Faida za mikinzano/migogoro katika mahusiano

Faida za mikinzano/migogoro katika mahusiano

Joined
Mar 5, 2014
Posts
93
Reaction score
49
Nilikuwa miongoni mwa wanaochukia sana kukorofishana na mtu ninayehusiana naye mfano mke wangu,ndugu zangu n.k ila nimefanya utafiti mdogo tu nikagundua kuna faida nyingi za mikinzano katika mahusiano.
Hakuna kazi ngumu kama kuyaanzisha mahusiano na kuyaendeleza kwa muda bila ya uwepo wa misuguano/mikizano au migogoro"maintaining dynamic and harmonious relationship".
Suala la msingi hapa siyo kuiogopa na kuikwepa sana mikinzano hiyo ila ni kujitahidi kuipunguza na kutokuiachia ikakua sana na kuzaa matatizo yasiyokwisha.
Kama mume au mke unapaswa kujifunza ktk mikinzano au migogoro inayotokea ktk mahusiano yako na mumeo/mkeo,unapaswa kuangali a mikinzano hiyo ilisababishwa na nini, kwa nini, wapi,n.k hii itakusaidia kumuelewa zaidi mwenzako.
Wakati mwingine ni vizuri kuiachia misuguano na mikinzano ikawepo ili kwani kupitia mikinzano/migogoro hiyo pendeleo za pande zote zinazohusiana hujisajili na hapa ndipo watu "HUFAHAMIANA ZAIDI KATIKA BAADHI YA MAMBO YAO"
Binadamu kwa asili tuna tabia ya kufichapendeleo zetu(kujihami)defensive mechanism tabia ambayo naweza nikaiita ni kiini cha"UNAFIKI"mara nyingi kupitia migogoro watu wengi hujikuta wanashindwa kushindana na dhamiri zao ha hivyo kusema mambo mengi yanayowakera kwa kumaanisha(kwa dhati).
Usiichukie sana mikinzano bali chukia sana kuiachilia ikakua zaidi na kuwa vita,chukia kuacha kujifunza kutokana na mikinzano ukutanayo nayo
 
Kutofautiana huimarisha mahusiano na kuongeza ukaribu + maelewano ila kama hamko imara ndio bye bye tena. Kama ni ndugu hamtoongea, kama ni wapenzi mtaachana, kama ni marafiki mtasusana n.k

Jambo la muhimu ni kutokuupa huko kutofautiana uzito zaidi ya inavyopaswa.
 
Hakuna kazi ngumu kama kuyaanzisha mahusiano na kuyaendeleza kwa muda bila ya uwepo wa misuguano/mikizano au migogoro"maintaining dynamic and harmonious relationship".
WISEMEN SAY..........
487003_493086567379733_131600924_n.jpg
 
kikubwa watu wawe optimistic. "wagombanao ndio wapatanao" iwe applicable.
 
aisee niliwahi kuwa na demu kila nikigombana nae au tukikinzana kidogo tu,,yeye alikuwa anakimbilia na kusema x wake hajawah kugombana nae wala kumgombeza nikamwambia basi alikuwa anakuogopa au mlikuwa mnaogopana.....:tape:
 
Back
Top Bottom