Familia zenye mduara wa talaka……………..! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Familia zenye mduara wa talaka……………..!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Feb 7, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Feb 7, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kuoa na kuacha au kuolewa na kuachwa ni mambo yasiyoweza kwenda kimya ndani ya nyumba. Mme anapoacha na kuoa tena, na mke anapoachwa au kuolewa tena, mara nyingi huwa na maneno au kauli wanazozitoa kuhusiana na matukio hayo. Ni bahati nzuri sana kama kauli hizo zinaonyesha kulaani kuacha au kuachwa kwa wahusika (wao wenyewe kujilaumu)na hazionyeshi kwamba kuacha au kuachwa huko ni suala la kufurahiwa. Bila shaka wazazi wengi wanapokuwa wanaacha au kuachwa kwa mara ya kwanza na zile zianazofuata, huwa tayari wana watoto. Watoto hawa husikiliza kile kinachosemwa na wazazi kufuatia kuachana huko na kuna wakati hufikia hata kuuliza kinachoendelea. Wazazi bila kujua hujikuta wakiropoka kwa watoto hao.

  Kauli kama "wanaume wako wengi, tusitishane, ukiniacha nitaolewa hata kesho," ni kauli hatari sana kwa watoto wa kike kuisikia. Kauli hii inapofuatia kwa mama aliyeitoa kuachwa, mtoto wa kike anakuwa amejengewa dhana kwamba kwenye ndoa hakuna haja ya mtu kuvumilia kwani suluhu muafaka ni kuachana na mume msumbufu na kutafuta mwingine ambaye kwa kawaida hupatikana. Inapotokea mama kama huyu kuachwa na kuolewa tena somo kwa mtoto linakuwa limekamilika. Kuna uhakika wa tisa kwa kumi kwamba binti huyu hataweza kuja kuishi kwenye ndoa.

  Kauli kama "hata siku moja mwanamke asikutishe, wako wengi na wazuri sana, akikuletea ujinga, unaacha tu." Inapofuatiwa na mwanaume huyo kuoa na kama imesikiwa na mtoto wa kiume kuna hatari kubwa. Mtoto huyo ataamini kwamba, ni kweli kunapozuka kutoelewana kwenye ndoa, dawa ni kumtimua mwanamke na kuoa mwingine. Kauli zenye kudhuru zenye kuwafanya watoto waamini kwamba, kuachana kwenye ndoa ndiyo suluhu muafaka ziko nyingi na zinatofautiana kwa uzito. Kila mmoja wetu anapoisikia au kutamka kauli yenye madhara kwa mtoto au watoto kuhusiana na kuachana katika ndoa anaweza akaitambua. Kuna wakati huwa tunashangaa kwamba watoto wa familia fulani huwa hawakai na mume au mke mmoja katika ndoa zao, bali kuoa au kuolewa na kuacha au kuachwa. Jibu mojawapo la kitendawili hiki ni hilo. Ni moja kati ya majibu kwa sababu inawezekana kukawa na sababu nyingine. Kwa mfano tabia ya wazazi ambao wenyewe hawajaachana kuwatolea watoto kauli zenye kuonyesha kwamba, mtu hana haja ya kusumbuliwa kwenye ndoa, kwani suluhisho la usumbufu ni kuondoka.

  Wazazi wanapoachana badala ya kuwaonyesha watoto kwamba kuachana huko ni suluhisho tamu na zuri, inabidi wawasisitizie kwamba wasije wakakubali wakiwa wakubwa kuachana na waume zao au wake zao, labda pale tu kila njia ya kusuluhisha tofauti zao inaposhindikana. Hii inawafanya watoto kuelewa kwamba pamoja na wazazi wao kuachana, wao hawapaswi kufikia hapo.
   
 2. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #2
  Feb 7, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  too long, nitazeeka nikiwa nasoma hii kitu
   
 3. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #3
  Feb 7, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,237
  Likes Received: 3,654
  Trophy Points: 280
  Napenda kusahihisha,sio mwanaume pekeyake huacha,na sio mwanamke pekeyake huachwa hayo hutokea pande zote mbili,other parts of the mada are gud,i like this!
   
 4. c

  christer Senior Member

  #4
  Feb 7, 2012
  Joined: Feb 12, 2010
  Messages: 131
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  nice thread maana mdomo ulikponza kichwa
   
 5. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #5
  Feb 7, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,237
  Likes Received: 3,654
  Trophy Points: 280
  It seems your someone's x!Dont wory,maisha ni matam hata kama uko pekeyako!
   
 6. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #6
  Feb 7, 2012
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hii ni jeuri isiyo na maana.
  Hayo huwa ni maneno ya hasira na hayatolewi wakati wa amani hata siku moja.
  Mpaka ifikie mnagombana mbele ya watoto na kutoleana kashafa hivi, basi hamfai kuitwa "baba" au "mama".

  Ukiweza kutamka maneno kama hayo mbele ya wanao basi ujijue una mdudu kichwani.
   
 7. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #7
  Feb 7, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,867
  Likes Received: 6,219
  Trophy Points: 280
  ...........oraiti
   
 8. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #8
  Feb 7, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Thanks Mtambuzi
   
 9. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #9
  Feb 7, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Thread nzuri sana hasa ukizingatia hizi point weldone mchapa magazeti leo gazeti lako limekuja na point nzito sana.

  Nimependa hizi point na ndo zinazo sababisha talaka mara nyingi sana hasa kama mwanaume hajui kujicontrol wakati huo...na anafikiria talaka ni lele mama.

   
 10. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #10
  Feb 7, 2012
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Baba yangu aksante sana kwa hili somo.
   
 11. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #11
  Feb 7, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Unkoo! maneno yako ya leo yameniingia haswaaaaa! mana kule wale wanao achana ukasikia" Nilikua nakusubiri unipe hiyo talaka kwa hamu kwanzanilishakuchoka mkwa mume gani ,kwa lipi?
   
 12. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #12
  Feb 7, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Mwanangu kumbe upo!
  nakusalimu huko ulipo......................
   
 13. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #13
  Feb 7, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Na mwanaume kila akioa anaachwa na wanawake huyu tutamzungumziaje?
   
 14. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #14
  Feb 7, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Huyo mwanaume bila shaka atakuwa ana GUBU..............................
  Ni wanawake wachache sana wanaomudu kuwavumilia wanaume wenye GUBU.
   
 15. Black Rose

  Black Rose JF-Expert Member

  #15
  Feb 7, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 243
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  atakua ana GUNDU huyo
   
 16. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #16
  Feb 7, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  kuna mduara wa talaka

  na kuna mduara wa kuzaa bila kuolewa
  nimeona familia nyingi saana

  kuna imani dada wa kwanza akizaa kabla ya kuolewa wengine hufuata

  na kuna imani kuwa dada wa kwanza akichelewa kuolewa basi anawacheleweshea wengine kuolewa

  na kuna mduara unaonzishwa na mama pia.....

  tuliwahi kuzungumza kuhusu 'mzaliwa wa kwanza humu kwa mujibu wa mchungaji mwakasege....
   
 17. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #17
  Feb 7, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Vipi kuhusu mduara wa wanaume katika familia moja kuzaa zaa hovyo na wanawake kila kona................
   
 18. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #18
  Feb 7, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Hivi ni Gubu au Gundu?
   
 19. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #19
  Feb 7, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Huo ndo uanaume bana unaeneza ukoo wenu kila kona
   
 20. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #20
  Feb 8, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Nice guess but not really
   
Loading...