Faida za upinzani versus ushabiki wa kisiasa

WATANABE

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2011
Messages
1,091
Points
1,195

WATANABE

JF-Expert Member
Joined Apr 13, 2011
1,091 1,195
Tarehe 6 Novemba 2012 kupitia https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/349724-mnyika-watchout-maji-ubungo-yatakuondoa.html nilimshukia Waziri Kabaka kwa kushindwa kuwasilisha bungeni mikataba mbali mbali ya kimataifa inayohusu ajira ili kuridhiwa na bunge na aweze kuwa ujasiri wa kuhoji kuhusu maj katika jimbo la Mbunge mwingine, Niliandika hivi

"Hivi kati ya ukosefu wa Maji na ukosefu Ajira ni lipi tatizo kubwa hap nchini? Yapo majimbo ambayo hayana tatizo la maji lakini wakazi wake hususan vijana hawana ajira kabisa ilihali Waziri kakaa wizarani anashindwa hata kupeleka mikataba ya Ajira bungeni kwa ajili ya kuridhiwa. Hadi sasa Tanzania imeridhia mikataba 35 ya kimataifa inayohusu masuala ya ajira na haki za wafanyakazi http://www.ilo.org/dyn/normlex/en/f?...TRUMENT_SORT:3 na badi haijaridhia mikataba 57 inayohusu Ajiri na haki za wafanyakazi http://www.ilo.org/dyn/normlex/en/f?...TRUMENT_SORT:4"

Taarifa nilizopata ni kuwa baada ya Mkutano Mkuu wa CCM wa 8 Wizara Mama huyo anayoiongoza ya Kazi na Ajira imeshukiwa kisawasawa na hivi sasa mwisho wa mwaka wanakumbuka kuwasiliana na wadau mbali mbali wa maendeelo kuwabembeleza warudi kufanya kazi na wizara hiyo kutokana na hapo nyuma kushindwa kujibu barua, kuandika Proposal, na maandishi mbali mbali ya kutengewa fedha za utekelezaji wa miradi mbali mbali ya kuzalisha ajira.

Kwa hakika wa
dau wengi wa maendeleo waliaca kabisa kufanya kazi na wizara hii na ndio chanzo cha kasi ndogo ya uzalishaji wa ajira, Kaiz waliyokuwa wakiifahamu ni kufanya ukaguzi Asubuhi na mchana katika migahawa, jioni katika baa na gesti. BIG Up CCM kwa kuanza kufanya Mapinduzi ya ndani ya chama na Serikali. Keep up the tempo!!!

Ndio maana tuliisapoti CDM 2010 ili kuitoa CCM usingizini, Uchukuzi imeamka, Nishati imeamka, Fedha imamka, Ujenzi ilikuwa macho na inaendelea kuwa macho. Kazi na Ajira ndio sasa imeanza kutolewa katika usingizi mzito.

Sasa ni zamu yetu wadau wote CCM , CDM n.k tushirikianae kila mtu anavyojua ili kuiamsha Wizara ya Elimu ili anagalau Serikali itimize wajibu wa kumtumia kila mwanafunzi wa shule ya msingi 10,000/= iliyoahidiwa kwa mwaka. Kiasi kinchotakiwa ili kutimiza hilo ni Bilioni 100 tu. Kinana, Mangula, Kikwete wake up pelekeni hizo pesa ili watoto wa maskini wasome

Kibaya yule aliyemwamsha mwenzie (CDM) tunaona ndio anaanza kupata usingizi wa urais wa 2015 na wapenzi wake kujiamini kupita kiasi wakati ambapo CCM wamefanya timing miradi yote mikubwa kufunguliwa 2014/5 sijui watakuwa na lipi la kusema wakati huo tunapanda mabasi ya kwenda kasi, Treni n.k

Waache hao wanaoanza kuiga kupanga safu na makundi ya kugombea urais waendele kuota urais wa 2015
 

Forum statistics

Threads 1,389,124
Members 527,846
Posts 34,017,662
Top