Farao asiyemjua Yusufu kaja

VIVIANET

JF-Expert Member
Aug 30, 2015
2,129
2,918
Kwenye Biblia kuna simulizi moja nzuri sana ya maisha ya Yusufu katika nchi ya Misri. Baada ya Yusufu kuuzwa katika nchi ya Misri kama mtumwa Mungu alimtendea muujiza wa kutafsiri ndoto iliyowashinda wanajim na wenye maarifa wote wa Misri, wakati huo Yusufu akiwa mfungwa kwa kosa la kusingiziwa kutaka kubaka mke wa bwana wake. Ililazimu Yusufu kuitwa ikulu kuja kusaidia ktafsiri ndoto iliyomkosesha mfalme Farao amani. Mungu alimsaidia kutafsiri ndoto hiyo na mfalme kuridhia Yusufu kuwa waziri mkuu.

Ila baada ya Farao aliyemjua Yusufu na kuthamini mchango wake mkubwa na hekima aliyoitoa iliyosababisha nchi yote ya Misri kupona katika maangamivu ya njaa kuli iliyoikumba nchi, Farao aliyefuata hakumjali Yusufu na matokeo yake alimtesa, pia aliwatesa watu wake.

Nimefananisha kwa karibu sana na tukio kubwa lililompata kaka yangu Nape Nnauye, kwa hatua ccm ilipokuwa imefikia hakuna hata mwanachama na mtanzania mwenye hekimana busara anaweza kubeza juhudi za Nape, alifanya juhudi kubwa sana kuiokoa ccm kukubalika tena. Mzee Kikwete alikuwa kama Farao aliyemjua Yususfu na kujali juhudi na jitihada zake alizoonyesha, ila huyu Farao asiyemjua Yusufu anaona wanaccm wa zamani kama takataka na ameamua kwa dhati kuanza kuwatesa wale wote ambao Farao alimaliza muda wake aliwajali na kuwaheshimu.

Nahisi muda simrefu wapo wengi ambao hawateendelea kukubaliana na hili linalofanywa na Farao asiyemjua Yusufu. Naamini muda simrefu watu watashangaa kuona watu walioipenda ccm na wapigania ccm wakizodolewa waziwazi

Tutabisha ila tutayaona muda simrefu
 
Huyu bwana ana madharau ni balaa. Duniani kote watu huthamini mchango wa mtu ktk ujenzi /ukuzaji wa taasisi kama chama cha siasa. Huyu jamaaa ana wanyanyasa key players wa ccm akiamini walikuwa nje ya kambi yake.
 
Siku moja atawakumbuka tu
 
Kwenye Biblia kuna simulizi moja nzuri sana ya maisha ya Yusufu katika nchi ya Misri. Baada ya Yusufu kuuzwa katika nchi ya Misri kama mtumwa Mungu alimtendea muujiza wa kutafsiri ndoto iliyowashinda wanajim na wenye maarifa wote wa Misri, wakati huo Yusufu akiwa mfungwa kwa kosa la kusingiziwa kutaka kubaka mke wa bwana wake. Ililazimu Yusufu kuitwa ikulu kuja kusaidia ktafsiri ndoto iliyomkosesha mfalme Farao amani. Mungu alimsaidia kutafsiri ndoto hiyo na mfalme kuridhia Yusufu kuwa waziri mkuu.

Ila baada ya Farao aliyemjua Yusufu na kuthamini mchango wake mkubwa na hekima aliyoitoa iliyosababisha nchi yote ya Misri kupona katika maangamivu ya njaa kuli iliyoikumba nchi, Farao aliyefuata hakumjali Yusufu na matokeo yake alimtesa, pia aliwatesa watu wake.

Nimefananisha kwa karibu sana na tukio kubwa lililompata kaka yangu Nape Nnauye, kwa hatua ccm ilipokuwa imefikia hakuna hata mwanachama na mtanzania mwenye hekimana busara anaweza kubeza juhudi za Nape, alifanya juhudi kubwa sana kuiokoa ccm kurudi madarakani. Mzee Kikwete alikuwa kama Farao aliyemjua Yususfu na kujali juhudi na jitihada zake alizoonyesha, ila huyu Farao asiyemjua Yusufu anaona wanaccm wa zamani kama takataka na ameamua kwa dhati kuanza kuwatesa wale wote ambao Farao alimaliza muda wake aliwajali na kuwaheshimu.

Nahisi muda simrefu wapo wengi ambao hawateendelea kukubaliana na hili linalofanywa na Farao asiyemjua Yusufu. Naamini muda simrefu watu watashangaa kuona watu walioipenda ccm na wapigania ccm wakizodolewa waziwazi

Tutabisha ila tutayaona muda simrefu
Usifananishe maandiko matakatifu na matukio ya ujinga wa mtu kujitakia mwenyewe, mchango mchango...huwezi kuwa mtumwa wa michango ya watu in your life if you need to move forward..Nape ilikw ni wajibu wake kufanya hivyo n he was paid..nadharia za ujinga kufikiria km unavyodhani.
 
Basi furahi kwakuwa utawala wa farao umefika mwisho!

Si ndiyo maana yake?
 
Usifananishe maandiko matakatifu na matukio ya ujinga wa mtu kujitakia mwenyewe, mchango mchango...huwezi kuwa mtumwa wa michango ya watu in your life if you need to move forward..Nape ilikw ni wajibu wake kufanya hivyo n he was paid..nadharia za ujinga kufikiria km unavyodhani.

Ebu nionyeshe ujinga wangu katika andiko langu.. Pia nionyeshe kosa la Nape liko wapi? na mwisho nisaidie ni wapi ambapo imekatazwa tusitumie maadniko katika kuelezea yale yanayotusibu, la sivyo utakuwa mjinga mara mbili maana utachanganya huo ujinga uliouona kwangu plus wa kwako
 
Yusufu alitakiwa anyamaze asiongee popote baada ya nafasi yake kupewa MTU. Farao ana nafasi tele kama alivyompa mama take LeKubwas baada ya kuufyata.
 
Ujinga wako ni kueleza hbr za mchango wa mtu kwny jambo fulani km kinga ya kutochukuliwa hatua hata km amekosea, pili Nape si lazima awe waziri kwa vile tu ana mchango fulani, tatu Biblia ni neno la Mungu hutafsir Biblia km unavyotafsiri gazeti la udaku, nne Nape km waziri anapaswa kuheshimu nafasi hiyo huwezi kuwa unaitwa itwa kwny matukio mnajadiliana kwny tukio halaf unatoa uamuzi bila hata kujipa muda wa kupima kwa undani uliyoelezwa na mahusiano na kazi yako, Nape alikosa hata kuheshimiwa mara cjui steve nyerere kamtaja kwny mambo gani..wanauona km mwenzao tu wakati yeye ana dhamana kubwa na anastahili kuheshimiwa, angalia tofauti sasa km huyu aliyechaguliwa hao wasanii watampanda kichwani..
 
Labda umesahau kama Yusufu ndiye alikuwa mpanga mipango na msimamizi wa kila kitu pale Misri kwahiyo alikuwa anaongea sana
 
"Nimeitoa ccm shimoni" kwa nini usitumie tumeitoa? Huyu kawa na nguvu kiasi gani mpaka yeye aitoe ccm shimoni? Hakumuona Kinana wala Mangula. Anataka tuamini angefanya nini kumkata mamvi kama Kikwete asingetoa kibali?

Na mfananisha na yule tajiri wa Kwenye Biblia aliye tengeneza ghala kubwa akajaza mazao akaishia kuambiwa mpumbavu wewe.

Kwa vile kwa mtazamo wake aliitoa ccm shimoni alifikiri ataachwa baada ya kutofautiana na Rais.

Na washawasha!
 
Kwani anayesema anainyoosha Tanzania ana nguvu gani? anaposema sikuambiwa na mtu kuchukuwa fomu nilienda mwenyewe na siwezi kuambiwa na mtu huyu ni mpangie wapi je ana nguvu gani? hivi huyu anayesema Dar ya Makonda amewaumba wana Dar?
 
Bwana huyu ananikumbusha mfalme herode na binti aka. Binti alipocheza vizuri mbele he baba mfalme akafurahi mbaya akamwambia achague zawadi ......bashitiiii akaomba kichwa cha napiiiii movi ikaisha
 
Ujinga wako ni kueleza hbr za mchango wa mtu kwny jambo fulani km kinga ya kutochukuliwa hatua hata km amekosea, pili Nape si lazima awe waziri kwa vile tu ana mchango fulani, tatu Biblia ni neno la Mungu hutafsir Biblia km unavyotafsiri gazeti la udaku, nne Nape km waziri anapaswa kuheshimu nafasi hiyo huwezi kuwa unaitwa itwa kwny matukio mnajadiliana kwny tukio halaf unatoa uamuzi bila hata kujipa muda wa kupima kwa undani uliyoelezwa na mahusiano na kazi yako, Nape alikosa hata kuheshimiwa mara cjui steve nyerere kamtaja kwny mambo gani..wanauona km mwenzao tu wakati yeye ana dhamana kubwa na anastahili kuheshimiwa, angalia tofauti sasa km huyu aliyechaguliwa hao wasanii watampanda kichwani..
Aisee sikutegemea kuwa we ni mjinga kiasi hicho.
Kila andiko kwenye biblia Lina pumzi ya Mungu na linafaa kwa mafundisho
Hivyo maneno yote ktk biblia yanafaa kutufunza na kujua nini kinachoendelea ktk ulimwengu huu
 
Huyu bwana ana madharau ni balaa. Duniani kote watu huthamini mchango wa mtu ktk ujenzi /ukuzaji wa taasisi kama chama cha siasa. Huyu jamaaa ana wanyanyasa key players wa ccm akiamini walikuwa nje ya kambi yake.
sasa aliwataka wa nini kama fomu alichukua mwenyewe kila kitu mwenyewe
 
"Nimeitoa ccm shimoni" kwa nini usitumie tumeitoa? Huyu kawa na nguvu kiasi gani mpaka yeye aitoe ccm shimoni? Hakumuona Kinana wala Mangula. Anataka tuamini angefanya nini kumkata mamvi kama Kikwete asingetoa kibali?

Na mfananisha na yule tajiri wa Kwenye Biblia aliye tengeneza ghala kubwa akajaza mazao akaishia kuambiwa mpumbavu wewe.

Kwa vile kwa mtazamo wake aliitoa ccm shimoni alifikiri ataachwa baada ya kutofautiana na Rais.

Na washawasha!
Alikua na haki kusema hivyo na ni kweli.
Kwani hujui walichofanya nape na makamba wakati wa kuhesabu kura.
Ulisahau kauri ya nape kuwa kuwa hata iweje tutashinda hata kwa bao la mkono.
We unajua maana ya kauri hiyo?
 
Back
Top Bottom