Familia ya Tundu Lissu yatoa tamko "tumeandika barua 11"

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,293
24,173
July 1, 2019

Msemaji wa familia ya Tundu Lissu, wakili wa kujitegemea Bw. Alute Mughwai amesema wamekuwa na mawasiliano na Bunge kupitia barua 11 zilizojibiwa.

Msemaji wa familia anabainisha yanayoendelea sasa kuhusu kufukuzwa ubunge waliyategemea kutokea.

Moja ya barua inasema madaktari bingwa watatu wangeenda Nairobi kuangalia afya ya mgonjwa Tundu Lissu ili wizara ya afya ya Tanzania iweze kumpatia msaada mgonjwa Tundu Lissu kufuatana na mahitaji yake halisi ya Kiungonjwa na majeraha. Familia iliombwa kutoa ushirikiano kwa madaktari hao wakifika jijini Nairobi, Kenya ili kufanikisha kazi za madaktari hao bingwa toka Tanzania.

Kutokana na taratibu za kiserikali, kabla madaktari wa wizara hiyo hawajafika Nairobi, mgonjwa alihamishiwa Belgium kwa matibabu zaidi. Hivyo tena familia iliifahamisha Bunge kwa barua kuwa Tundu Lissu amehamishiwa Ubelgiji na familia kuipatia anuani ya mahali ilipo hospitali na mgonjwa nchini Ubelgiji.

Ofisi ya Bunge ilikiri kupata barua ya familia kwa kuihakikishia itawasiliana na wizara ya Afya ili kujua taratibu zitakazofuata. Barua hiyo ya ofisi ya Bunge mbali ya kuijibu familia ya Lissu pia nakala yake ilinakiliwa kwa Spika Job Ndugai na Mh.Tundu Antipas Lissu kupitia anuani ya hospitali na mtaa ya huko Luvern Belgium kwa taarifa.

Wakili wa Kujitegemea Alute Mughwai kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hajui mbunge Tundu Antipas Lissu hajulikani alipo haina mashiko.

Kuhusu Tundu Lissu kushindwa kujaza fomu toka Sekretariati ya viongozi ya Maadili ya Umma, wakili Alute Mughwai alisema fomu hizo kisheria hutakiwa hujazwa kila mwaka na viongozi na kuzirejesha tarehe 31 December kila mwaka. Wakili Mughwai anasema hicho ni kizingizio kipya.

Maana Tundu Lissu hakuweza kujaza fomu za udhuru wa kwenda kutibiwa Nairobi na vivyo hivyo mbunge Tundu Lissu asingeweza kujaza fomu za Maadili wa Viongozi wakati akiendelea na matibabu ya majeraha nje ya Tanzania.

Itakumbukwa kwa miezi minne jijini Nairobi, Kenya Tundu Lissu alikuwa amelazwa ktk chumba cha wagonjwa mahututi yaani ICU anakumbushia wakili Alute Mughwai msemaji wa familia. Na anaongeza wakili Mughwai kuwa hata siku Tundu Lissu anasafirishwa kwenda Belgium kwa matibabu bingwa alichukuliwa kwa machela na ambulance mpaka uwanja wa Jomo Kenyatta International Airport uliopo jijini Nairobi, Kenya.

Mazingira yote haya ya mgonjwa Tundu Lissu, ofisi ya Bunge ilikuwa inayafahamu kwa mawasiliano rasmi ya barua zilizojibiwa kiofisi.

Wakili Alute Mughwai amesema fomu za Maadili kutoka ofisi ya Sekretariati ya Maadili ya Viongozi wa umma kiutaratibu hupelekwa Bungeni, ambapo mbunge huzichukua ofisi ya Bunge, kuzijaza na kisha kuziacha ofisi ya Bunge huku nakala ikibaki ofisi ya Bunge na jukumu la kurejesha fomu ofisi ya Sekretariati ya Maadili ni la Ofisi ya Bunge. Wakili Alute alitegemea Ofisi ya Bunge kuitaarifu ofisi ya Sekretariati ya Maadili juu ya udhuru wa matibabu ya mbunge Tundu Lissu.

Vile vile wakili Alute Mughwai anauliza ilishindikana vipi ofisi ya Bunge kumpelekea fomu za Maadili ya Viongozi Mh. Tundu Lissu kwa anuani ya hospitali na hata c/o ubalozi wa Tanzania Belgium au hata kwa familia iliyokuwa inawasiliana nayo kwa ukaribu kupitia barua.

Hitimisho : msemaji wa familia, wakili wa kujitegemea Alute Mughwai akiongea kwa utulivu wa mwanasheria-msomi nguli huku akiwa amesheheni hoja zenye mashiko na shauku ya kuingia kilinge cha kupambanisha hoja za kisheria mbele ya Waheshimiwa Majaji kupata mizania inayoegamia haki, amesema sakata hili ni la kutengeneza na kutegeana. Hivyo kama alivyosema Tundu Lissu kuamua kwenda mahakamani kutafuta haki yake, familia inamuunga mkono na watakuwa naye katika kutafuta kupata haki yake.
Source : millard ayo
 
Hivi ndivyo CCM inavyoangamia kwa kukosa viongozi wenye maarifa!!!

Hii kesi kama kweli wataifungua,ni wazi hata mtoto wa darasa la saba anaweza kusimama kama wakili wa Lissu na akishinda kesi!!

Alafu hao madaktari walishindwa kwenda au kuna mtu aliwazuia?

Na Madaktari hawa, kweli wangeamua kutokwenda hivi hivi na hata kupoteza perdiem?

Nawaza kwa herufi kubwa!!
 
Alichofanyiwa TAML ni uonevu uliokithiri na tusimlaumu Ndugai isipokuwa kama hatumjui wa kumlaumu.

Ninawasihi watanzania tumuombee sana TAML na familia yake wanapopitia katika jaribu hili la pekee sana. MUNGU awasimamie na kueashindia hata mahakamani. Ushindi wao mahakamani dhidi ya udhalimu na uonevu, ni ushindi wa watanzania wote.
 
July 1, 2019

Msemaji wa familia ya Tundu Lissu, wakili wa kujitegemea Bw. Alute Mughwai amesema wamekuwa na mawasiliano na Bunge kupitia barua 11 zilizojibiwa.

Msemaji wa familia anabainisha yanayoendelea sasa kuhusu kufukuzwa ubunge waliyategemea kutokea.

Moja ya barua inasema madaktari bingwa watatu wangeenda Nairobi kuangalia afya ya mgonjwa Tundu Lissu ili wizara ya afya ya Tanzania iweze kumpatia msaada mgonjwa Tundu Lissu kufuatana na mahitaji yake halisi ya Kiungonjwa na majeraha. Familia iliombwa kutoa ushirikiano kwa madaktari hao wakifika jijini Nairobi, Kenya ili kufanikisha kazi za madaktari hao bingwa toka Tanzania.

Kutokana na taratibu za kiserikali, kabla madaktari wa wizara hiyo hawajafika Nairobi, mgonjwa alihamishiwa Belgium kwa matibabu zaidi. Hivyo tena familia iliifahamisha Bunge kwa barua kuwa Tundu Lissu amehamishiwa Ubelgiji na familia kuipatia anuani ya mahali ilipo hospitali na mgonjwa nchini Ubelgiji.

Ofisi ya Bunge ilikiri kupata barua ya familia kwa kuihakikishia itawasiliana na wizara ya Afya ili kujua taratibu zitakazofuata. Barua hiyo mbali ya kuijibu familia ya Lissu pia nakala yake ilipelekwa kwa Spika Job Ndugai kwa taarifa.

Source : millard ayo

Short chasis anayajua haya yote. Tatizo ni shinikizo toka kwa Tanzania Breweries.
Bahati mbaya sana, Short chasis hawezi kusimamia mhimili wake. Anekuwa mateka was TBL.
 
Alichofanyiwa TAML ni uonevu uliokithiri na tusimlaumu Ndugai isipokuwa kama hatumjui wa kumlaumu.

Ninawasihi watanzania tumuombee sana TAML na familia yake wanapopitia katika jaribu hili la pekee sana. MUNGU awasimamie na kueashindia hata mahakamani. Ushindi wao mahakamani dhidi ya udhalimu na uonevu, ni ushindi wa watanzania wote.
Na tunatoa wito kwa Chadema kuilinda familia ya Lissu ili isije kupotezwa kwa lengo la kuficha ushahidi
 
Back
Top Bottom