao "yaaah, kila kitu wameseti, thus why wamesema tuingie ndani, Sikieni tunadakika thelathini tu za kufanya kazi yetu" Niliongea, kisha kila mmoja akaanza kuvaa nguo za kujisitiri na mambo tuyoweza kukumbana nayo katika kazi yetu tunayoenda kuifanya

Wote tulivyo maliza kujipanga tiyari kwa kazi nzito tunayoelekea kuifanya Katika Benki yetu kubwa hapa nchini, tukashuka ndani ya Gari nakuanza kuelekea usawa na ilipo benki hii, tulivyoifikia ilipo kila mmoja akaelekea njia yake, Hatukutaka kupitia njia kuu ya benki hii kwa sababu ya majukumu tuliyokuja kuyatekeleza ndani humo, uzuri ni kwamba kila mmoja alikua amesoma ramani ya njia atakayo pita.

Mimi binafsi nilipita njia iliyokua nyuma ya benki, katika milango ya dharula waitumiayo wahudumu pindi likitokea tatizo, japo ilikua imefungwa kwa lock maalumu lakini niliweza kupita salama salmini kwasababu mfumo wa mawasiliano wa benki ulikua umekwishwa kuharibiwa na Mkuu wetu wa mawasiliano ambaye ndiye aliyenipa ruhusa ya kuwa tuingie ndani, Mfumo wa mawasiliano wa benki hii uliharibiwa kwa dakika zipatazo arobaini na tano, muda huo wote hakuna mtu ambaye angeweza kutuona, kwakua hata Cctv Camera zilikua hazifanyi kazi kama inavyotakiwa. Kwakua hatukua na muda wa kupoteza nilitembea harakahara mpaka sehemu ya hazina kuu ya Benki hii ya taifa, Macho yangu yalinitoka kama Bundi mara baada ya kuona pesa nyingi mahala hapa, palikua na hela za mataifa tofautitofauti, hela kama dolla, yen, kwacha, uro, shilingi ya hapa nchini nazingine nyingine.

"Tiyari nimeshafika ila wenzangu bado siwaoni?" nilizungumza kwa kutumia kifaa maalumu kinachotuunganisha na mkuu wetu wa mawasilano "Okey, Jonathan hapo ndani ya Hazina mna lidude flani, kubwa hivi nenda hapo utaona kila kitu kisha fwata maelekezo watakuja tu, kwasababu milango waliyopita wao nimeshindwa kuharibu lock zake" alizungumza Mkuu wetu katika kitengo cha Mawasiliano, nami sikufanya makosa nikaliendea dude lilo kubwa humu ndani ya hazina, nakweli maana katika kifaa hicho nikaweza kuona jinsi benki yote ilivyokaa tena nikaona mpaka sehemu walizokwama wenzangu, kupitia kifaa hicho ambacho ni lidude likubwa nikafanikiwa kufungua milango waliyokwama wenzangu.

Kumbe hata hawakuwa mbali, maana nilivyofungua tu milango hiyo nao wakatokeza, kila mmoja wao akashikwa na bumbuwazi mara baada yakuona jinsi hazina ya nchi yetu ilivyopambwa na hela nyingi kiasi hicho
"Jamani tuanze kazi yetu, hatuna muda wa kupoteza hapa" nilizungumza mara baada ya kuona jinsi wenzangu walivyozuba mara baada ya kuona mpunga
"walisema tuchukue zipi? Sasa Mkurugenzi" Mamba aliniuliza swali hilo
"hapa hatuchagui kitu, ila dolla ndio ziwe nyingi" nilimjibu, kisha kila mmoja akachukua begi yake alikolificha, tukaanza kuchukua hela za nchi utafikiri tumeruhusiwa kuzichukua, kila mmoja alivyohakikisha amechukua kiasi cha kutosha akasimama ili kusikiliza utaratibu unaofwata.

"nadhani kila mmoja anaikumbuka vizuri ramani ya njia yake, hivyo basi tutatoka kama tulivyoiingia humu ndani, tunadakika kumi na tano tu humu ndani" nilizungumuza huku nikawa nawaangazia macho yangu, kila mmoja wao alikua haamini kama ndo tunataka tutoke tena bila kutambulika ila mimi kwa uzoefu wangu niliona ni hali ya kawaida tu, ambayo inakwenda kukamika muda mfupi ujao.

Mmoja mmoja akaanza kutoka kuelekea mlango wake aliopitia wakati anaingia humu ndani, nami ndo nikawa wa mwisho nikipitia njia yangu, njia tulizopita wote zilikua ni njia za dharula, ambapo haikuwa rahisi kutambulika. Dakika chache wote tukawa tumetoka ndani ya Benki kuu ya Taifa hapa nchini, tukiwa tumelitia hasara kubwa Taifa letu, tukaelekea mahala ilipo gari yetu, tukaingiza begi zetu zilizojaa pesa, kila mmoja alivyomaliza kuweka tukaanza kupongezana.

"daaah! Yaani hata siamini, kazi njema sena hii jamani" kila mmoja alitamka maneno hayo kwa mwenzake wakati anamkumbutia, Tukiwa hapo nje kwenye gari letu, Tumejidai kwa kufanikiwa kutoka salama salimini ndani ya benki, Mara tukaona defender tano za polisi zikija mkuku mkuku mahala tulipo, jambo lililotuogofywa sana mimi na wenzangu.
ITAENDELEA

BIASHARA CHAFU

Sehemu ya 02

Na Mulabha Ntandala :

Tukiwa tumejidai nje ya gari letu, mara baada ya kutoka nje ya benki salama salimini tukaona deffender tano za polisi zikija mkuku mkuku mahala tulipo, jambo lililotuogofya sana mimi na wenzangu.

"Itakuwa wameshatushitukia mkuu!" aliongea Joven akiwa amejawa na woga sana, nakunifanya nami nifikilie kwa muda kabla sijamjibu
"hamna kitu kama hicho, naona wapo na mishe zao maeneo haya" niliongea kwa kujiamini kidogo, ili kuwaimarisha hawa wenzangu nilio ongozana nao. Kweli bwana deffender hizo zilipita mahala tulipo kwa mwendo uleule wa farasi na sisi tukabaki tukizisindikiza kwa macho mahala zinapoelekea, hali iliyopelekea mimi na wenzangu wote tuwe na furaha ya namna yake

"Jamani hatuna muda wakupoteza hapa twenzetu" niliongea, kisha kukafwatiwa na vitendo,
mmoja mmoja akaanza kuingia kwenye gari letu, namimi nikawa wa mwisho kuingia ndani ya gari, naye dereva wetu bwana Kizito hakuwa na chakufanya zaidi akalitoa gari letu kwa wa fujo eneo hili la benki. Muda mfupi baadaye tulifika makao makuu yetu

Claud White House (Ikulu ya Claud) ndiyo yalikua makao yetu makuu, ambayo yalikuwa yamejificha ndani ya mitaa ya Osterbey jijini dare es salaam, tulipokelewa vizuri sana na mkuu wetu bwana Claud
"vijana wangu leo naona mumefanya kazi nzuri, ndani ya benki ya wahuni" aliongea mkuu wetu bwana claud, huku akionyesha furaha aliyonayo siku hii ya leo

"Ni mambo ya kawaida tu mkuu, subiri mambo yanyooke wewe mwenyewe utafurahi" Nilizungumza maneno haya pindi mkuu aliponipatia mkono wake kunipongeza
"unazidi kunifurahisha Jonathan, naamini tukifanya kazi hii na wewe kwa miaka miwili mbele, nitakua bilionea mkubwa hapa nchini" aliongea claud, kisha akawaita wafanyakazi wake waje kuchukua pesa tulizotoka kuiba benki, wengi wa wafanyakazi wake waliokua ni wasichana warembo mno na wachache wao walikua ni wavulana wadogo ambao bado hawajafunzwa maswala ya wizi ambayo ndiyo mhimiri mkuu wa mkuu wetu claud.

Muda wa saa nne usiku, kila mmoja alitawanyika kwenda kulala katika chumba chake ndani ya jumba hili lililojengwa kwa utaalamu wa hali ya juu, mpaka bosi wetu akaipa jina la Claud House White (Ikulu ya Claud), kwakweli Mr claud hakukosea kabisa kuipa jina hili kwani ukiingia ndani ya jumba hili unaweza ukahisi upo china ama Uingereza, Kila kitu ndani ya jumba hili kinaendeshwa kwa kutumia umeme na kama umeme ukikata kuna jenereta za moja kwa moja zinazohisi kama umeme umekata nakuendelea kuzalisha umeme bila mtumiaji kugundua kitu chochote (Automatic generator).

Geti la nyumba hii limeunganishwa na mashine ambazo zina uwezo wa kutambua gari zote za Mr claud, pindi mashine zikitambua kama gari la Mr claud lipo nje basi geti hujifungua bila ya mtu yeyote kufungua geti hilo, kama sio gari lake basi mashine hizo hutuma taarifa hizo kwenye kitengo maalumu cha mawasilano ndani ya nyumba hii, ambapo kitengo hiki cha mawasiliano hutambua jina la mtu na mtumiaji wa gari husika kisha hurudisha taarifa kwenye mashine kwamba gari lifunguliwe ama lizuiliwe. Kitengo cha mawasiliano huwa na mtu muda wote kwa sababu mawasilano ndio chanzo cha usalama katika shughuli zetu hizi chafu.

Nilifika ndani ya chumba changu nikalala muda wa saa nne na nusu usiku, Usiku huu nililala sana tofauti na kawaida yangu kwasababu niliamka muda wa saa moja na nusu, wakati kawaida yangu ilikua ni kuamka muda wa saa kumi na moja kamili asubuhi, utaratibu huu nilijipangia kwa sababu ya shughuli zangu nyingi ninazozifanya. Nikachukua simu yangu mahala nilipoiweka, nikaiwasha na kufungua mtandao wa kijamii wa facebook

"Hela zapotea kimahajabu benki kuu" kilikua ndicho kichwa cha kwanza cha habari nilichokutana nacho kwenye page kubwa ya Mwandishi mahiri hapa nchini Millard ayo, nikacheka kidogo kwa sababu nilijua yakua wasababishaji wa tukio hilo ni sisi, sikutaka kuendelea tena kusoma habari zilizopo siku hii kwenye mtandao wa facebook hivyo ikanibidi nitoke (nilog out). Nikatoka chumbani kwangu nakuelekea sebuleni ndani ya ikulu hii ya bwana Claud.

Nilishituka kidogo mara baada ya kukuta shughuli mbalimbali zikiendelea sebuleni hapa, nikaangaza macho yangu pande zote za sebule hii nikaona kila mtu yupo bize na shughuli
"Jane kitu gani Kinaendelea hapa ndani?" nilimuuliza binti aliyekuwa mmojapowapo kati ya watu waliopo sebuleni hapa
"Ooooh Jonathan, kumbe hujui? Leo kuna bonge moja la party humu ndani" alizungumza Jane, nakunifanya nitaharuki kidogo
"sherehe ya nini? Tena Jane" nilizungumza kwa mshituko kidogo

"Bosi ameridhishwa na kazi yenu Jonathan ndio maana ameanda sherehe hii" alizungumza Jane, nakunifanya nimshangae Bosi huyu, nikamuaga Jane kisha nikatoka nje ya Ikulu hii ya bwana Claud. Niliwaza sherehe hiyo itakua ya namna gani? Ila sikuipatia picha, nikaamua kuingia ndani ili nikapate kifungua kinywa, muda wa saa saba sikuamini mambo niliyoyaona, yaani sebule ilikua imepambwa kwa namna ya hajabu ambayo ilinifanya nibaki nimeduwa kwa muda.
ITAENDELEA

BIASHARA CHAFU

Sehemu ya 03

Na Mulabha Ntandala :

Muda wa saa saba sikuamini mambo niliyoyaona, yaani sebule ilikua imepambwa kwa namna ya hajabu ambayo ilinifanya nibaki nimeduwa kwa muda. Sebule hii ilipambwa vizuri kwa vitamba mbalimbali na kunakishiwa kwa maua ya rangi tofautitofauti, hali iliyoifanya sebule hii iwe na mvuto wa namna yake
"Jane mambo yenyewe ndiyo haya tena" nilimuuliza Dada huyu huku nikiwa bado naendelea kutizama mandhali ya sebule hii.

"Yaaah Jonathan, vipi? Kwani tumepamba vibaya au" aliuza Jane huku akiwa amepambwa na tabasamu mwanana usoni pake, hali iliyonifanya nami nianze kutabasamu ijapo sikua na hamu ya kufanya hivyo
"mmepamba vizuri sana, ujue nilivyotoka chumbani kwangu nilijua labda nimekosea sebule, hivi mulijifunza wapi? Shughuli hizi za upambaji" nilimuuliza Jane, swali lililomfanya azidi kutabasamu zaidi

"Aaaah Jonathan bwana inaonesha wewe ni mcheshi sana yaani" aliongea Jane huku akiwa anajichekesha chekesha
"Kawaida Jane, ila si unijibu kwanza mwenzio" nilizungumza, huku nikiwa nimeachia tabasamu hafifu
"yaaah tumejifunza humu humu ndani ila kwa kupitia wenzetu waliosomeshwa na Bosi wetu" alizidi kufunguka zaidi mrembo Jane, nakunifanya nami nianze kuongeza vitu ambavyo nilikua sijavijua hapo awali
"sawa bwana maandalizi mema" niliamua kumuaga Jane kwakuwa tiyari macho yalikua yamerizika kutizama mahala hapa, nikawa nasubiria muda wa sherehe yenyewe tu ufike.

Kwakweli ilikua ni sherehe kubwa sana, naweza sema ilikua ni mojawapo ya sherehe kubwa kuwahi kutokea katika maisha yangu yote, chakula kwanza kilichopikwa kilikua ni chakula chenye tbs zote za ubora, vinywaji ndo siongei, watu wote tulikula tukanywa na kusaza. Baada ya chakula wote tukapumnzika kwaajili ya pini hapo baadaye, muda huu ukawapa wakuu wetu kutoa ya moyoni kwa vijana wao ambao ndo sisi

"Jonathan, kazi nzuri nimefurahishwa na utendaji wako wa kazi na wengine kwa ujumla ila nimemtaja Jonathan kwakua ndiye ambaye ameonyesha mwanga kwa vijana wetu tuliokua nao kwa muda mrefu mahali hapa" aliongea Mr Cheyo, ambaye yeye ni mwalimu wa vijana wapya wanaojiunga na kikundi chetu, nakutufanya wote tuitikie kwa pamoja
"Tunashukuru mkuu" baada ya hapo alipokea kijiti bwana James
"Kwakweli Jonathan umetupa mwanga sana yaani sana kwasababu hapo awali hatukuwahi kufikilia swala kama hili katika biashara zetu, swala la kwenda kuvamia benki tena benki kuu. Jonathan bigaapu sana yaani naamini tutafika mbali sana kwasababu yako" aliongea bwana James mtu wa karibu sana na bosi ambaye ikitokea bosi hayupo baasi yeye ndiye hukaimu nafasi yake, maneno yake yalinifanya nitingishe kichwa tu kama ishara ya kushukuru

"Mimi nitakuwa mbali kidogo na wenzangu, kwakua mimi nilikua nyuma ya vijana hawa muda wote walipokua wakitekeleza maswala haya benki, kiukweli kazi walioifanya inafurahisha sana lakini jinsi walivyoifanya pale mwishoni sikupendwezwa nao, Jonathan mmefanikiwa kutoka vizuri ndani ya benki badala ya kutimua mbio nyie ndo kwanza mnaanza kupongezana kwenye eneo la hatari hebu fikilieni maswala yetu ya mawasiliano yengebuma muda ule wakati mpo kupongezana mngefanyaje, kwakua ni mwanzo sio mbaya ila muda mwingine kumbukeni kazi kwanza maswala ya pongezi nyumbani" aliongea bwana Charls mkuu wa mawasilano ndani ya Ikulu hii ya bwana Claud, maneno yaliyowafanya watu wote waniangalie mimi kama ni mtu mwenye makosa yasiyosameheka pia kwa upande mwingine nami ilinijenga kwakua nikweli tulitumia makosa katika jambo hilo

Mkuu Wetu bwana Claud hakuongezea chochote zaidi alitusihi tukaze kamba zaidi katika dili zetu za usoni, muda wa pini ulipofika kila mmoja ili bidi aingie kati kuonyesha maujuzi yake, kwa upande wangu sherehe yangu ilikua imeishia katika upande wa kula na kunywa basi hivyo wakati bosi na wenzangu wanaendelea kucheza mimi nilikua nawaangalia tu, kila mmoja wao alikua akijitahidi kucheza vizuri kadri awezavyo ili awapate mabinti warembo, waliokua ndio wafanyakazi ndani ya jumba hili la bwana Claud

"Jonathan twende tukacheze mwaya" sauti ya msichana mrembo ndiyo iliyonishtua kwenye dimbwi la mawazo, naye hakuwa mwingine bali alikua Jane
"ata sijui kucheza Jane, ndio maana nimewaachia watu wenye vipaji vyao wavionyesheshe mbele" niliongea huku nikiwa na aibu ya kufwatwa na msichana mrembo kama Jane

"Wewe usijali twende tu nitakufundisha mimi mwenyewe" aliongea Jane wakati huo amenishaka mkono na ananivutia sehemu ya kuchezea nami sikutaka hilo, hali iliyowaacha midomo wazi wakuu wangu pamoja na wenzangu ambao wote walikua wakimmezea mate mrembo huyo, nami sikupanga kumwangusha mrembo huyu bali nilijipanga kumupagawisha vilivyo.

Wakati tunaingia sehemu ya kuchezea wimbo uliokua ukisikika ulikua ni Alingo wa P square, wimbo ambao nilikua nauelewa na naupenda vilivyo, nilianza kucheza taratibu huku Jane akinisindikiza kwa macho kabla hajaungana nami kucheza. Tulicheza vizuri mno jambo lililopelekea watu wote waliokuwepo mahala hapo waanze kutushangilia kwa makofi na nderemo, nami nikazidisha mikogo zaidi mara baada ya kuanza kucheza staili za mfalme wa pop hapa ulimwenguni (Michael Jackson) za kusheki huku bibiye Jane naye akizidi kunizungushia kiuno kama RayC.
ITAENDELEA

BIASHARA CHAFU

Sehemu ya 04

Na Mulabha Ntandala :

Tulicheza vizuri mno, jambo lililopelekea watu wote waliokuwepo mahala hapa waanze kutushangilia kwa makofi na nderemo, nami nikazidisha mikogo zaidi mara baada ya kuanza kucheza staili za mfalme wa pop hapa ulimwenguni (Michael Jackson) za kusheki huku bibiye Jane naye akizidi kunizungushia kiuno kama rayc.

Hali iliyomburudisha kila mtu aliyekuwepo eneo hili, nakupelekea watushangilie sana, mara baada ya wimbo huu wa Alingo kuisha nikatoka sehemu ya kuchezea nakuelekea sehemu iliyokua na viti, nikaa kwenye kiti kimojawapo mara baada ya kulifikia eneo hili huku kijasho chembemba kikinitiririka mara baada ya shughuli nzito niliyotoka kuifanya muda mfupi uliopita. Muda wa saa tano usiku tulihitimisha sherehe yetu iliyofaana sana, habari mpya ndani ya ikulu hii ya bwana Claud ikawa ni uwezo wangu wa kucheza muziki, huku kila mmoja akiongelea lake juu yangu mimi na mtoto mrembo Jane, nikajifanya kama nimeziba masikio ili kuondoa maneno maneno.

Zilipita siku mbili tukiwa ndani ya Jumba hili la namna yake tukiwa hatujafanya dili lolote la maana, jambo hili likapelekea muda mwingi mimi na wenzangu tutumie kuongea na mabinti warembo ambao walikua ndio wafanyakazi ndani ya mjengo huu. Sikutaka kufanya mazoea sana na binti hata mmoja ndani ya jumba hili kwani nilijua madhara ya kufanya hivyo, hivyo hata Jane niliacha kumwongelesha makusudi ilimradi tu nisiwe karibu nayeye japo Jane alitumia njia kadhaa za ushawishi ili niongee nae njia hizo zote zikagonga mwamba.

Hali hii ilimfanya Jane aanze kunichukia kwa kasi sana, yaani ndani ya siku hizo mbili tukawa kama Paka na panya yaani hatuwezi kuiva ndani ya chungu kimoja wakati juzi yake tumeonyesha maaajabu ya kucheza muziki mimi nayeye, ila sikupata shida kwa sababu nilikua najua nini nafanya kwa muda huu, nilisonga mbele na mambo yangu japo Jane alizidi kuonyesha chuki za waziwazi juu yangu nami hata sikulijali hilo nikazidi kupiga story na mabinti wengine ndani ya mjengo wa bwana Claud, jambo lililopelekea kila binti ndani ya mjengo huu atamani kuongea nami ijapo kwa sekunde tu yote ikiwa ni kwasababu ya ucheshi wangu na mvuto niliojaliwa na mwenyezi mungu ndio ukazidi kuwapagawisha mabinti wote.

"Vijana nadhani mmepunzika vya kutosha, sasa kesho jiandaeni kuna sehemu tunaelekea" alitamka maneno haya bwana Claud jioni ya siku ya pili, nakutufanya wote tufurahi kwakuwa tulikuwa tumezikumbuka sana dili hizi
"Sawa mkuu, hatujajua tunaenda vipi? Sehemu hiyo" tulizungumza tukiwa na shauku na hamasa ya kuelekea eneo hilo
"kesho tuneelekea wote huko na upande wa mawasiliano tutamwachia bwana mdogo Job ambaye ameanza kujifunza maswala ya mawasiliano kwa muda mrefu sasa" alijibu Bwana Claud nakufanya wote tutaharuki hali hii, kwasababu hali kama hii haijawawi kutokea.

Wote ikabidi tukubaliene na matokeo haya, kesho yake asubuhi Bosi, James, Cheyo na Charls wakuu wetu wote tukaongozana nakufanya tuwe na watu kumi na moja wote pamoja na wakuu wetu nakuanza kuelekea sehemu ambayo hadi muda huu bosi peke yake ndiye aliyekua akijua ni wapi? Tunaelekea, Gari yetu ikaja kutia nanga pembozoni kidogo mwa jiji la dar es salaam, tukashuka ndani ya gari na kuanza kusubiri amri kutoka kwa mkuu

"Mnaliona jengo lile pale?" aliuzaa bwana Claud, wakati huo amenyoosha kidole chake cha shahada upande wa kulia
"yaaah! Unamaanisha jengo la Matiku Supermarket" alijibu bwana Charls, nakufanya wote tuangalie mahali ilipo supermarket hio
"haswa vijana wangu inatakiwa tuenda mule ndani, tukishaingia ndani tunaelekea moja kwa moja sehemu ya kukusanyia mapato yao, hapo hamna kuremba tunachukua kila kitu, ila hakikisheni kila mmoja wenu ameweka siraha yake mahali salama" aliongea bwana Claud kwa sauti iliyoshiba kiasi kuonyesha ni jinsi gani Yupo siriazi katika hili

Bila kupepesa macho wote tukaelekea kwa kasi ya umeme mahali ilipo Matiku Supermarket, tulivyoifikia tukaingia ndani kwa kasi ya hajabu jambo lililowashtua wateja waliokua ndani ya Supermarket hii, sisi hatukulijali hilo tukasonga moja kwa moja mpaka sehemu ya kukusanyia mapato katika supermarket hii, tulivyolifikia eneo hili wote tukachomoa siraha zetu kwenye suluali zetu na kuwaamuru wahadumu wa mahala hapa watoe hela zote.

Woga na hofu ukawagubika wahudumu tuliowakuta eneo hili, jambo lililopelekea waanze kutoa pesa nyingi katika sehemu walipokua wanazihifadhi, baada ya kututolea pesa za kutosha, tukazikusanya pesa hizo na kuziweka katika mifuko maalumu tuliyokuja nayo eneo hili kisha tukaanza kutoka eneo hili la Matiku Supermarket kwa tahadhali kubwa.

Tukiwa ndio tumefanikiwa kutoka ndani ya Supermarket hii, mara tukasikia
"hivyo hivyo mlivyo simameni na mjisalimishe wenyewe, kabla hatujachukua hatua zaidi juu yenu" ilikua ni sauti ya askari polisi aliyekua akiongea kwa kutumia kipaza sauti, nilivyojaribu kuangaza macho yangu sikuamini nilichokua nakiona eneo hili, yaani eneo lote lilikua limetapakaa Polisi na nilivyojaribu kuwaangalia wenzangu wote walikua wakitetemeka sana huku kijasho chembemba kikiwatiririka.

ITAENDELEA..
 

Attachments

  • 1466262118433.jpg
    1466262118433.jpg
    23.5 KB · Views: 56
Back
Top Bottom