Faida za Parachichi katika mwili wa Binadamu

mzizi mkavu nisaidie, nikila avocado nashiba siku nzima, yaani haijalishi nimekula kiasi gani...... Inatokana na nini?
 
mzizi mkavu nisaidie, nikila avocado nashiba siku nzima, yaani haijalishi nimekula kiasi gani...... Inatokana na nini?
@BADILI TABIA mkuu kama alivyokujibu mkuu@Mafuluto kuwa ndani ya tunda la avucado kuna fiber nyingi ndio inayokufanya unakuwa husikii njaa ukilila hilo tunda la avucado hakuna madhara yoyote endelea kulila hilo tunda

Ndiyo fiber hiyo, ambayo inapatikana na wingi ktk tunda hili !!
mkuu@Mafuluto asante kwa msaada wako wa kuelimisha watu ubarikiwe
 
Thanks MziziMkavu
weekend hii nimetengeneza juice ambayo ilikuwa na vitu vifuatavyo:-
2 Nanasi
2 Avocado
2 Bananas
2 Cucumber
2 Carrots
Fungu la tembere na
20 passion fruits.

Nimepata si tu 5ltrs of juice, bali chakula. Nikinywa glass moja, inanitosha kabisa kulalia. Ofisini ndicho nitachoshindia today. Nina uhakika ninapta manutrients ya kutosha tu na weight naiangalia pia.

Thanks kwa tips nzuri za afya!
 
Kaunga,

Unakaa mitaa ipi umenitamanisha sanaa.


Thanks MziziMkavu
weekend hii nimetengeneza juice ambayo ilikuwa na vitu vifuatavyo:-
2 Nanasi
2 Avocado
2 Bananas
2 Cucumber
2 Carrots
Fungu la tembere na
20 passion fruits.

Nimepata si tu 5ltrs of juice, bali chakula. Nikinywa glass moja, inanitosha kabisa kulalia. Ofisini ndicho nitachoshindia today. Nina uhakika ninapta manutrients ya kutosha tu na weight naiangalia pia.

Thanks kwa tips nzuri za afya!
 
Thanks MziziMkavu
weekend hii nimetengeneza juice ambayo ilikuwa na vitu vifuatavyo:-
2 Nanasi
2 Avocado
2 Bananas
2 Cucumber
2 Carrots
Fungu la tembere na
20 passion fruits.

Nimepata si tu 5ltrs of juice, bali chakula. Nikinywa glass moja, inanitosha kabisa kulalia. Ofisini ndicho nitachoshindia today. Nina uhakika ninapta manutrients ya kutosha tu na weight naiangalia pia.

Thanks kwa tips nzuri za afya!

ooh mama Kaunga fungu la tembele tena oops will try this over the weekend ..
Niambie test madame kabla sijaharibu siku yangu
 
Last edited by a moderator:
Mziz mkavu,thanks....
nina tatizo la vidonda vya tumbo natumain tunda hili litanisaidia...
@Tumaah Aidha, tunda hili linasaidia uyeyushaji wa chakula tumboni hasa kwa wale wenye matatizo ya vidonda vya tumbo, kwani parachichi lina nyuzinyuzi "fiber" ambayo ni muhimu kukinga kuta za utumbo. Watu wenye maradhi ya anaemia, diabetes, matatizo ya mfumo wa neva, matatizo ya mishipa ya moyo hasa wa artery wanashauriwa kula tunda hili mara nyingi.
 
MziziMkavu nikitia sukari au asali katika juice ya parachichi kuna madhara yoyote?
@Kaparatus hakuna madhara yoyote yale ila haipendezi tu kuchanganya Asalina hilo tunda la Parachichi kunywa asali kisha kula hilo tunda kila kitu na faida zake.

Faida zake zimenifurahisha nitazidi kulitumia
Swali- mafuta yake je hatanenepeshi?
@manasa mafuta yake hayanenepeshi wala hayana madhara hebu soma hapa VIRUTUBISHO VYA PARACHICHI

Kwa ujumla, parachichi ni chanzo kizuri cha Vitamini K, Vitamini B6 na Vitamini C.
Aidha, tunda hili lina kiwango kizuri cha virutubisho aina ya Folate, kopa na ufumwele (Fiber). Fiber ni muhimu katika kuwezesha mtu kupata choo


laini na bila matatizo. Bila kusahau kwamba tunda hili ni chanzo kizuri pia cha madini ya Potasiamu: ina kiwango kikubwa kuliko hata ndizi.
Ingawa parachichi ni tunda, lakini lina kiwango kikubwa cha mafuta (fats) ambayo yanakadiriwa kuwa kati ya asilimia 71 – 88, kiwango ambacho ni cha juu kwa asilimia 20 ukilinganisha na matunda mengine. Kwa wastani, parachichi moja lina gramu 30 za mafuta, lakini kati ya hizo, gramu 20 ni za


mafuta mazuri kiafya (Monounsaturated fats na Aloic Acid) ambayo husaidia kujenga afya bora mwilini.
Utafiti zaidi kuhusu tunda hili unamalizia kwa kusema kwamba parachichi lina takribani aina 20 za Vitamin, madini na virutubisho muhimu


(Phytonutriens) ambavyo hutuo kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mengi hatari. Baadhi ya Vitamini zilizomo na asilimia zake kwenye mabano ni pamoja na Vitamin E (4%), Vitamin C (4%), Folate (6%), Fiber (4%), Iron (2%) na Potasium (4%).


Kwa ujumla tunda la Parachichi lina faida nyingi kiafya na tunatakiwa tuyale kwa wingi, hasa ukizingatia huu ndiyo msimu wake. ni jambo la kushangaza sana kuona kwamba watu wengine msimu wa maparachichi unaingia hadi unakwisha, mtu hajala hata moja.
 
avocado.jpg



FAIDA YA TUNDA LA PARACHICHI - PEA (AVOCADO)
Ndani ya tunda hili kuna maji kiasi kidogo sana ukilinganisha na matunda mengine lakini kuna mafuta mengi na unaweza kuchanganya kula na tunda lingine kama vile apple, ndizi, chungwa au hata maziwa kwa kutengeneza juisi.

TINDIKALI
Licha ya kuwa na mafuta parachichi lina tindikali (acid) mbalimbali ikiwemo inayojulikana kama amino ambayo husaidia sana kukinga na kutibu maradhi katika mwili wa binadamu. Tunda hili pia lina protini ya kiwango cha juu.
Pia kuna tindikali inayoitwa oleic acid kwenye parachichi ambayo husaidia kukinga magonjwa ya moyo, kiharusi na kansa.

VITAMINI “E” NA B6
Imeelezwa na wataalamu kuwa tunda hili lina kiwango kikubwa cha vitamini E kuliko ile inayopatikana kutoka kwenye mazao ya wanyama.Parachichi lina vitamini hiyo nyingi kuliko inayopatikana katika mayai ambayo yanasifika kwa kuwa na vitamini e, hivyo hii inathibitisha kuwa lina faida kubwa mwilini.

Licha ya vitamini E pia ndani ya parachichi kuna vitamini B6 na kuna madini ya chuma (Iron) kwa wingi na madini ya potassium, pamoja na vitamin B6 na E mlaji anaweza kuletawa nafuu sana kama alikuwa na matatizo ya stress, matatizo ya uzazi kama ugumba na jogoo kutopanda mtungi Nguvu za kiume pia tunda hili linasaidia (impotence) .

FAIDA ZA PARACHICHI
Licha ya binadamu kufaidika na virutubisho vya tunda hili kuna faida nyingi za parachichi kama vile majani ya mti wake pamoja na magamba, baadhi ya watu hutumia kutibu maradhi ya kuharisha.

Majani na magamba hayo hutibu pia tatizo la gesi tumboni, kutuliza kikohozi pamoja na matatizo ya ini na kusafisha njia ya mkojo.
Hata hivyo, kwa mujibu wa wataalamu wa dawa za mitishamba, dawa hii haifai kutumiwa na wanawake ambao wana mimba kwani wakitumia inaweza kusababisha kuharibika kwa ujauzito.


HEDHI
Hata hivyo, wataalamu wa tiba mbadala wanasema dawa hiyo inaweza kuwasaidia sana wanawake ambao wameshindwa kuona siku zao kwa wakati, na wakitumia vyema wanaweza kuanza kuona siku zao.

Aidha, tunda
hili linasaidia uyeyushaji wa chakula tumboni hasa kwa wale wenye matatizo ya vidonda vya tumbo, kwani parachichi lina nyuzinyuzi “fiber” ambayo ni muhimu kukinga kuta za utumbo. Watu wenye maradhi ya anaemia, diabetes, matatizo ya mfumo wa neva, matatizo ya mishipa ya moyo hasa wa artery wanashauriwa kula tunda hili mara nyingi.

Lakini pia tunda hili limethibitishwa na wataalamu kuwa linapunguza kwa kiwango kikubwa cholesterol kutoka kwenye damu hasa kwa watu wanene.

Tunda hili husaidia kulainisha ngozi na kuondoa mikunjo, hung`arisha na kulainisha nywele na kuzisaidia kukua pia kuziimarisha na kuzuia kukatikakatika.

Parachichi unaweza kulila kwa kulimenya au kwa kulisaga na kutengeneza juisi na kama nilivyoeleza hapo juu unaweza kuchanganya na matunda mengine kama tulivyoyataja na hutaharibu virutubisho vilivyomo badala yake utaongeza ubora wa juisi yako.

Watoto wadogo pia unaweza kuwapa tunda hili na wakafaidika na haya tuliyoyaandika.
Parachichi pia huweza kutumika kama siagi kwa kupaka kwenye mkate au kuchanganya na wali.​

Haya wale wanaopenda ngozi zao za mwilini zisijikunje hata wakiwa watu wazima wadumu kula tunda hili kila siku katika maisha yao basi ngozi za mwili wao hazitajikunja hata usoni watakuwa kila siku vijana hata wakiwa wazee.

Naomba ufafanuzi zaidi hapo kwenye Red.
 
Naomba ufafanuzi zaidi hapo kwenye Red.
@Mgalatia (Majani na magamba hayo hutibu pia tatizo la gesi tumboni, kutuliza kikohozi pamoja na matatizo ya ini na kusafisha njia ya mkojo) Ukichemsha hayo magamba na majani yake husaidia kuondowa Gesi iliyo tumboni kwako, na pia husaidia kuondosha hayo matatizo ya ini na kusafisha njia ya mkojo chemcha pamoja unywe.
 
Back
Top Bottom