Falling from heights and get hurt

Falling from heights and get hurt

Izato

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2019
Posts
5,481
Reaction score
11,746
Hiki kinachoanza kuonekana kuwa vita ya wazi dhidi ya Mch. Gwajima naweza kusema kageukwa kimsimamo na wale wote waliokuwa hawana imani na chanjo za UVIKO 19 katika kipindi cha utawala wa JPM. Licha ya vita vya maneno ambavyo sasa vinaelekea katika uelekeo mpya, wote waziri wa afya na naibu wake walikuwa wakijipendekeza sana kwa JPM huku wakiwa mabingwa wa kuhimiza watu kupiga nyungu, kutumia tiba mbadala na kunywa vinywaji vingi vya kiasili na hata kuogopa kuvaa barakoa hadharani.

Sijui ni nini kimewakuta na hata sasa kuja na kiki mpya. Ileile timu kusifu na kuabudu imegeuza nyimbo za sifa na kuabudu kisa eti leo kuhani mpya kasimama madhabahuni.

Kundi lote limeshasau yote yale kuhani aliyetangulia aliyoyaami, wamemgeuka japokuwa wote ni wapo ndani ya dini ileile yenye imani moja. Yes! Almost all of them, not one not two but many of them.

Sasa ni zamu ya Mch. Gwajima pengine atafuata "young man Mr. Slowly slowly naye atafuata kwa kuwa wanaonyesha kutopendezwa na jinsi ya nyimbo za hiyari zinavyochezwa. Msisitizo si tena barakoa, kuzingatia umbali, kutumia vitakasa mikono ama kupuga nyungu, wimbo ni mmoja nao ni lazima wote tukachanjwe, tusichanganye mambo kwa kuwa miluzi mingi humpoteza mbwa.

Ni lazima tutii hiyari ya "priestess" juu ya chanjo ili akapate kuinuliwa zadi ya "the former priest" ambaye zile zake alipotosha imani licha kuwa ndiye mwendesha ibada aliyekalia kiti cha enzi.

Lazima tujifunze kustahimiliana kihoja juu ya uhiyari wa kupata chanjo. Tulianza kutumia vitisho na vyombo vya dola ili kukabiliana na hoja kinzani za wapinzani wa chama tawala. Sasa bila hata aibu yoyote ile tunaanza kutumia vitisho na matumizi ya vyombo vya dola katika uhiyari wa matumizi ya chanjo za UVIKO 19!

Mch. Gwajima bado tupo baadhi watu bado tusubiri majibu ya hoja ulizozitoa kuhusu uhiyari wako wa kutokuchanjwa. You get hurt by falling from heights.
 
Hiki kinachoanza kuonekana kuwa vita ya wazi dhidi ya Mch. Gwajima naweza kusema kageukwa kimsimamo na wale wote waliokuwa hawana imani na chanjo za UVIKO 19 katika kipindi cha utawala wa JPM....
Ndugu Mbege, baada ya Gwajiboy wahamie kwako kwani kwa upotoshaji hasa juu ya covid unashika namba mbili.
 
Ndugu Mbege,baada ya Gwajiboy wahamie kwako kwani kwa upotoshaji hasa juu ya covid unashika namba mbili.
Hapana mkuu Vessel, suala ni kukubali kuwa uwepo wa hoja kinzani upo kwa baadhi ya wananchi, ambapo kuna umuhimu wa kuzijibu hoja zao. Matumizi ya vitisho na dola kuziba watu hao midomo si jambo la busara hata kidogo
 
Hapana mkuu Vessel, suala ni kukubali kuwa uwepo wa hoja kinzani upo kwa baadhi ya wananchi, ambapo kuna umuhimu wa kuzijibu hoja zao. Matumizi ya vitisho na dola kuziba watu hao midomo si jambo la busara hata kidogo
Suala la matumizi ya dola,kuwafumba mdomo na lupango imekuwa no jambo la kawaida kwa wenye hoja kinzani za kisiasa zaidi chadema,ila hapa kwenye upotoshaji wa covid binafsi natofautiana na wenye hoja kama za Gwajiboy.
 
Suala la matumizi ya dola,kuwafumba mdomo na lupango imekuwa no jambo la kawaida kwa wenye hoja kinzani za kisiasa zaidi chadema,ila hapa kwenye upotoshaji wa covid binafsi natofautiana na wenye hoja kama za Gwajiboy.
Mkuu Vessel, ni walewale tu, walianza na wapinzani sasa mkono wa chuma utatumika kila sehemu. We subiri tu utaona matokeo yake.
 
Back
Top Bottom