kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,428
- 13,936
Wanafunzi huwa wanajichagulia wenyewe vyuo 3 kati ya vyuo vingi vilivyoko nchini kwa kutumia mtandao ya internet au simu unaoendeshwa na ama TCU au NACTE. Kati ya vyuo hivyo vitatu alivyovichagua yeye mwenyewe mwanafunzi atachaguliwa na jina lake litapelekwa kwenye chuo kimoja tu kati ya hivyo vitatu kutokana na ufaulu wa mwanafunzi kuhusu kozi aliyoiomba na kipaumbele alichotoa kwenye uchaguzi wa kozi na vyuo husika. Hivyo basi, mwanafunzi asipopelekwa chaguo lake la kwanza atapelekwa la pili au la tatu.
Faida za kutumia mtandao badala ya vyuo vyenyewe kufanya udali wa wanafunzi ni pamoja na:
1. Uchumi: Imempunguzia gharama mwanafunzi na mzazi ya kutoa/kulipa hela nyingi za kuchukulia form (application) za maombi ya chuo kutoka vyuo mbalimbali. Mwanafunzi hana uhakika kuwa kutuma maombi kwenye chuo kimoja kunatosha kupata nafasi. Sasa hivi anatoa sh. 30,000 tu kwa vyuo vyote atakavyovichagua/pendekeza.
2. Kumeepusha mwanafunzi mmoja kusajiliwa/dahiliwa zaidi ya chuo kimoja kwa wakati mmoja
3. Mwanafunzi hahitaji kusafiri kukifuata chuo kilipo ili kuomba kusajiliwa.
4. Mwanafunzi ni rahisi kuhama kutoka chuo kimoja kwenda kingine
5. Inamrahisishia mwanafunzi kufahamu chuo gani kuna nafasi na wapi kumejaa
6. Inamrahisishia mwanafunzi kufahamu taarifa na sifa mbalimbali za vyuo kwa urahisi.
Kama kila chuo kitaamua kufanya udahili wake chenyewe mwanafunzi atarudi kulekule kulikosababisha TCU na NACTE wabuni udahili wa pamoja kwa njia ya mtandao.