Familia ya Tundu Lissu yapingana na CHADEMA sakata la yeye kupigwa risasi

Nililijua hili vijana wa UVCCM wengi wenu mna akili ndogo sana sana ya kuelewa mtu anacho kiongea na mmenyimwa kabisa upeo vichwani mwenu ndio maana wengi wenu mazuzu,

kaka yake lissu kumuelewa kile alicho kiongea inakubidi uwe na akili ya kawaida kabisa ya kureason lakin vijana wa UVCCM mmeshindwa kabisaaa yaani mmetoka weupeee habu fuatilia matamshi yake kwa umakini sana utaelewa nini kipo moyoni mwake tena kwa uwazi kabisa , mpangilio wa hoja zake unaeleza kabisa ana fikra gani juu ya tukio la lissu lakin kwa vile hamna akili na uelewa wenu ni mdogo mtoka kapa mmekuja mbio mbio huku kama mazuzu
Wewe umeelewaje? Au imekuchoma?
 
Nini maana ya kupinga? Chadema kama chama imetoa msimamo wao wa kutaka uchunguzi ufanywe na vyombo HURU ambavyo labda wanaamini vinapatikana zaidi nje ya nchi!! Familia inasema ina imani na jeshi la polisi! Na hapo hapo inasema itakapokaa itatoka na maamuzi/maoni yao(juu ya nani achunguze?)! Wapi wamepingana? Mmoja keshatoa msimamo wake(kuhusu uchunguzi!!!) mwingine kasema atatoa msimamo wake baadaye! Kwani baadaye imeshafika?hata mimi naliamini jeshi la polisi kwa mambo fulani! Kama tu ninavyoweza kuiamini intarahamwe kwa umahiri wao juu ya mambo fulani!
kwanini chama kitoe msimamo wake bila kushirikisha familia as if mhanga ni ALIEN?, after all, bado familia inasisitiza kuwa "pale itakapoona" ni muhimu kuwa na uchunguzi" watatoa mapendekezo yao kama familia. Kwanini chama kina "overide" familia????
 
Familia ya Tundu Lissu yapingana na CHADEMA Sakata la Yeye Kupigwa Risasi


Wakati Chama cha Demokrasia na Maendeleo, kikisisitiza uchunguzi wa kushambuliwa Mbunge Tundu Lissu ufanywe na vyombo vya kimataifa familia yake imezungumza kuhusiana na tukio hilo na kusema wao hawana mashaka na jeshi la polisi kufanya uchunguzi.

Kauli hiyo ya familia imetolewa Jijini Arusha na Wakili Alute Mughwai ambaye ni kaka wa Tundu Lissu ambapo amesema mpaka sasa familia haijatoa maamuzi ya moja kwa moja ni nani achunguze tukio hilo lakini mpaka sasa wana imani na uchunguzi unaofanywa na jeshi la polisi.

Wakili Mughwai amesema pindi familia ikikaa kwa mara nyingine watazungumzia suala hilo na kuja na kauli nyingine ya pamoja ya familia kuhusiana na msimamo wao wa ni nani afanye uchunguzi wa tukio hilo kama kutakua na ulazima wa kufanya hivyo.

"Hatujakaa sisi kama wanafamilia kutoa msimamo wetu kuhusiana na uchunguzi wa tukio hilo, kwamba hatuna imani na jeshi la polisi na uchunguzi ufanywe na vyombo vya kimataifa lakini kama tukikutana tukawa na msimamo wetu tutatoa maoni yetu kama haja itakuwepo," amesema Mughwai.

Aidha ameongeza kwamba wao kama familia hawana tatizo lolote la kibiashara, wala hawana tatizo na Tundu Lissu hivyo watu wasije wakaunganisha matukio na kuhusisha kushambuliwa kwake na matukio ya biashara na kuongeza kuwa ndugu yao siyo mfanyabiashara bali biashara yake ni siasa pamoja sheria.

Mbali na hayo amewataka jeshi la polisi kuanzia uchunguzi wao kwa kufuatilia mkutano aliokuwa akizungumzia suala la Bombadier kukwama nchini Canada na alipozungumzia suala la kufuatiliwa na watu asiowafahamu.

Hata hivyo Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema jana kilisema kinahitaji serikali iruhusu wachunguzi wa kimataifa kuingia nchini kufanya uchunguzi juu ya shambulio la kupigwa risasi kwa Mbunge na Mwanasheria wao Tundu Lissu mnamo Septemba 7 mwaka huu mchana eneo la 'Area D' mjini Dodoma
Kwa hiyo hao wana familia watakapo kaa huenda wakaamua arudishwe nchini Tanzania ili aendelee na matibabu akiwa hukohuko nchini
 
Ni kweli huyo Alute namfahamu ni ndugu yake ni mwanasheria pia na ni kada wa ccm na ni mpinzani mkubwa wa Lisu ndugu yake kwenye siasa. Waliwahi simama mahakamani Lisu akimtetea mbunge wa chadema na Alute akimtetea wa ccm lakin haitoshi nimeshuhudia Lisu akifanya mkutano singida na huyo bwana akainua mkono na kuuliza swali la kumpinga ndugu yake . Sitegemei hata siku mmoja kama Alute aende kinyume na ccm

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwa nini polisi hawakumnyang'anya hiyo simu, unataka kutuambia alikimbia au walishindwa kufanya hivyo?!
kama wanamtaka kwa nini wasimfuate hapo Kenya, kani pale ni sayari nyingine kusikofikika?! Acha kubinuka sarakasi wakati huna nguo za ndani
Kwa kukusaidia punguza ujinga, Polisi wa Tz hawana mamlaka kwenda Kenya kumchukua mtu ni anaombwa toka Polisi wa Kenya hapo kuna mawili kukubaliwa au kukataliwa!..
mwisho wa mamlaka ya polisi wa Tanzania ni mpakani
 
kwahiyo lissu hajapigwa risasi? sielewi hiyo familia inapinga kitu gani.
Familia haipingi ila UVFISIEM ndio wanailisha familia maneno mengine ili kutoa picha tofauti!

Hivi wale walinzi wa pale Area D wameshakamatwa ili wasaidie upelelezi?
 
Dereva ni shahidi namba 1 na ni suspect no 1 wamlete Dar kwanini wamemficha Nairobi? Siku hiyo hiyo dereva alipaswa kunyang'wana simu yake ibaki na polisi kwa upepelezi, mwenyewekiti unawasiwasi na nini kumficha shahidi no 1? ???
Wenzetu hawataki kabisa kujadili hili! Mimi nasema yawezekana dereva wamemuweka 'kizuizini'! si kwa hiyari yake.
 
Kwa kukusaidia punguza ujinga, Polisi wa Tz hawana mamlaka kwenda Kenya kumchukua mtu ni anaombwa toka Polisi wa Kenya hapo kuna mawili kukubaliwa au kukataliwa!..
mwisho wa mamlaka ya polisi wa Tanzania ni mpakani
kesi kubwa hii, kwa hiyo ukiwa WANTED NCHI ZA NJE NA UNAJULIKANA ULIPO, Haiwezekani kupatikana. Mahojiana yanaweza kupatikana tusitiane ujinga. INTERPOL ?? kuna kuficha kitu!!
 
Back
Top Bottom