Falsafa ya CHADEMA ni hii, ya CCM iko wapi?



Ritz, nadhani umechanganya mambo, kuna tofauti kubwa sana kati ya falsafa (phyilosophy), key message, strategy, opeations, theme and objective.

Kwenye red: Ulitakiwa useme, nchi nzima (ambayo by the way inaongozwa na serikali ya ccm) inakabiliwa na changamoto nyingi sana.
 
Kwa kifupi falsafa ya CDM ni the opposite of CCM in every sense. CDM iko kufanya kazi kwa kuyaondoa maovu yote yaliyofanywa na CCM kwa watanzania kwa zaidi ya miaka hamsini.
 

Falsafa ya Chadema ni nini na sera ya Chadema ni nini na kauli mbiu ya Chadema ni nini?
 
Naona unataka kujivunjia heshima yako humu Jamvini tofautisha sera na falsafa...Chadema sera zao ni za kibepari na ndio maana mfadhili wake mkuu wa nje ni chama cha Conservative cha Uingereza ambacho ni cha mapepari.

Mkuu nadhani umeelezwa vizuri kuwa operation sangara, vua gamba vaa gwanda na m4c ni operation tu na haiwezi kuwa falsafa. Falsafa ni dhana pana inayotafsiri maisha ya mtu
 
Sipingi wala siungi mkono mada,ila hoja alizotoa mleta mada ni nzito!
Matusi hayatabadili hoja hizi,ila CDM waje na hoja zingine nzito kukanusha madai ya mleta mada.
 

Ukiona mgonjwa anaomba uji ujue iziraeli anamnyemelea!
 

Zimebaki kuwa porojo wewe na wenzako mkiongozwa na Nape mlipewa nafasi ya kuwataja hao mnaosema wanawafadhili CDM mmebaki kuleta majungu yasiyo na udhibitisho.Hamuwezi kurudisha heshima ya chama chenu kwa hila wala uongo
 

inawezekana unawakumbusha jambo, lakini umeshuindwa namna ya kuliwasilisha.

Kuna tofauti kubwa kati ya FALSAFA na KAULI MBIU.

Operation sangara, Vua gamba vaa gwanda, na M4C, hazina sifa ya kuwa FALSAFA, bali zinakila sifa za kuitwa KAULI MBIU.

Ukitaka kuijua falsafa ya CHADEMA, Huna budi kupata kadi yao na katiba yao, lazima imezengumzwa.

kukupa kwa kifupi ni kwamba,

FALSAFA, ni msimamo wa mtu/kundi/taasisi/ ....juu ya jambo/mambo fulani. Sasa imani ya CHADEMA katika masuala mbalimbali ni kama ifuatavyo:-

1. Mgawanyo wa madaraka. Mihimili mitatu ijitegee, kila mhimili usimamie mihimili mingine ili kuleta uwajibikaji. Kwa maana hiyo, CHADEMA hawakubaliani na na mtu kuwa mubunge na hapo hapo kuwa waziri. waziri ni mtendaji wa wizara, hivyo anapaswa kuajiriwa kulingana na sifa zake, na wala si mwanasiasa wakati mbunge ni mwakilishi wa wananchi, anatumwa na wananchi kuisimamia serikali.

2. Serikali ya majimbo ni falsafa nyingine inayoaminika ndani ya CHADEMA. Hivyo, watakapo shika madaraka, kila mkoa utageuka na kuwa jimbo, ili viongozi wa mikoa wapatikane kwa kura za wananchi. Mkuu wa mkoa/jimbo/state, atachaguliwa, Mkurugenzi wa halimashauri, ataajiriwa na sio kuteuliwa. hii itasaidia viongozi wilayani na mkoani kuwajibika moja kwa moja kwa wananchi.

3.
 
ukikubali kutumiwa na kuweka utu wako rehani, huo ni utumwa wa fikra, na ndio tatizo kubwa la vijana wa lumumba ofisi ndogo.
 

KWA UFAFANUZI HUU, HATA Nape ATAKUWA AMEELEWA.
 
Jiandae kuhesabiwa na source itakuwa ofisi kuu ya takwimu usijifiche tafadhali.

 
Jaribu kuhoji baadhi ya masuala nyeti baada ya kufanya utafiti ili uje na vielelezo vyenye mashiko. ongea kwa takwimu na vidhibitisho ili jamii ipate kuelewa , ukisema prof mmoja na ukitaja chama cha conservative cha uk bila kuelezea kiasi cha fedha kinachotoa na katika account gani, unaonekena kama mpika majungu na mwenye wivu tu. haipendezi kwa mtu wa umri wako kuwa na papara ya mambo yasiyo na uhalisia kama haya! anyway pole kwa roho mbaya kwa cdm!
 
Ritz ni vema ungesoma maana ya Falsafa, Sera, Itikadi na Kauli mbiu kabla ya kupost hii thread. Hii thread is in your disadvantage.

TUMBIRI (PhD - In Progress at HULL, CPA(T), MBA(UDSM),Bcom(UDSM), PCM(Mzumbe High School - 2[SUP]nd[/SUP] Overall Best Student inForm six National Exams).

tumbiri@jamiiforums.com
 
Sijawahi kuona Jf wa ajabu kama huyu, sijawahi kupata point katika uzi zake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…