Familia ya Tundu Lissu yapingana na CHADEMA sakata la yeye kupigwa risasi

Familia ya Tundu Lissu yapingana na CHADEMA Sakata la Yeye Kupigwa Risasi

Wakati Chama cha Demokrasia na Maendeleo, kikisisitiza uchunguzi wa kushambuliwa Mbunge Tundu Lissu ufanywe na vyombo vya kimataifa familia yake imezungumza kuhusiana na tukio hilo na kusema wao hawana mashaka na jeshi la polisi kufanya uchunguzi.

Kauli hiyo ya familia imetolewa Jijini Arusha na Wakili Alute Mughwai ambaye ni kaka wa Tundu Lissu ambapo amesema mpaka sasa familia haijatoa maamuzi ya moja kwa moja ni nani achunguze tukio hilo lakini mpaka sasa wana imani na uchunguzi unaofanywa na jeshi la polisi.

Wakili Mughwai amesema pindi familia ikikaa kwa mara nyingine watazungumzia suala hilo na kuja na kauli nyingine ya pamoja ya familia kuhusiana na msimamo wao wa ni nani afanye uchunguzi wa tukio hilo kama kutakua na ulazima wa kufanya hivyo.

"Hatujakaa sisi kama wanafamilia kutoa msimamo wetu kuhusiana na uchunguzi wa tukio hilo, kwamba hatuna imani na jeshi la polisi na uchunguzi ufanywe na vyombo vya kimataifa lakini kama tukikutana tukawa na msimamo wetu tutatoa maoni yetu kama haja itakuwepo," amesema Mughwai.

Aidha ameongeza kwamba wao kama familia hawana tatizo lolote la kibiashara, wala hawana tatizo na Tundu Lissu hivyo watu wasije wakaunganisha matukio na kuhusisha kushambuliwa kwake na matukio ya biashara na kuongeza kuwa ndugu yao siyo mfanyabiashara bali biashara yake ni siasa pamoja sheria.

Mbali na hayo amewataka jeshi la polisi kuanzia uchunguzi wao kwa kufuatilia mkutano aliokuwa akizungumzia suala la Bombadier kukwama nchini Canada na alipozungumzia suala la kufuatiliwa na watu asiowafahamu.

Hata hivyo Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema jana kilisema kinahitaji serikali iruhusu wachunguzi wa kimataifa kuingia nchini kufanya uchunguzi juu ya shambulio la kupigwa risasi kwa Mbunge na Mwanasheria wao Tundu Lissu mnamo Septemba 7 mwaka huu mchana eneo la 'Area D' mjini Dodoma

Kwani ni vibaya familia kusema hivyo na Chadema kusema kama walivyosema? Kwangu mimi sioni shida maana watu wanatofautiana mawazo na maono. Si unaona hata kwa kesi ya Uhuru Kenyatta? Majaji 5 walikubali matokeo ya uchaguzi mkuu Kenya yafutwe na urudiwe na 2 waka'dissent'. Hii siyo dhambi ya mauti. People don't think uniformly.
 
Dereva ni shahidi namba 1 na ni suspect no 1 wamlete Dar kwanini wamemficha Nairobi? Siku hiyo hiyo dereva alipaswa kunyang'wana simu yake ibaki na polisi kwa upepelezi, mwenyewekiti unawasiwasi na nini kumficha shahidi no 1? ???
Ndugu binafsi sijawahi kuwaamini polisi, ktk hili la Lissu polisi wamekuwa reluctant sana kuchukua hatuwa, ni kama vile wanasubiria kuambiwa la kufanya, upepo kwanza unasomwa kisha tamko linatolewa.
 
Dereva ni shahidi namba 1 na ni suspect no 1 wamlete Dar kwanini wamemficha Nairobi? Siku hiyo hiyo dereva alipaswa kunyang'wana simu yake ibaki na polisi kwa upepelezi, mwenyewekiti unawasiwasi na nini kumficha shahidi no 1? ???
dereva ni mwanafamilia....
 
Huyu nae atakuwa amekipenda cheo kipya huko ccm cha mtu/mwanafamilia asiye eleweka
Ushenzi mtupu
1. Hatujakaa kama familia.....tukikaa tutatoa.....

2. Kama familia hatuna mashaka na polisi

Which is which here?[/QUOTE Huyu nae atakuwa mwanafamilia asiye eleweka familiani
 
Familia ya Tundu Lissu yapingana na CHADEMA Sakata la Yeye Kupigwa Risasi

Wakati Chama cha Demokrasia na Maendeleo, kikisisitiza uchunguzi wa kushambuliwa Mbunge Tundu Lissu ufanywe na vyombo vya kimataifa familia yake imezungumza kuhusiana na tukio hilo na kusema wao hawana mashaka na jeshi la polisi kufanya uchunguzi.

Kauli hiyo ya familia imetolewa Jijini Arusha na Wakili Alute Mughwai ambaye ni kaka wa Tundu Lissu ambapo amesema mpaka sasa familia haijatoa maamuzi ya moja kwa moja ni nani achunguze tukio hilo lakini mpaka sasa wana imani na uchunguzi unaofanywa na jeshi la polisi.

Wakili Mughwai amesema pindi familia ikikaa kwa mara nyingine watazungumzia suala hilo na kuja na kauli nyingine ya pamoja ya familia kuhusiana na msimamo wao wa ni nani afanye uchunguzi wa tukio hilo kama kutakua na ulazima wa kufanya hivyo.

"Hatujakaa sisi kama wanafamilia kutoa msimamo wetu kuhusiana na uchunguzi wa tukio hilo, kwamba hatuna imani na jeshi la polisi na uchunguzi ufanywe na vyombo vya kimataifa lakini kama tukikutana tukawa na msimamo wetu tutatoa maoni yetu kama haja itakuwepo," amesema Mughwai.

Aidha ameongeza kwamba wao kama familia hawana tatizo lolote la kibiashara, wala hawana tatizo na Tundu Lissu hivyo watu wasije wakaunganisha matukio na kuhusisha kushambuliwa kwake na matukio ya biashara na kuongeza kuwa ndugu yao siyo mfanyabiashara bali biashara yake ni siasa pamoja sheria.

Mbali na hayo amewataka jeshi la polisi kuanzia uchunguzi wao kwa kufuatilia mkutano aliokuwa akizungumzia suala la Bombadier kukwama nchini Canada na alipozungumzia suala la kufuatiliwa na watu asiowafahamu.

Hata hivyo Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema jana kilisema kinahitaji serikali iruhusu wachunguzi wa kimataifa kuingia nchini kufanya uchunguzi juu ya shambulio la kupigwa risasi kwa Mbunge na Mwanasheria wao Tundu Lissu mnamo Septemba 7 mwaka huu mchana eneo la 'Area D' mjini Dodoma
Nililijua hili vijana wa UVCCM wengi wenu mna akili ndogo sana sana ya kuelewa mtu anacho kiongea na mmenyimwa kabisa upeo vichwani mwenu ndio maana wengi wenu mazuzu,

kaka yake lissu kumuelewa kile alicho kiongea inakubidi uwe na akili ya kawaida kabisa ya kureason lakin vijana wa UVCCM mmeshindwa kabisaaa yaani mmetoka weupeee habu fuatilia matamshi yake kwa umakini sana utaelewa nini kipo moyoni mwake tena kwa uwazi kabisa , mpangilio wa hoja zake unaeleza kabisa ana fikra gani juu ya tukio la lissu lakin kwa vile hamna akili na uelewa wenu ni mdogo mtoka kapa mmekuja mbio mbio huku kama mazuzu
 
Huyu naye hajitambuwi,Mara hatujakaa kama familia,mara ooo hii ni kauli ya familia.
 
Dereva ni shahidi namba 1 na ni suspect no 1 wamlete Dar kwanini wamemficha Nairobi? Siku hiyo hiyo dereva alipaswa kunyang'wana simu yake ibaki na polisi kwa upepelezi, mwenyewekiti unawasiwasi na nini kumficha shahidi no 1? ???
Kwani hiyo namba haiwezi kuwa traced electronically??
Mbona za wanaotuma msg zinapatikana fasta?
Kama huu uvamizi ungefanywa na mtu wa upinzani angekuwa alishakamatwa ili wapate Kiki ya kuongelea.

Kwa sababu ni wao wameamua waje na cinema ya meja kuvamiwa na kutolewa risasi.
Taarifa zinapatikana Baada ya Rais kufika kumuona na operation imeshafanyika!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom