Familia hii imechanganyikiwa

Familia hii imechanganyikiwa

Gobole Lenye Risasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2014
Posts
11,519
Reaction score
23,693
Mzee Ulaya ni dereva wa miaka mingi wa magari ya mizigo yanayoenda Zambia na nchi nyingine kusini mwa Afrika.

Mtoto wake wa kwanza a.k.a Mzimu naye alipenda kazi ya babaye, ameangukia katika kazi hiyo hiyo ya udereva wa magari ya mizigo masafa marefu.

Mzee ulaya kama walivyo madereva wengi alifanikiwa kupata mwanamke pale tunduma wa kusukuma siku wakiwa kwenye folenu border.binti mmoja mzuri.

Na pia mtoto wake Mzimu naye kama ilivyo ada kwa madereva akawa amejiwekea kituo eneo hilo hilo alipata Mama mmoja wa mjini mzuri sana wakawa wapenzi.

Mzee Ulaya katka mahusiano yake na Bint mrembo hakuwa akitumia barakoa.alitembea hivi hivi.si haba...akampa mimba bint.

Bahati nzuri siku hiyo Mzee yupo Tunduma na Mtoto pia. Mzee Ulaya akamwambia mwanawe aka Mzimu kuwa akamsalimie mama yake mdogo na kumwona mdogo wake maana hakuwa anamfahamu mke mdogo wa babaye.

Yule bint akasema amejifungua ila temporary anakaa kwa mamaye. Basi mzee ulaya akaelekezwa akawa ameongozana na mwanaye wanaenda kumsalimia Mzazi.

Kufika Mzimu anakuta pale ndo nyumbani kwa Mpenzi wake Jimama...na yule ambaye amejifungua mke mdogo wa baba yake ni mtoto wa Mpenzi wake Jimama. Baba mtu kuambiwa kuwa mama wa yule mke mdogo wake ni mpenzi wa mwanawe akapatwa na hasira na kuanza kumfokea mwanawe.

"Wewe kwa nini unatembea na mijimama hii mtoto mdogo!" Na ndipo Mzimu akajibu kuwa alipoenda alikuta tayari mtoto wa yule mama amechukuliwa so akaona yeye abaki na mama mtu.so naye mzee why anatembea na vibinti vidogo?

Swali likawa je yule mtoto ataitwa nani na kijana?na mzee atamwita nani mama yake binti?na kijana atamwita nani bint ya jimama?

Hapo ndo tukakumbuka hii familia siyo kabisa. Mwaka flani mzee Ulaya alikuwa anaishi na Mke wake wa kwanza Bi Sakina. Bi Sakina akawa amemleta mdogo wake ambaye ni mama yake mdogo Mzimu. Kumbe Mzimu akawa anamtongoza mama yake mdogo.Mama yake akagundua kuwa usiku Mzimu huchomoka na kwenda kumla mama yake mdogo.

Siku hiyo akaweka mtego.alipoona umekaribia usiku kuna sauti ya mlango kufunguliwa akachungulia na kumwona Mzimu ameingia chumbani kwa mama yake mdogo.mama yule kwa kughafilika akapiga kelele sana.

Mzee Ulaya akashtuka na kutoka kasi ameshika panga.kwenda Uliza nini tatizo...maana alidhani kuna mwizi.ndo mkewe anasema nimemwona Mzimu anaingia kwa mama yake mdogo chumbani.

Mzee akasema."aaargh mi nlidhani kuna mwizi kumbe kijana anaenda kuosha mpini" akarudi zake kwenda kulala.


Hii ndo familia ya Mzee Ulaya na mwanawe aka Mzimu. Inatatiza sana jamii ya karibu.
 
Aisee.. Watu wengi now days wanaishi kama huyo Mzee ulaya na mwanae mzimu
 
Back
Top Bottom