Falsafa ya ufisadi ngumu kueleweka na wana CCM, watawala

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,224
3,290
Hii falsafa imebainika kuwa ngumu sana kueleweka na watawala wa CCM na wanachama wake.

Ufisadi umebahatika kupambwa na kutukuzwa kwa majina mbali mbali, mwanzo uliitwa takrima, bahashishi na hata kuitwa zawadi. Watawala hawa wa CCM walibadilisha kila jina ili kujenga uhalali na ulitetewa sana.

Mwalimu Nyerere alijitahidi kuweka misingi na kupambana na kila aina ya ufisadi ikiwemo rushwa. Azimio la Arusha liliweka msingi huo.

Waliotengeneza Azimio hili ni wana CCM na waliolivunja ni wana CCM. Mageuzi haya yanasemwa ndio yaliasisi mifumo na kuacha mianya ya kifisadi na ilikuja kubainika baadae.

Mageuzi ya mfumo wetu wa uchumi mwishoni mwa miaka 1980 na mwanzoni mwa 1990 ilitoa mianya. Awamu zilizofuatia za CCM zilitumia mianya hiyo ya mageuzi kwa kutunga sera na kanuni zilizoruhusu ufisadi. CCM haiwezi kuepuka kubeba lawama hizi kwani wao ndio waliopitisha kanuni hizo hata kama wapinzani walipinga.Walitumia wingi wao kuruhusu kanuni na sera za kifisadi.

Kuanzia mikataba ya madini na hata ujenzi. Nchi ilikithiri kwa ufisadi .

DHANA YA UFISADI MTAKATIFU NA UFISADI DHAMBI.
Sasa CCM na watawala wanatuaminisha katika dhana hii ya ufisadi. Kwa watawala wa CCM ufisadi dhambi ni kule kuwa MPINZANI na kuwa na tuhuma za kifisadi na Ufisadi mtakatifu ni kuwa mwana CCM na kutuhumiwa kuwa na ufisadi. Imebainika kwamba kumbe CCM inawajuwa mafisadi kiukweli lakini haiwezi kuwachukulia hatua kwa kuwa ni wana CCM. Imebainika mara watu hawa wanapohama CCM huandamwa na kufichuliwa huo unaoitwa ufisadi. CCM ni moja na ni ile ile. Wimbo huu wa ufisaddi unaanza kuimbwa na wanachama wa kawaida hadi wakubwa wao. Utashangaa kweli . Yaani CCM fisadi mtakatifu anabadilika kuwa CCM fisadi dhambi mara tu atangazapo nia ya kuwa MPINZANI.

MAHAKAMA YA UFISADI v/s WATUHUMIWA.

Mahakama hii ilipigiwa chapuo na utawala wa CCM wa awamu ya tano, walituiaminisha kuwa kuna mafisadi papa na kwamba wangechukuliwa hatua kwa haraka. Tulishangaa kusikia hakuna mtu aliyepelekwa mahakamani kwa ufisadi licha ya kutumika nguvu nyingi kuandaa hili. Yaani utawala wa CCM ulitanzika kumjuwa fisadi ni nani baada ya kuunda mahakama ?. Kule kuchafuwa kote wapinzani waliokuwa CCM kuwa mafisadi ilishindikana nini kuwashtaki kwa ufisadi na wakati huku majukwaani mnatuaminisha watu hao kuwa mafisadi kwa nini ?

MATUKIO YA KIFISADI NA UTAWALA WA CCM.

Kuna matukio mengi ya kifisadi yametokea na wahusika wakuu wakiwa wana CCM na watawala, kuanzia matukio ya mikataba ya kiwira na umiliki wake, sakata la umeme wa IPTL, Richmond, Escrow n.k. Masakata haya yaliwahusisha wana CCM na watawala hawakuchukuliwa hatua za maana zaidi ya kulindana na kufanyiana visasi tu. Tumeshangaa hadi leo wahusika kuwa wapo mitaani na hawaulizwi. Tulishangaa hata wale wezi wa Escrow kuambiwa warejeshe fedha na kuachwa kuchukuliwa hatua za kisheria. Kuna miradi mingapi imekufa na iliwanufaisha wakubwa wa CCM? kuna mikataba mingapi inainyonya nchi hadi leo na bado ina maslahi ya watawala na wakubwa wa CCM?

MSHANGAO
Katika maelezo yote hayo hapo juu na ukweli ulio wazi wa ufisadi uliopo bado utawala umeshindwa kuwachukulia hatua wahusika. Tatizo ni kuwa ufisadi ni mfumo kama ulivyo kwa CCM kuwa ni mfumo, hujui uanzie wapi maana CCM na watawala wote ni wale wale. Mshangao unakuja kwa hawa wanaohama CCM eti ndio huitwa mafisadi na majizi ?
Kwa nini usishangae basi ikiwa ni hivyo vipi CCM itaacha kuwa kiwanda cha kuzalisha mafisadi?

Lazima ushangae kwa nini mtu akiwa CCM siyo fisadi lakini akihamia upinzani anakuwa fisadi by nature? kumbe CCM inalea mafisadi na kuwalinda ? kwa nini usishangae?


MWISHO.

Kwa kumalizia, changamoto kubwa kwa wana CCM na watawala ni kushindwa kujuwa upi ni ufisadi na yupi ni fisadi. Dhana hii inawaumbuwa na kuonekana kucheza na akili za watanzania kumbe hakuna nia ya dhati ya kuwashughulika mafisadi zaidi ya VISASI tu. Mfumo wa utambuzi inabidi uwe wazi na kusiwe na upendeleo.

Bidii ifanywe kwa nia ya dhati ili kuushughulikia ufisadi, mazingira ya sasa CCM haiwezi kushughulika na ufisadi kwani ni sawa na kujishughulikia wenyewe kwa wenyewe. Ndio maana hatukushangga mahakama kukosa mafisadi lakini hao mafisadi wapo wamejichimbi ndani ya ccm.

CCM BILA MAFISADI INAWEZEKANA KWA KUZALIWA UPYA LAKINI SI KWA HUU MVINYO WA LEO WA KUPAKWA MAFUTA CHUPA ILE ILE TUKIAMINI NI TOLEO JIPYA



Kishada.

 
Tatizo ule wimbo wa wacha wavimbe... acha waisome no... hapo akili zao zinahamia...
 
Kuna mkanganyiko mwingi kuhusu ufisadi ndani ya serikali na CCM
 
Bila shaka CCM kikiwa chama Tawala kinahusika na status ya ufisadi uliopo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom