Familia ya bilionea Mrema yasambaratika, mali zapotea ovyo

Waziri2025

Senior Member
Sep 2, 2019
148
379
Mpasuko mkubwa umezikumba familia za Marehemu bilionea, Faustine Mrema aliyefariki Agosti, 2018 baada ya wajane kuanza kutuhumiana kwa ubadhilifu wa mali na kufikishana mahakamani.

Mke mkubwa wa Marehemu, bi Janeth Kimaro na watoto wawili wa Marehemu, Michelle Mrema na Vivian Mrema ambao ni wasimamizi wa Mirathi za Marehemu wamepingwa mahakamani kwa madai ya kufuja mabilioni ya fedha za marehemu zinazodaiwa kufikia kiasi cha sh. bilioni 1 bila kuwashirikisha ndugu wengine.

Kesi hiyo namba 5 ya mwaka 2020 na kesi namba 20 ya mwaka 2020 zimefunguliwa katika mahakama kuu kanda ya Arusha, mbele ya jaji Robert Kassimu huku walalamikaji wakiwa ni wajane wa marehemu ambao ni Frida Mberesero na Veliani Maleko na wengine wakimpinga Mjane mkubwa wa Marehemu kuwa wasimamizi wa Mirathi.

Wakili wa upande wa mashtaka, Yusufu Mlekwa na Gwakisa Sambu walisema kuwa wateja wao wanawapinga wasimamizi wa Mirathi wakitaka waondolewe kwa madai kwamba wameshindwa kukusanya na kugawa Mali kwa wanufaika katika kipindi cha miezi sita tangu wateuliwe Julai 23, 2019.

Madai mengine ni Matumizi mabaya ya Mali za Marehemu bila kuwashirikisha ndugu wengine, kujimilikisha baadhi ya Mali kinyume na utaratibu na kushindwa kulipa madeni kama utaratibu unavyoelekeza.

Kesi hizo zimeahirishwa na zitatajwa tena mahakamani hapo, Septemba 1 na 7 mwaka huu.

Baadhi ya Mamilioni yaliyochotwa na wasimamizi wa Mirathi kinyume na utaratibu ni kiasi cha shilingi ,Mil.70,000,000 zilizotolewa tarehe 11.7.2019 Sh. 40,000,000 zilizotolewa tarehe 19.9.2019 sh. 50,000,000 tarehe 24.12.2019 Sh. 14,000,000.

Wakati mamilioni ya fedha hizo zikitumika kinyume na utaratibu wafanyakazi wa hotel ya Impala na Naura wakikosa mishahara kwa.zaidi ya miezi 7 inayofikia kiasi cha zaidi ya milioni 700.

images%20(2).jpg
 
Back
Top Bottom