OMBI: Naiomba Serikali ipunguze ADA ya Vyuo Vikuu Ifanane na ile ya High school( Advanced level)

sansaba

Senior Member
Mar 8, 2018
103
268
Habarini Wanajamvi,
Moja kwa moja acha niende kwenye jambo husika, Kutokana na ubovu wa Elimu ya Vyuo Vikuu naiomba serikali ishushe ADA mpaka Tsh. 70, 000/= kwa mwaka sawa na ADA ya form FIVE na SIX kwa hapa nchini. Kwanini nayasema haya?

Nayasema kwa sababu Vijana wengi wanamaliza hawana ujuzi wowote kichwani tofauti na madesa yaani ukimchukua form six aliyemaliza na graduated student mmoja viwango vya elimu ni sawa tofauti ni mitaala ndio tofauti ila ujuzi kichwani ni zero.

Leo nitakiangazia chuo chetu mama na pendwa hapa nchini, The University of Dar es salaam wao wanapenda kuita UDSM. na nitajikita kuongelea College moja pendwa sana na ndio kitovu cha Maendeleo hapa nchini College of Engineering and Technology( CoET).

CoET; hii ndaki ina idara nyingi sana na muhimu sana mfano idara ya umeme, mekanikia na viwanda n.k, Tukija kwenye suala la ADA wanalipa wastani wa1.3M kwa mwaka, yaani hii pesa ni kubwa sana kulingana na elimu wanayoipata pale ni vitu viwili tofauti sana, Shida ya pale wanajikita kufundisha nadharia sana na si vitendo lakini wakija huku mtaani wakihitaji kazi. Kazi nyingi ni za vitendo kwa hio wanaboronga kazi na kukimbia kwa kusingizia wamepata kazi sehemu yingine ama wamepata vyuo vya kusoma tena.

Nimekaa nikagundua makosa yapo hapo kwenye uongozi wa chuo husika. Mitaala bado mibovu haiwapatii vijana elimu ya kutosha ili wawe na uwezo hata wa kujiajili, kwamba vijana wakimaliza pale wanatakiwa tena wakae tena mtaani kwa kufanya kazi kwa zaidi ya miaka minne ndio wawe wahandisi. Ukiangalia toka kijana aanze kusoma hadi kuja kuwa mhandishi inachukua miaka 21 toka darasa la kwanza ukijumlisha miaka 7 au 8 ya kuanza elimu ya msingi unapata miaka 28, hapo kijana ndio angalau anapata elimu kwa hapa nchini hapo no kupoteza muda. Pale CoET na chuo kwa ujumla kuna maprofesa ila wapo kimya wanaona elimu waitoayo ipo sawa. Kama wameshindwa kusimamia Elimu watoeni wakalime, kazi kuomba rushwa ya ngono tu kwa mabinti zetu. Shenzi type

Nikianza na chuo husika naomba msikie haya
.. Badilisheni mitaala ya Elimu hiyo sio misaafu ama katiba ya JMT.
.. Wapeni vijana muda mwingi wa kufanya vitendo achaneni na kuiga elimu ya mbele, tafutenu standard na structure ya Elimu yenu.
.. Simamieni na toeni ushauri kwa vijana maana nyie ni kama walezi pia.

Kama hapo juu hayatatekelezwa basi serikali punguzeni hizo gharama za masomo maana wazazi mnawatesa bure na kuwaongezea vijana madeni kutoka HESLB kwa wale wanufaika wa mikopo. Pia serikali kagueni hizi taasisi zinatoa elimu ya ovyo sana warekebisheni wafanye yaliyo mema,

Mwisho
Sioni haja ya kujenga viwanda nchini huku wanao simamia ni ngozi nyeupe, tutakuwa watumwa hadi lini?. basi kama vijana wetu hawana uwezo futeni hizo shule wakae ndani wakalime na wachunge mbuzi kwa babu zao.

N:B UDSM ni mada case lakini haya yote yanatokea kwa vyuo vyetu vyote nchini .

Karibuni wadau kwa mitazamo mbalimbali.

Asante.
 
Una hoja ya msingi. Hata mimi nimegundua elimu ya chuo kikuu ina udhaifu mwingi sana kwenye baadhi ya kozi. Hivyo kuna umuhimu pia Serikali kuajiri Wahadhili wanaojua kufundisha na siyo tu kuangalia kigezo cha GPA kubwa.

Ukija kwenye hiyo nadharia zaidi kuliko vitendo, ni kweli! Na hapo napo waboreshe ili wataalamu wetu wawe na tija kama tunavyo ona kwenye baadhi ya vyuo kama MUST na DIT ambako wanachuo wao huthubutu nyakati fulani fulani kugundua/kutengeneza hata baadhi ya mashine.

Ila kwa hiyo CoET, aisee sijawahi kusikia wakigundua chochote! Labda wahitimu au walimu wao waje hapa kutuelimisha zaidi.

Kuhusu ada kuwa elfu 70! Hapana siungi mkono hoja. Tutakuwa tumeishusha thamani Elimu yetu ya chuo kikuu kwa kiwango cha juu sana. Kumbuka pia kuna wanafunzi wanaotoka nje ya mipaka yetu. Sasa na wenyewe watalipa ada ya dola ngapi kwa mwaka! Na huoni tutaibebesha serikali mzigo mzito sana wa kufidia ma gap yatakayo jitokeza?
 
Elimu itakuwa ya kuunga unga bajeti za serikali zilivyo za shida nyingi ,Uwekaji wa ada ulizingatia mambo mengi
 
Sawa sawa mkuu, kumbe tuendelee kuumia kwa ulipaji wa Ada kubwa wakati elimu haina kiwango chochote?
Ifikie mahali tukubali kuanza upya baadhi ya mifumo tuache janja janja, now days pale UDSM wageni kutoka nje wamekuwa wachache sana tena hasa watu wa uganda,.. Tukubali tumefeli na t uanze upya
.
Nimechoka kuwaona wachina pale ubungo wanajenga Wakati huo tuna wataalamu kama kina mfugale ni aibu sana kwa Taifa.
Una hoja ya msingi. Hata mimi nimegundua elimu ya chuo kikuu ina udhaifu mwingi sana kwenye baadhi ya kozi. Hivyo kuna umuhimu pia Serikali kuajiri Wahadhili wanaojua kufundisha na siyo tu kuangalia kigezo cha GPA kubwa.

Ukija kwenye hiyo nadharia zaidi kuliko vitendo, ni kweli! Na hapo napo waboreshe ili wataalamu wetu wawe na tija kama tunavyo ona kwenye baadhi ya vyuo kama MUST na DIT ambako wanachuo wao huthubutu nyakati fulani fulani kugundua/kutengeneza hata baadhi ya mashine.

Ila kwa hiyo CoET, aisee sijawahi kusikia wakigundua chochote! Labda wahitimu au walimu wao waje hapa kutuelimisha zaidi.

Kuhusu ada kuwa elfu 70! Hapana siungi mkono hoja. Tutakuwa tumeishusha thamani Elimu yetu ya chuo kikuu kwa kiwango cha juu sana. Kumbuka pia kuna wanafunzi wanaotoka nje ya mipaka yetu. Sasa na wenyewe watalipa ada ya dola ngapi kwa mwaka! Na huoni tutaibebesha serikali mzigo mzito sana wa kufidia ma gap yatakayo jitokeza?
 
Mkuu hao malecturers wanakula pesa za bure
Imagine Mtu anakipindi kimoja per week tena masaa 2, na akiingia unaona hafanyi chochote

Lakini hawa hawa wanalipwa 1M na kuendelea hadi 3M huko,
Mbaya zaidi wanawaamini vijana walio maliza hapo wabaki kufundisha nasikia hao ndio hakuna kitu

Kiufupi Taasisi za Elimu nchini hakuna kitu
Elimu itakuwa ya kuunga unga bajeti za serikali zilivyo za shida nyingi ,Uwekaji wa ada ulizingatia mambo mengi
 
Unalinganisha na wapi? Tuanzie hapo? Then pambanua hiyo ada imekuwaje iwe ya hicho kiwango? Kusema ni rahisi kutekeleza sio lelemama. Hebu tupe mrejesho kwa nini unasema hicho kiwango ni kikubwa na umetumia vigezo gani na kama una ushahidi model ipi ipo wapi na imefanikiwa vipi?

BTW hao Maprof wanaoomba ngono sidhani kama ndio agenda iliyopo kwenye kuajiriwa? Hizo ni tabia sasa kama tunaongelea tabia tusichanganye na yale ambayo tumeyapanga na tunayatarajia.
 
Hence

Under curtis peribus; Secondary School = University Education
 
Back
Top Bottom