Familia yajiua Iringa

Familia yajiua Iringa

Magazetini

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
593
Reaction score
1,713

mungi.gif

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi.PICHA|MAKTABA

Kwa ufupi

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi na kwamba mama huyo alifariki dunia alipokuwa akipatiwa matibabu katika Zahanati ya Kilolo.

Kilolo
Mwanamke mmoja wa Kijiji cha Mtitu wilayani hapa, Grace Lubava (33), amemuua mtoto wake kwa sumu na kisha naye kujiua kwa njia hiyohiyo na baadaye mumewe, George King'ung'e (45), kujinyonga kwa kamba kutokana na vifo hivyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi na kwamba mama huyo alifariki dunia alipokuwa akipatiwa matibabu katika Zahanati ya Kilolo.

"Kifo cha mama na mtoto kilitokea baada ya mumewe kumzuia mkewe kwenda kumwona baba yake ambaye alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Tosamaganga," alisema Mungi.

Alisema kuwa mume alimzuia mke huyo kwenda hospitali kwa madai kuwa alikuwa anakwenda kwenye mambo yake binafsi jambo ambalo lilimkera mwanamke huyo kiasi cha kufikia uamuzi huo.

Kamanda Mungi alisema baada ya King'ung'e kubaini vifo hivyo na msingi wake, aliamua kwenda porini na kujinyonga.

CHANZO: Mwananchi
 
wazawa wa iringa majanga sana aisee,hasira za kunyimwa kwenda kumuona baba yako ndio uamue kumuua mwanao ambaye hajui kabisa source ya mzozo wenu,na wewe mwenyewe kuamua kujiua,mume naye akaamua kufuata mkondo ule ule..........hichi ni kitu cha ajabu kabisa.
 
yani kitu kidoogo unaamua kujiom=ndoa na mtoto pia amani .... hivi watu wa huko wangekuwa kule wanakojitoa muhanga wangekuwa hili kabila limeisha aisee.... maumuzi magumu sana haya
 
aleeeee............mweeeehhhhhh
shemej yangu TIQO tuonane kesho jion mitaa ya gangilonga ama sjui kihesa utaamua wewe
 
Last edited by a moderator:
Kumbuka tangu enzi za Mkwawa hawa nmpi watu wa kujitoa mhanga. Hawa wanawafaa sana La Shabaab
 
ivi ni hasira tu !?? Au mapepo..?
Noma sana,
 
Back
Top Bottom