Amnesty yaitaka Madagascar kuachana na adhabu ya kuwahasi wanaobaka Watoto

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,617
Shirika la Haki Za Binadamu la Amnesty limesema Madagascar inafaa kuachana na Sheria mpya inayoruhusu kuhasiwa kwa kuchomwa sindano au kufanyiwa upasuaji kwa watu waliopatikana na hatia ya ubakaji wa watu wenye Umri wa chini ya Miaka 18 kwani ni "ya kikatili, ya kinyama na inayopunguza hadhi,"

Januari 2024, Rais Andry Rajoelina alipendekeza marekebisho katika kanuni ya jinai, ambayo inajumuisha kuhasiwa kwa kuchomwa sindano au kufanyiwa upasuaji kama adhabu kwa watu waliopatikana na hatia ya ubakaji dhidi ya watoto, mabadiliko ambayo yaliungwa mkono na Bunge

Taarifa ya Tigere Chagutah, Mkurugenzi wa Amnesty Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini imesema "Adhabu ya Kuhasiwa ambayo inachukuliwa kama ya kikatili, ya kinyama na inayopunguza hadhi, kwa wale waliopatikana na hatia ya ubakaji wa watoto haitatatua hali ya kutoripotiwa kwa Vitendo hivyo na ni kinyume na vipengele vya Katiba ya Madagascar dhidi ya mateso na matibabu mengine ya kinyama, pamoja na viwango vya kikanda na vya Kimataifa vya Haki za Binadamu"

===========

Abolish castration law - Amnesty urges Madagascar

Madagascar should abolish a new law which allows for the chemical and surgical castration of people convicted of raping minors as it was "cruel, inhuman and degrading", rights group Amnesty International has said.

Last month, President Andry Rajoelina proposed the amendments to the penal code - that include chemical and surgical castration as punishment for individuals found guilty of rape against minors.

These changes have since been agreed by MPs.

In a statement, Tigere Chagutah, Amnesty's regional director for east and southern Africa, said:

Quote Message: In Madagascar, rape cases remain under-reported, and perpetrators often go free due to the victims' and their families' fear of retaliation, stigmatisation, and a lack of trust in the judicial system.

Implementing chemical and surgical castration, which constitutes cruel, inhuman and degrading treatment, as a punishment for those found guilty of raping minors will not solve this and is inconsistent with Malagasy constitutional provisions against torture and other ill-treatment, as well as regional and international human rights standards."

Source: BBC
 
Huu upuuzi wa amnesty unaandaa binadamu wa hovyo Sheria Kali zinazosimamiwa vyema ndizo ndio zinazojenga jamii iliyo Bora mfano mzuri hapa kwetu tunawaza wezi Mali za Umma wauawe lkn huyo mtunga Sheria na mpitisha Sheria nae ni mwizi anakuja na vifungu vya amnesty.
 
Haya makosa ya emotion yanayotengeneza temporary insanity yanatakiwa yawe handled kwa tahadhari kubwa.

Tuna watoto wa kike wanaweza kuangukia mikononimwa watu wa hivyo na kuwa victims

Tuna watoto wa kiume wanakuwa, wapo wanaobalehe vibaya hasa wale wenye hormone nyingi za kiume ( testosterone) huwasababishia kichaa Cha muda ( adolescence insanity) kwa kipindi hicho Kila shimo analoliona hufikiri ni la kuchemeka tuu, akikutana na kuku twende, mbuzi twende, hapo kama hamjamshtukia mapema na kupewa ulinzi na ushauri nasihi atapotea

Sasa kijana wako anakutwa na Hali kama hiyo , ushahidi ni watertight anapotelea lela milele. Kwa wale ambao vijana wao wamepita hatua hiyo mapema wamshukuru Mungu lakini wajue pia Wana wajukuu, lazima tuwe karibu na kuchunguza mienendo ya vijana wetu.

Mtoto wako akitenda kosa hilo utasema sheria ni ya kikatili kweli kweli

Lakini binti yako mpendwa mdogo mwenye nidhamu, ana akili darasani mnamwandalia future nzuri anakutana na jitu Zima linamwaribu na kumharibia Maisha utaona hata hiyo miaka 30 haitoshi Bali alitakiwa auawe hadhatani.
 
Adhabu pendekezwa ua kuhasi ni kinuyume na haki za binadamu na kamwe haitasaidia kuondoa tatizo. Hata sheria ya Tanzania ya miaka 30 ni ukatili dhidhi ya utu. Adhabu ya ubakaji miaka 5 inatosha sana kwa mtu kujirekebisha.
 
Hii sheria sio nzuri kwa kweli ni ukatili imagine mwanao wa kiume kafanyiwa hivyo utajisikiaje kukosea kupo ila adhabu isiwe kubwa kuliko kosa zipo adhabu zinazoweza kumfanya ajutie makosa na sio mpaka umfanye walk in dead na vipi wanawake wanaobaka watoto wa kiume unakuta mtu mzima anamfundisha mtoto mdogo wa kiume ikiwa hajui kabisa kitendo chochote adhabu yake ikoje? Sawa mwanaume ni rahisi kukosea ila tukija kwenye swala la hukumu tusimame katikati mfano wanafunzi wa hapa tz inajulikana adhabu yake ukimpa mimba lakini hao hao wanafunzi wa kike wamekuwa nao ndio chanzo cha matatizo kuna siku moja nilikuwa sehemu nipo ndani ya nyumba kwa nje kulika na mwanafunzi wa kike na wakiume walisimama karibu na dirisha ikiwa hawanioni kwa ndani kama nawasikiliza cha ajabu mtoto wa kike ndie alikuwa akimtongoza mwanaume tena kwa hisia kama movie za Philippines na zawadi akampati so what next......
 
Zungumzia kuhasi bhana!

Kwani adhabu za makosa ya jinai huwa zinajali mtoto ama mjukuu wako kafanya?

Hii sheria ingelipitishwa na Tz maana Kuna mabazazi wengi sana.

Tuuone umwamba wao zikishatolewa watamfanyia nani.

Tena' zikishang'olewa wanatakiwa waachiliwe bila masharti.

Maana simba ukishaling'oa meno na kucha halina madhara yoyote hata ukulifuga nyumbani kwa mapambo.
 
Hayo unayasema kwa sababu hayajakutokea au halijatokea tatizo hilo kwenye Moja ya mpendwa mwanafamilia yako. Hayo unayasema kwa sababu unadhani mbakaji anatoka kwenye familia za watu wengine wenye malezi mabaya. Kumbe mbakaji anaweza kuwa mme wako mpendwa mwenye kazi na future nzuri hata ukimuuliza kilichomponza hawezi kujibu na ukimwangalia aliyembaka ama ni mtuto asiyejitambua au mwanamke wa ajabu ajabu

Anaweza kuwa mtoto au mjukuu wako mpendwa ambaye unamsomesha kwa garama english.medium na anaakili kweli na mshika dini. Ukifikiria kilichomponza unakosa jibu Kila ukienda kumsalimia magereza ukichungulia kule ndani alipowekwa na majambazi sugu magunjwa ya ajabu na ufirauni wa Kila aina unabugujikwa machozi na kuona future ya mtoto au mjukuu wako imefutika na hata akitoka kashaharibika sio yule tena. Kumbuka hata waliptunga hiyo sheria ya SOSPA walichukulia tuu upande mmoja kama wewe lakini ndugu yako akishapata janga ni janga la familia ,wote mnahangaika namna ya kumwokoa bila kujali kama ulishiriki kutunga hiyo sheria au la
 
Hii sheria sio nzuri kwa kweli ni ukatili imagine mwanao wa kiume kafanyiwa hivyo utajisikiaje kukosea kupo ila adhadu isiwe kubwa kuliko kosa zipo adhabu zinazoweza kumfanya ajutie makosa na sio mpaka kumfanye walk in dead na vipi wanawake wanaobaka watoto wa kiume unakuta mtu mzima anamfundisha mtoto mdogo wa kiume ikiwa hajui kabisa kitendo chochote adhabu yake ikoje? Sawa mwanaume ni rahisi kukosea ila tukija kwenye swala la hukumu tusimame katikati mfano wanafunzi wa hapa tz inajulikana adhabu yake ukimpa mimba lakini hao hao wanafunzi wa kike wamekuwa nao ndio chanzo cha matatizo kuna siku moja nilikuwa sehemu nipo ndani ya nyumba kwa nje kulika na mwanafunzi wa kike na wakiume walisimama karibu na dirisha ikiwa hawanioni kwa ndani kama nawasikiliza cha ajabu mtoto wa kike ndie alikuwa akimtongoza mwanaume tena kwa hisia kama movie za Philippines na zawadi akampati so what next......
Wewe unaongelea ubinafsi, eti: 'imagine nwanao wa kiume kufanyiwa'!

Sheria haifuati mwanao sijui nani Yako kafanya.

Kama mzazi unatakiwa kuwa nyuma ya maadili ya wanao.

Je anayebakiwa mwanaye mbona haujameongelea?

Hapa Tz adhabu hizo hatuna, lakini Kuna adhabu Kali sana mtu akipatikana na hatia ya kutenda.

Sasa nwanao akipatikana na hatia akafungwa 30 ama maisha, utakuwa na faida naye ipi?

Kikubwa tuwalee watoto kwa maadili,lakini adhabu Kali sana kwa makosa kama hayo ya kishenzi lazima zipitishwe na kutumika ili kukomesha ama kupunguza ushenzi katika jamii.

Tena' hii ya kuhasi ni bab kubwa na ni nzuri, hata Tanzania ingeasisiwa ili kulinda wanawake na watoto.
 
Sa
Hayo unayasema kwa sababu hayajakutokea au halijatokea tatizo hilo kwenye Moja ya mpendwa mwanafamilia yako. Hayo unayasema kwa sababu unadhani mbakaji anatoka kwenye familia za watu wengine wenye malezi mabaya. Kumbe mbakaji anaweza kuwa mme wako mpendwa mwenye kazi na future nzuri hata ukimuuliza kilichomponza hawezi kujibu na ukimwangalia aliyembaka ama ni mtuto asiyejitambua au mwanamke wa ajabu ajabu

Anaweza kuwa mtoto au mjukuu wako mpendwa ambaye unamsomesha kwa garama english.medium na anaakili kweli na mshika dini. Ukifikiria kilichomponza unakosa jibu Kila ukienda kumsalimia magereza ukichungulia kule ndani alipowekwa na majambazi sugu magunjwa ya ajabu na ufirauni wa Kila aina unabugujikwa machozi na kuona future ya mtoto au mjukuu wako imefutika na hata akitoka kashaharibika sio yule tena. Kumbuka hata waliptunga hiyo sheria ya SOSPA walichukulia tuu upande mmoja kama wewe lakini ndugu yako akishapata janga ni janga la familia ,wote mnahangaika namna ya kumwokoa bila kujali kama ulishiriki kutunga hiyo sheria au la
Sawa inauma, Sasa tufanyeje embu tusimame kwa wanaofanyiwa huo ukatili.

Au unashauri ni nini cha kufanya hasa baada ya kitendo hicho kufanyika?
 
Hii sheria sio nzuri kwa kweli ni ukatili imagine mwanao wa kiume kafanyiwa hivyo utajisikiaje kukosea kupo ila adhabu isiwe kubwa kuliko kosa zipo adhabu zinazoweza kumfanya ajutie makosa na sio mpaka umfanye walk in dead na vipi wanawake wanaobaka watoto wa kiume unakuta mtu mzima anamfundisha mtoto mdogo wa kiume ikiwa hajui kabisa kitendo chochote adhabu yake ikoje? Sawa mwanaume ni rahisi kukosea ila tukija kwenye swala la hukumu tusimame katikati mfano wanafunzi wa hapa tz inajulikana adhabu yake ukimpa mimba lakini hao hao wanafunzi wa kike wamekuwa nao ndio chanzo cha matatizo kuna siku moja nilikuwa sehemu nipo ndani ya nyumba kwa nje kulika na mwanafunzi wa kike na wakiume walisimama karibu na dirisha ikiwa hawanioni kwa ndani kama nawasikiliza cha ajabu mtoto wa kike ndie alikuwa akimtongoza mwanaume tena kwa hisia kama movie za Philippines na zawadi akampati so what next......
Kumbaka mtoto ni ukatili wa hali ya juu mno
 
Wewe unaongelea ubinafsi, eti: 'imagine nwanao wa kiume kufanyiwa'!

Sheria haifuati mwanao sijui nani Yako kafanya.

Kama mzazi unatakiwa kuwa nyuma ya maadili ya wanao.

Je anayebakiwa mwanaye mbona haujameongelea?

Hapa Tz adhabu hizo hatuna, lakini Kuna adhabu Kali sana mtu akipatikana na hatia ya kutenda.

Sasa nwanao akipatikana na hatia akafungwa 30 ama maisha, utakuwa na faida naye ipi?

Kikubwa tuwalee watoto kwa maadili,lakini adhabu Kali sana kwa makosa kama hayo ya kishenzi lazima zipitishwe na kutumika ili kukomesha ama kupunguza ushenzi katika jamii.

Tena' hii ya kuhasi ni bab kubwa na ni nzuri, hata Tanzania ingeasisiwa ili kulinda wanawake na watoto.
Tatizo wengi hamjui undani wa matukio kama haya kwanza ni matukio ambayo huwa hayana ushahidi wa wazi nikisema ushahidi wa wazi najua unaelewa kesi kama hii inategemea sana ushahidi wa kisayansi na ukumbuke kesi zinazohusisha ushahidi wa kisayansi ni mbaya sana kuliko tofauti na kesi nyingne mfano: "wewe umeniibia ushahidi ni kitu changu unacho na fulani amekuona kweli unacho tumehakikisha" hapo ushahidi upo wazi je ushahidi wa kisayansi nani anajua zaidi ya wataalam, ikiwa hujui hata kusoma tu kipimo cha malaria unategemea nini unahukumiwa kikatili kama hivyo hata ukirudi mtaa umepoteza kila futures wanaopinga sio wajinga sio kama wao wanapenda hayo matukio ya ukatili kwa watoto wa kike ila ushahidi wake una utata ni matukio ya siri na ikitokea hukumu kama hiyo ikaja huku kuna watu mtawaonea huruma tena msiombe maana hii nchi inakesi nyingi sana za kusingiziwa.
 
Adhabu pendekezwa ua kuhasi ni kinuyume na haki za binadamu na kamwe haitasaidia kuondoa tatizo. Hata sheria ya Tanzania ya miaka 30 ni ukatili dhidhi ya utu. Adhabu ya ubakaji miaka 5 inatosha sana kwa mtu kujirekebisha.
Nina vivid example tukiwa watatu ndani Mimi na dada zangu walibakwa na wezi na kuambukizwa ukimwi, kilichoniokoa nilikuwa mdogo
 
Tatizo wengi hamjui undani wa matukio kama haya kwanza ni matukio ambayo huwa hayana ushahidi wa wazi nikisema ushahidi wa wazi najua unaelewa kesi kama hii inategemea sana ushahidi wa kisayansi na ukumbuke kesi zinazohusisha ushahidi wa kisayansi ni mbaya sana kuliko tofauti na kesi nyingne mfano: "wewe umeniibia ushahidi ni kitu changu unacho na fulani amekuona kweli unacho tumehakikisha" hapo ushahidi upo wazi je ushahidi wa kisayansi nani anajua zaidi ya wataalam, ikiwa hujui hata kusoma tu kipimo cha malaria unategemea nini unahukumiwa kikatili kama hivyo hata ukirudi mtaa umepoteza kila futures wanaopinga sio wajinga sio kama wao wanapenda hayo matukio ya ukatili kwa watoto wa kike ila ushahidi wake una utata ni matukio ya siri na ikitokea hukumu kama hiyo ikaja huku kuna watu mtawaonea huruma tena msiombe maana hii nchi inakesi nyingi sana za kusingiziwa.
Nimekuelewa mkuu.
Mwenzako niliangalia sheria za haki zisizo na mushkeri kama USA au UK, hilo la nchi corrupt kama ya kwetu, ni kweli hukumu zinaweza kutoka za kirushwa wakatiwa hatiani wasiohusika.
 
Mbakaji atolewe KENDE 1 bila ganzi, au mzigo upasuliwe na nyundo, kuna vitendo vya kikatili saana, unabakaje wapo mpaka wadada wa buku 3.
 
Huu upuuzi wa amnesty unaandaa binadamu wa hovyo Sheria Kali zinazosimamiwa vyema ndizo ndio zinazojenga jamii iliyo Bora mfano mzuri hapa kwetu tunawaza wezi Mali za Umma wauawe lkn huyo mtunga Sheria na mpitisha Sheria nae ni mwizi anakuja na vifungu vya amnesty.
baba alimbaka mama yako ukazaliwa ukakuta kafanyiwa hivyo , tafakari
 
Back
Top Bottom