Faiza Ally amuomba msamaha Sugu, adai Sugu "anachezewa" ili amsahau mwanae

Zurie

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
1,745
4,275
Mwanadada Faiza Ally akiwa kwenye interview na Zamaradi TV ameelezea maisha yake na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi kuanzia kukutana kwao, kuachana na hadi ugomvi wao wa kuhusu matunzo ya mtoto.

Kukutana kwao

Faiza anamlaumu Sugu kwa 'kumharibia' ladha ya wanaume wa Kitanzania kwani alishazoea kuwa kwenye mahusiano na Wazungu kwani alikuwa akitembelea hoteli za kitalii.

Faiza anasema Sugu alimkuta akiwa na maisha yake yaani pesa, magari na kila kitu hivyo anampenda bila sababu yoyote.

Kuachana

Faiza ingawa hajaeleza moja kwa moja sababu ya kuachana na Sugu, amegusia kuwa imechangiwa na mama mkwe yaani Marehemu mama wa Joseph. Amedai mama huyo hakuwahi kumpenda ingawa alimtendea wema sana.

Anadai baada ya kuachana na Sugu, wifi yake alimueleza kuwa mama aliwahi kuapa kuwa Faiza hawezi kufanikiwa kuishi na Sugu na hatopata chochote kwa mwanaye huyo.

Amesema anahisi mama Sugu hakumpenda kwa sababu ya usasa na uzungu mwingi aliokuwa nao kwani alikuwa anaenda naye beach na kuvaa bikini mbele yake bila kujali kuwa yule ni mama wa kitanzania.

Ugomvi kuhusu matunzo ya mtoto

Faiza ni muigizaji wa filamu lakini amejulikana sana kutokana na bifu lake na Mbunge Sugu ambapo mara nyingi amekuwa akilalamika kutosaidiwa kumlea binti yao Sasha Desderia.

Faiza anaeleza kuwa Sugu hamtunzi mtoto wake na ameanza kumlipia ada ya shule hivi karibuni tena kwa masharti kadha wa kadha ikiwemo kumwambia "Happy(mke wa Sugu) anamtafutia Sasha shule"

Anaendelea kudadavua kuwa amewahi kwenda kwa waganga ama "maustadhi" kuombewa dua na mara zote akishafanyiwa visomo baba Sasha hujirudi na kumtafuta mwanae japo kwa muda mfupi hivyo anaamini kuna nguvu za giza zinatumika kumpumbaza asimkumbuke mwanaye.

Ugomvi na Mke wa Sugu aitwaye Happy

Faiza amemuita Happy shetani akidai hana mapenzi na mwanae na kuwa ana sura nyingi na anaigiza maisha ili aonekane mama bora.

Faiza anasema mwanaye Sasha alipokwenda Mbeya kipindi Sugu yuko gerezani, alizuiwa kwenda kwenye hoteli ya baba yake kwa sababu zisizo na mashiko.

Pia anadai kuwa Happy kama mwanamke hakuwa na busara kukubali Sugu ampeleke yeye mahakamani kudai custody ya mtoto wa miaka miwili ili apelekewe yeye kumlea.

Vile vile ameeleza kuwa akaunti feki za instagram zinazomtukana yeye ni za Happy kwani Happy sio staa wa kuwa na fanpage zinazotukana maadui zake.

Faiza amefunguka vitu vingi ikiwemo mapenzi yake kwa Sugu. Zaidi, angalia interview yake




Pia soma


 
Huyu anafanya jitihada kubwa kuharibu future ya Mwanawe kwa kumtumia kutafuta Kick
 
Back
Top Bottom