Kuna vyuo hapa nchini ambavyo vimekuwa na utaratibu wa kutoza faini mwanfunzi anapochelewa kulipa ada mfano mwezi mmoja au miwili baada ya chuo kufunguliwa bila kujali mwanafunzi husika ana mkopo ama anajilipia mwenyewe kwa kudunduliza visenti kidogo kidogo.Kwa mfano faini za chuo kikuu SAUT-Mwanza ni sh.100,000 hata kama mtu alikuwa anadaiwa 5,000 inabidi alipe faini hiyo.Kwa hili mimi naona halifai kabisa.