hii inanihusu sana, nafanya kazi si kwa kupenda kabisa, nimekuwa mtumwa, kazi ni utumwa hata kama unalipwa, naamka asubuhi na mapema si kwa kupenda, narudi nyumbani usiku si kwa kupenda, Maisha yangu yanamtegemea Mwajiri wangu, da inaniuma sana kwa kweli, kama wakina Thomas edson walifeli mara 10,000 na baadae akaja kufanikiwa vipi kuhusu mimi? nimefeli mara ngapi?
Mkuu naenda kuchukua maamuzi magumu kabisa katika historia ya maisha yangu, ni lazima niwe huru bila kujalisha huo uhuru utanilaza njaa, naenda kuchukua maamuzi bila kujali ndugu, jamaa na marafiki watanuonaje, najua hawatanielewa kwa sasa ila ipo siku watanielewa hata kama ni baada ya miaka 20