Familia zenye mduara wa talaka……………..!

Kuoa na kuacha au kuolewa na kuachwa ni mambo yasiyoweza kwenda kimya ndani ya nyumba. Mme anapoacha na kuoa tena, na mke anapoachwa au kuolewa tena, mara nyingi huwa na maneno au kauli wanazozitoa kuhusiana na matukio hayo. Ni bahati nzuri sana kama kauli hizo zinaonyesha kulaani kuacha au kuachwa kwa wahusika (wao wenyewe kujilaumu)na hazionyeshi kwamba kuacha au kuachwa huko ni suala la kufurahiwa. Bila shaka wazazi wengi wanapokuwa wanaacha au kuachwa kwa mara ya kwanza na zile zianazofuata, huwa tayari wana watoto. Watoto hawa husikiliza kile kinachosemwa na wazazi kufuatia kuachana huko na kuna wakati hufikia hata kuuliza kinachoendelea. Wazazi bila kujua hujikuta wakiropoka kwa watoto hao.

Kauli kama "wanaume wako wengi, tusitishane, ukiniacha nitaolewa hata kesho," ni kauli hatari sana kwa watoto wa kike kuisikia. Kauli hii inapofuatia kwa mama aliyeitoa kuachwa, mtoto wa kike anakuwa amejengewa dhana kwamba kwenye ndoa hakuna haja ya mtu kuvumilia kwani suluhu muafaka ni kuachana na mume msumbufu na kutafuta mwingine ambaye kwa kawaida hupatikana. Inapotokea mama kama huyu kuachwa na kuolewa tena somo kwa mtoto linakuwa limekamilika. Kuna uhakika wa tisa kwa kumi kwamba binti huyu hataweza kuja kuishi kwenye ndoa.

Kauli kama "hata siku moja mwanamke asikutishe, wako wengi na wazuri sana, akikuletea ujinga, unaacha tu." Inapofuatiwa na mwanaume huyo kuoa na kama imesikiwa na mtoto wa kiume kuna hatari kubwa. Mtoto huyo ataamini kwamba, ni kweli kunapozuka kutoelewana kwenye ndoa, dawa ni kumtimua mwanamke na kuoa mwingine. Kauli zenye kudhuru zenye kuwafanya watoto waamini kwamba, kuachana kwenye ndoa ndiyo suluhu muafaka ziko nyingi na zinatofautiana kwa uzito. Kila mmoja wetu anapoisikia au kutamka kauli yenye madhara kwa mtoto au watoto kuhusiana na kuachana katika ndoa anaweza akaitambua. Kuna wakati huwa tunashangaa kwamba watoto wa familia fulani huwa hawakai na mume au mke mmoja katika ndoa zao, bali kuoa au kuolewa na kuacha au kuachwa. Jibu mojawapo la kitendawili hiki ni hilo. Ni moja kati ya majibu kwa sababu inawezekana kukawa na sababu nyingine. Kwa mfano tabia ya wazazi ambao wenyewe hawajaachana kuwatolea watoto kauli zenye kuonyesha kwamba, mtu hana haja ya kusumbuliwa kwenye ndoa, kwani suluhisho la usumbufu ni kuondoka.

Wazazi wanapoachana badala ya kuwaonyesha watoto kwamba kuachana huko ni suluhisho tamu na zuri, inabidi wawasisitizie kwamba wasije wakakubali wakiwa wakubwa kuachana na waume zao au wake zao, labda pale tu kila njia ya kusuluhisha tofauti zao inaposhindikana. Hii inawafanya watoto kuelewa kwamba pamoja na wazazi wao kuachana, wao hawapaswi kufikia hapo.
well said mtambuzi! hapo red nadhan kutawaokoa haswaa! na siku izi talaka kama fashion yan mmh! huruma.
 
Back
Top Bottom