YEHODAYA
JF-Expert Member
- Aug 9, 2015
- 36,902
- 52,003
Jana kwenye kipindi cha TBC saa tatu usiku kwenye kipindi cha siku 100 za MAGUFULI kinachorushwa mfululizo kila siku waziri Lukuvi alikutana na Kituko cha mwaka pale alipofanya ziara ya kustukiza masjala na alipokuta faili la hati ya mtu limekaa miaka mitatu kwenye ofisi ya Ardhi kwamba haliwezi toka ofisi moja kwenda ofisi ya Ardhi makao makuu liandikiwe hati kwa sababu shilingi elfu ishirini hazijaletwa na wizara ya ardhi kwenye hiyo ofisi ya Ardhi iliyokalia hilo faili la mteja ambaye kutwa kucha anapiga kiguu na njia kuuliza hati yake imefikia wapi kwa miaka mitatu.
Waziri alipowabana kuwa mlimwambia mwenyewe kuwa tatizo ni hiyo Elfu ishirini? Wakasema hapana.Waziri alionyesha kukerwa mno.
Yaani Ardhi kuna baadhi ya watendaji wa ajabu sio wabunifu wa kutatua kero za wananchi kama kero ndogo kama hiyo.Looo! Faili lilionekana limechoka limejaa vumbi hadi basi.Ni kama waliliweka kwenye kaburi la masjala.
Kuna mwingine ambaye faili lake la kero limekaa muda mrefu hebu atupe uzoefu wake na elezea ni wapi huko sio lazima iwe ardhi tu.