Familia ya Lissu yafanya kikao na uongozi wa Bunge. Washindwa kufikia muafaka baada ya CHADEMA kukosa mwakilishi

Siamini kama lisu ATAKUJA KUKAA MEZA MOJA NA NDUGAI KUJADILI MATATIZO YAKE.
OK tuyaache haya.
Lisu kuna kitu anachoamini kuhusu kushambuliwa kwake.sidhan kama ataweza kukaa nao.

..TL alishasema kutibiwa ni haki yake kama mbunge.

..Na alitoa maagizo familia isiandike barua ya maombi.

..Baada ya msimamo huo sasa ndiyo kimekuja kikao cha bunge, familia, na chadema.

..Na wameshindwa kuchukua maamuzi kwasababu chadema hawakuwa na mwakilishi.

..Kwa kifupi itakuwa ni kashfa kubwa kama TL atarudi nchini bila kuwa amepatiwa haki yake ya matibabu na Bunge. Na hicho ndicho Ndugai anajitahidi kukiepuka hapa.
 
Binafsi sioni tatizo kwa Bunge hata wsipomhudumia, tatizo naloona kwanini CHADEMA wanafanya siasa kwenye stahiki za Lissu kama mtmishi siasa wafany lakini wamuache mwenzao apate haki zake. Pongezi kwa Familia kwa kuliona hilo
 
Sawa.moyo Wa MTU kichaka.Mimi nadhani angeumwa malaria ndo ingekuwa haki yake kutibiwa na bunge lakini si kushambuliwa na risasi.
 
Hizi ni zilipendwa za Diamond, ukurasa mpya umefunguliwa na bora Chadema wamewekwa pembeni, maana wale ni wajinga wanachotaka ni kutafuta umaaeufu wa kisiasa bila kujali Lissu anaumia vipi

Mjinga ni wewe na Lumumba wote.
 
Ushahidi wa mitandaoni? Anayejua visuri issue hiyo ni Dereva wa Lussu, wamuachie waone kama mtego wa oanya hautanasa wasiokuwepo

Hapana, hata dereva hajui vizuri anayejua ni Lissu atakuja kuongea mwenyewe maana yeye ndiye aliyesikia uchungu wa risasi.
 
View attachment 600952

Wakati Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu akiendelea na matibabu katika Hospitali ya Nairobi, familia yake imefanya kikao cha siri na uongozi ya Bunge kujadili matibabu ya mbunge huyo.

Kikao hicho kimefanyika leo Jumatatu jijini Dar es Salaam na imeelezwa kimehudhuriwa na Spika Job Ndugai, Naibu Spika, Dk Tulia Ackson, Katibu wa Bunge, Thomas Kashilila, Mbunge wa Vunjo, James Mbatia, Mbunge wa Hanang’, Dk Mary Nagu na ndugu watatu wa Lissu, wanaume wawili na mwanamke mmoja.

Kikao hicho kilianza asubuhi, na ilipofika saa 7:40 mchana, alitoka Mbatia akielekea kwenye gari lake baada ya kumaliza kikao hicho. Mwandishi alimfuata kujua kilichojiri ndani ya kikao hicho, Mbatia alikiri kuwepo kwa kikao hicho lakini hakutaka kuzungumza lolote na kuelekeza aulizwe Spika Ndugai.

“Ni kweli tulikuwa kwenye kikao na familia ya Lissu, lakini siwezi kusema tumezungumzia nini. Kwa taarifa zaidi nendeni kwa Spika au Katibu wa Bunge, walikuwepo pia ndugu zake watatu, wafuateni wanaweza kuwaeleza,” alisema Mbatia.

Msemaji wa familia ya Lissu, Alute Mughwai alipotafutwa alisema kikao hicho kimefanyika kati ya familia na uongozi wa Bunge kuhusu mambo yanayomhusu Lissu, hata hivyo alisema hakijakamilika kwa sababu ya kukosekana kwa upande wa Chadema.

Mughwai alisema kikao hicho kimeahirishwa mpaka wakati mwingine pande zote zitakapotimia ili kulijadili suala hilo kwa ukamilifu wake. Alisema Chadema kupitia kwa mwenyekiti wake Freeman Mbowe walipewa mwaliko lakini hawakuweza kufika.

“Siwezi kukwambia tumezungumzia nini, moja ya masharti tuliyopeana ni kutokusema hadharani mambo tuliyoyajadili lakini yanamuhusu Lissu. Wote ‘interest’ yetu ni kuona Lissu anapona na kuendelea na majukumu yake kama kawaida,” alisema Mughwai.

Hata hivyo, jitihada za kumtafuta Spika wa Bunge pamoja na Katibu wa Bunge zilishindikana baada ya simu zao kuita bila kupokelewa.

Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano, Uenenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema alipoulizwa kuhusu kikao hicho amesema taarifa kuhusu kikao hicho zilipelekwa Ofisi ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na siyo kwenye chama.

Mpekuzi

Shida haina ubabe wala kiburi.
 
Binafsi sioni tatizo kwa Bunge hata wsipomhudumia, tatizo naloona kwanini CHADEMA wanafanya siasa kwenye stahiki za Lissu kama mtmishi siasa wafany lakini wamuache mwenzao apate haki zake. Pongezi kwa Familia kwa kuliona hilo
Hivi mkuu mbona unaandika kama vile Lissu haongei!!?? Ni mgonjwa ndiyo lakini anaongea na kila kitu kina baraka zake. Unaandika kama vile maamuzi yanafanyika bila yeye kushirikishwa. Nadhani unamfahamu vizuri Lissu na pia unaufahamu msimamo wake.......
 
Familia imeamua kuweka siasa pembeni, nyie mapovu yanawatoka, mtoto wao akifa yenyewe ndiyo itaathirika siyo Chadema , Lema wala Mbowe. Na ukiona kikao ambacho Mbatia amehudhuria kwa siri ujue amewapuuza Chadema, Mbatia ana busara sana, anajua kuona jambo la kipumbavu na kulipuuza
wee ndio mpuuzi na propaganda zako za kijinga, familia inatambua mchango wa cdm, ndio maana wakasema lazima wawepo
 
Drama gani wakati tukio lilipigwa na Chadema kiki ya Siasa na uoga wa kuwa ingebidi wamsimamishe yeye.. ha ha haaaaa

Subirini waanze kudhulumiana kwanza wenyewe waropoke.. huku upande mwingine wale wakiangalia huku wameshika mabomu ya kuwalipua.. upinzani kwishney
Alafu dereva wamemficha wakati huohuo wanataka uchunguzi wa haraka!
 
Binafsi sioni tatizo kwa Bunge hata wsipomhudumia, tatizo naloona kwanini CHADEMA wanafanya siasa kwenye stahiki za Lissu kama mtmishi siasa wafany lakini wamuache mwenzao apate haki zake. Pongezi kwa Familia kwa kuliona hilo

..Ndugai na Ummy Mwalimu walikosa ubinadamu kwa kumsusia TL wakati akiwa ktk hali mbaya na hatihati ya kukata roho.

..Wangefanya maamuzi sahihi na ya kibinadamu wakati ule bunge na taifa lingeepushwa na fedheha hii.

..Chadema hawajamzuia TL kupata haki zake. Mbowe alishaeleza kwamba hana tatizo na familia kuiomba serikali imtibu TL.
 
Back
Top Bottom