UWATA (Uamsho wa Wakristo Tanzania) ni dhehebu la dini ya kikristo kama yalivyo madhehebu mengine. Dini na dhehebu lolote anakaribishwa kujiunga dhehebu hili.
Kujiunga nao, unatakiwa kutubu dhambi na kuziacha kabisa.
Utambulisho wao wa mavazi kwa wanawake ni sketi ndefu ya marinda na blauzi au gauni ndefu yenye marinda, kukata nywele, kutovaa heleni, bangili, cheni, rozari wala mapambo aina yoyote. Kwa wanaume, suruali ya kitambaa na shati au tisheti, suruali za jeans haziruhusiwi.
Nyumba yao ya ibada wanaiita "faragha", yaani wanakutana na kusali pasipo kujionyesha machoni pa watu. Faraghani huwa hakuna mabenchi wala viti, bali kuna mikeka tu, hii wanaenzi agano la kale la mitume na kinabii.
Mwanzilishi wa imani hii anaitwa Harrison Mwakiswalele.