Faiza Ally afunguka kuwa anampenda sana Sugu kutoka moyoni na hajali kuchekwa kwa kigeugeu chake

brigedia mafia

JF-Expert Member
Jul 21, 2016
2,264
2,275
Faiza Ally au ukipenda muite mama Sasha amefunguka kuwa ana mpenda sana Sugu japo hapo awali alivunga kwa kusema hana time nae kwa kuwa kila mtu ana hamsini zake

Lakini wahenga wanasema mapenzi ni kikohozi hayawezi kufichika, Faiza hatimaye kupitia instagram amefunguka kuwa ana mpenda sana Sugu kuliko mwanaume yeyote yule hapa Tanzania na duniani ki ujumla

Faiza anadai kuwa ingawa kwa sasa ana mpenzi na Sugu pia ana mpenzi lakini hilo haliwezi kumzuia kusema hisia zake kwa kuwa hawezi kuudanganya moyo

Faiza akaendelea kusema kuwa yeye ana imani ya kuwa ,kwa kuwa Mungu ndiye aliye mleta Sugu kwake na akamuondosha hivyo basi ana imani ya kuwa ipo siku Mungu atamrudisha tena Sugu mikononi mwake au kumletea mwingine mwenye sifa kama za Sugu

Faiza pia akasema hajali hata kama watu watamcheka kwa uamuzi huo wa kujichoresha lakini ndio hivyo moyo ushampenda na hata mama yake na pia mtoto wake Sasha wanajua pia
1473933986808.jpg

1473933998850.jpg

1473934008763.jpg

1473934023408.jpg

1473934033470.jpg
 
Back
Top Bottom