Fao la kujitoa nssf, wafanyakazi tuna msimamo gani! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fao la kujitoa nssf, wafanyakazi tuna msimamo gani!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by chachu, Oct 26, 2012.

 1. c

  chachu Senior Member

  #1
  Oct 26, 2012
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ni siku chache zimepita tumemsikia mkurugenzi wa NSSF Dk akieleza kamati ya mashirika ya umma fao la kujitoa kamwe halitawezekana kwa mfanyakazi atakayejitoa hadi miaka 55 au 60. Wakati tunajiunga na mfuko huu hawakutueleza hayo ila kwa sasa kwa sababu wanazifanyia biashara na zimewanogea kwa sababu wanazifanyia biashara bila riba wameamua kuziwekia sheria kandamizi ile waendelee kunufaika nazo. Ni aibu kufananisha nchi yetu na nchi za ulaya ambazo hata kodi wanazolipa zinakidhi yale mahitaji ya jamii na dhamani ya hela yao ikiendelea kupanda wakati shilingi yetu ikishuka. Je thamani ya fao langu la mwaka huu litakuwa na dhamani sawa na kusubiria miaka 20..!? Tumekuwa watu wa kuiga kila kitu hatuwezi kuwa na mfumo wa kwetu unaoendana na maisha yetu? au ni uvivu wa kufikiri ndio maana tunaiga kila kitu kwa wenzetu! wafanyakazi tumekuwa janga, kodi kubwa sisi, mshahara hautoshelezi watu wengi wameweza kufungua au kuanzisha vipato vya ziada kwa kutumia mafao ya kujitoa.
  Wafanyakazi tuungane kwa pamoja kupinga na kusema hapana kwa hii sheria kandamizi. Kukaa kimya ndio mwanzo wa kuwapa nguvu akina Dk D kujiona wao wanaweza kusema wanavyojisikia.

  Nawakilisha wana GT tuchangie ktk hili tuone limekaaje.
   
 2. j

  jail JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 421
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  ni kiburi hiki hela wameweka kwenye miradi ya kisiasa na hawana uhakika kama zitarudi nahisi hawana pesa ndo maana wana hofu ya kushindwa kulipa endapo watu watajitoa wamewe keza kwenya miradi tata hairudishi hela mapema.sio mfuko wa kujiunga kwa sasa
   
 3. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  nimejianda kuishinikiza serikali ya vibaka kufuta sheria hiyo ya kihuni..niko tayari kuandamana
   
 4. a

  adolay JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 7,567
  Likes Received: 3,026
  Trophy Points: 280
  Kinachoendelea NSSF na kwingineko, ni UFISADI uliokomaa ukapevuka na kupevuka kisha kuvuka hata mipaka ya kuudhibiti uchu na urafi wa fedha za maskini wachache watanzania kwa visingizo visivoingia akilini, wakiwaacha watanzania sehemu kubwa bila msaada wowote kwenye umri huo nazaidi wakifa kwa njaa, kukosa matibabu na malazi hafifu. Hii sio huruma ila ni ujambazi wa mchana kweupe.

  inawezekana huko kwa wenzetu kwasababu wametengeneza mazingira mazuri inapotokea mwanachama kakosa ajira, hapa kwetu haiwezekani kabisa.Hakuna mazingira yaliyoandaliwa kumfanya mwanachama aishi kwa amani/matumaini akipata huduma za lazima hasa baada ya kuacha au kuachishwa kazi akiwa na umri chini ya miaka 55.

  Huyu Dau nilimtazama mara mbilimbili wakati akisema anasimamia sheria uso wake ulionesha dharau, kejeri na kiburi ndani yak. Hana aibu hata huruma ni fisadi fulani vile.

  1. Sina kazi, watoto wangu wamerudishwa nyumbani kutoka shule hawajalipa ada, Dau na serikali yake wanasimamia sheria ipi? sheria! watoto wao wanasoma, wangu wanasubili kuwa vibaka nyumbani? je hayo mafao yanafaidagani basi kwangu nafamilia yangu?


  2. Ni vipi nitaendelea kusubili hiyo miaaka 55 itimie sina mtaji, wala mradi wowote kuniwezesha kuishi kwa matumaini kufika huko? watalipa kwa kaburi langu, maana kufa ni lazima sina cha kunifanya niendelee kuishi bila kula wala afya bora . hapa kwetu siku hizi afya bora inapaikana nje ya inchi hususani India.


  3. Tuna wakulima na wasio nakazi zaidi ya 70%, hawa tunawaona kila siku wakizeeka wakiuguwa na kufa. serikali inatoa mafao gani kwa vikongwe endapo msingi ni kuwafanya waishi bila kutaabika? Je sera hapa ni kuhami matatizo ya uzeeni au kutuibia mafao yetu. (Ningekubaliana na sheria hiyo endapo kundi hilo la wakulima wangekuwa wanapewa chochote)

  4. Dau kama yeye ameshiba na anaakiba yakutosha, asitupangie lini tuchukuwe mafao yetu sisi wenye njaa na ambao kila siku inapokucha ni afadhari ya jana, Dau ni mnafiki maana anajuwafika serikali imeufilisi mfuko wake! alikuwa wapi kutueleza haya hapo kabla? na ilikuwaje walilipa hapo kabla hii sheria waliweka pembeni kwa misingi gani kama sio mazingira yetu kiuwezo shirika kushindwa kukidhi baadhi ya mahitaji ya msingi kwa wanachama wake?


  Tuwasubuiri wabunge waingie mkenge wa huyu pumbavuu Dau, tutaonana huku mitaani, adhabu ya kubaka na kuiba akiba zetu sio tu zitawatowa katika viti vyao vya ubunge, lakini kila mwanachama mpenda haki wa hii mifuko lazima tulipize visasi kwa wabunge vya aina yoyote ile, iwe ni kwa kutumia silaha au sumu vyovyote vile watakuja kuomba kura 2015. haiwezekani wao (wabunge) baada ya miaka yao mitano pale bungeni wanachukuwa mafao yao kwanini nawao wasisubili at 55 au zaidi???
   
 5. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  wenzetu wana un-employment benefit ndio maana hawana withdraw benefit! Dr.Dau ni swahiba mkubwa wa dhaifu ndio maana ana jeuri sana!
   
 6. M

  Mpekuzi Makini Member

  #6
  Oct 26, 2012
  Joined: Sep 5, 2012
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  life expectancy ya mtanzania ni miaka mingapi? ni sawa na ya Norway, UK, German, USA nk? wanataka kutoa mafao wakati mtu amekufa? mbona hawaziwekei vikwazo hivyo wanapotoa kwa miradi ya kisiasa na kukopesha wanasiasa? mnakumbuka milioni 50 alizokopeshwa mheshimiwa .....?
   
 7. M

  Mpekuzi Makini Member

  #7
  Oct 26, 2012
  Joined: Sep 5, 2012
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  muyaonapo haya kumbukeni wazalendo walioandika kijitabu na kuchambua historia ya nchi hii na tuendako (Je, tutafika?) ninaporejea kijitabu hicho nagundua na tunaona kwa wazi tuko kipindi cha "Mibaka Uchumi" na tunaona mibaka uchumi inavyojitajirisha bila kudai hali duni za wananchi walio wengi. Hata kidogo kilichopo wanataka wachukue - Je, tutafika?
   
Loading...