Familia za Madagascar 'zinakula matope' kutokana na ukame mbaya

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Ukame unaolikumba eneo la Kusini mwa Madagascar ni mbaya kuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha miaka 40

Shirika la mpango wa chakula duniani linaonya kuwa unaolikumba eneo la kusini mwa Madagascar kwa miongo minne unasababisha njaa na ukame mkubwa

Mkurugenzi wake, David Beasley, ambaye ndio ametembelea kanda hiyo, amesema bila msaada wa haraka kwa watu zaidi ya nusu milioni itakuwa ni "kubisha mlango kwa familia zinazokabiliwa na ukame ", huku watu wengine 800,000 wakielekea kupatwa natatizo hilo.

Amesema kuwa alishitushwa na kile alichokiona Kusini mwa Madagascar – ambako watoto walikuwa wamebakia tu na mifupa yenye ngozi, na familia zilikuwa zikila matope na matunda pori kwasababu hapakuwa na kitu kingine.

Beasley ameiita hali inayoendelea katika kusini mwa Madagascar ‘’janga la kimya lililo katika eneo lilililosahahulika.

Mzozo huo unasababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa, ambapo ukame umeendelea kuwepo na kuzilazimisha familia kuzihama nyumba zao, amesema Bw Beasley.

Amesema kuwa mataifa tajiri hayana maadili ya uwajibikaji ya kusaidia.

Hali hiyo imesababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa, ambapo ukame umeendelea kuwepo na kuzilazimisha familia kuzihama nyumba zao
 
Hivi kwanini majanga yanapotokea inachukua sana muda kuweza kutatua,Mpaka watu wafe hasa watoto,kuna nchi jirani kuna taasisi nk.zinasubiri shirika la chakula duniani, mpaka likae lijadiri huku watu wanaendeleaje kula matope,ndio ya Rwanda na Burundi kushindwa kuchukua hatua haraka mpaka muone watu wamedondoka
 
AU ipo km picha tu!! Majinhga yale!!! walicho jua ni kumpiga Mkoloni aondoke ili wapate Masifa ya kuwa viongozi wa Africa na wajinufaishe wao na familia zao tu baasi!! leo hawajali maafa km haya!!!

Hata tulio tayari kwenda kusaidia tutapigwa majungu!! Miafrica mlimfanyia Mungu dhambi kubwa sana, Rutuba yooote hiii!! tubuni hamtaki, badala yake mnatubu kwa Papa!! mwenye mavi tumboni km wewe!!
 
Back
Top Bottom