Je, wewe upo hatua ipi? Hatua za Ukuaji na maendeleo katika Saiko-jamii

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,878
JE, WEWE UPO KATIKA HATUA IPI? HATUA ZA UKUAJI NA MAENDELEO KATIKA SAIKO-JAMII?

Anaandika, Robert Heriel

NOTE: Andiko hili ni Kwa ajili ya watu wote!

Andiko hili lafaa Kwa watu wazima kujitambua na kujua namna ya kukabiliana na Mabadiliko ya ukuaji wetu WA kiakili, kimwili na kitabia Kwa manufaa bora Kwetu, Kwa familia, jamii na taifa zima, lakini pia lafaa Kwa malezi ya watoto Kwa ajili ya kuandaa kizazi bora chenye manufaa ndani ya taifa letu.
Kwani linahusu Akili na tabia(Saikolojia) ya Sisi binadamu katika ukuaji na maendeleo.

Leo nitagusia Kwa uchache Sana, Hatua za ukuaji na maendeleo ya mtu katika Saiko-jamii. Nitatumia zaidi nadharia ya mwanasaikolojia mmoja aitwaye Erik Erikson.

Erik Erikson alitoa hatua nane za ukuaji na maendeleo ya mtu katika Saiko-Jamii, hatua hizo nitazitaja na kuzifafanua Kwa njia rahisi kabisa, ili hata Wale ambao hasakufika Chuo, au kutosoma kozi za Saikolojia wapate maarifa;

1: TRUST Vs MISTRUST " KUAMINIANA dhidi ya KUTOAMINIANA. (Age 0-1½)
Mtoto wa miaka 0- 1½ unapomfanyia matendo ya Wema na upendo mara Kwa mara"thabiti"(consistently), unatabirika(predictable) na wakutegemewa au kuaminika(Reliable) basi TRUST itazaliwa, mtoto atakuamini, yaani kutakuwa na kuaminiana.

Lakini kama utunzaji wa mtoto"malezi" yatakuwa kinyume na Uthabiti, hayatabiriki na sio Reliable (hatategemewi au hayaaminiki) basi kinachotokea ni mtoto kukushuku(Suspicion), Hofu(Anxiety) na kutoaminiana(MISTRUST).

Ukifanikiwa katika hatua hii mtoto atakuwa na Tumaini "HOPE" yaani kukutumaini, kukutegemea, kukuamini.
Kipindi hiki unapaswa mtoto umlee Kwa upendo, matendo yako na maneno yako yawe ya Wema.

2. AUTONOMY Vs SHAME and DOUBT "KUJITAWALA dhidi ya AIBU na MASHAKA" (Age 1½-3)
Umri huu mtoto atakuwa anahitaji kujitawala, kujitegemea na kuwa huru kufanya vitu mwenyewe Kama kutembea Kwa miguu yake, kunywa au Kula pekeake, na kufanya vishughuli vya hapa na pale.

Mzazi unachopaswa kufanya ni Kumsapoti mtoto na kumsaidia, pale anapohitaji msaada. Hii itamjengea kitu inaitwa KUJIAMINI "CONFIDENCE"

Kumtawala na kumkataza mtoto kuliko pitiliza au kumkemea mtoto bila kumpa fursa ya yeye kufanya mwenyewe kutamfanya asijiamini kuwa anaweza kufanya vitu yeye mwenyewe pasipo kusaidiwa.

Kama utafanikiwa kumjengea mtoto Kujitawala basi utaunda ARI YA NAWEZA "WILL" ya mtoto.
Kushindwa ni kumfanya mtoto awe na Aibu na mashaka na asijiamini.

Hii itamuathiri huko mbeleni akiwa umri wa utu uzima

3. INITIATIVE Vs GUILTS. " ARI, SHAUKU Dhidi ya HATIA" (Age 3-5)
Kipindi hiki mtoto anakuwa na Ari au shauku ya kufanya vitu vingi, ataongeza kujichanganya na watoto wenzake, atakuwa mwingi WA maswali. Unachopaswa kufanya ni kuyachukulia maswali na mambo yote anayofanya kuwa ni muhimu na yanamaana kubwa hii itamfanya awe na KUSUDI "purpose"

Lakini kama utayaona mambo yake na maswali ya mtoto hayana maana au ni upuuzi, au usumbufu au kero utamfanya mtoto "ajihisi hatia" na hii ipo upande wa negative impact kuanzia stage one mpaka mwisho.

4. Competence Vs Inferiority. " UMAHIRI dhidi ya UDHALILI au UDUNI" (Age 5-12).
Hapa mtoto atakuwa anataka kufanya mambo Kwa ufanisi mkubwa, umahiri mkubwa, atakuwa anahitaji kujifunza mambo makubwa, kujua kusoma na kuandika, pia atazidisha kuchangamana na makundi "peer group". Kipindi hiki mtoto chanzo chake kikuu cha "KUJITHAMINI" (Self-esteem) kitakuwa ni marafiki wa nje. Kujithamini Kwa lugha rahisi ni "kutambua utu wako" hivyo mtoto atatambua utu wake(atajithamini) kupitia marafiki au watu wanaomzunguka.

Hapa mzazi ndio maana itampasa ahakikishe na kuratibu marafiki au watu wanaomzunguka M/watoto wake ili kujenga tabia njema ya mtoto.

Mzazi hapaswi kumtolea maneno machafu na maneno ya kushindwa Kwa mtoto pale anapofanya Jambo lake, wala hapaswi kumlinganisha mtoto wake na Watoto wengine, yaani kuwasifia watoto wengine na kumkosoa Sana mtoto wake, hii itamfanya azidi kujiimarisha kufanya zaidi na zaidi ili afanye vizuri zaidi.

Mzazi lazima uelewe kuwa Mtoto akiwa amefanya vibaya katika Jambo Fulani anafahamu na anaumia Kwa kushindwa kufanya vizuri, hivyo unapaswa umsapoti, umsaidie, na kumpa moyo kuwa amejitahidi na amekaribia kuweza, hii itamfanya awe Mahiri"competent" kwani atakuwa anajaribu mara Kwa mara mpaka atakapoweza kabisa.

Ukimkosoa mtoto atajisikia "dhalili" "Duni" (inferior) na hiyo itamuathiri huko mbeleni.

5. IDENTITY Vs Role Confusion, " UTAMBULISHO dhidi ya KUTOKUWA NA UTAMBULISHO ( Age 12-18)
Hiki ni kipindi cha balehe, mtoto tayari anaanza kuwaza atakuwa Nani, aidha ni mwalimu, Daktari, mhasibu,
Ataanza kuwaza mahusiano ya kimapenzi, na kuchagua Aina ya mwenza amtakeye kwenye maisha yake, nyumba na magari anayoyataka. Kipindi cha kuwaza Future (siku zijazo).

Hapa kuna Mabadiliko ya kimwili kutokana na Balehe, Mabadiliko haya yanaweza kuathiri akili na tabia ya mtoto Kwa namna Hasi au chanya.

Utambulisho wa mtoto utazingatia zaidi jamii yake inayomzunguka, lakini endapo itatokea mtoto akapenda kazi ambayo haiheshimiwi ndani ya jamii mfano Mwana muziki, au Mcheza Singeli, hii itamfanya apate Role Confusion au Identity Crisis yaani hatajua au hajui baadaye atakuja kuwa Nani.

Hii itamfanya hata akisomea Fani au Taaluma Fulani nje ya kile anachokipenda asikifurahie.

6. INTIMACY Vs ISOLATION " UKARIBU au URAFIKI dhidi ya KUTENGWA.(Age 18-40)
Kipindi hiki ndio ambao wengi wetu tupo hapo. Ni kipindi ambacho Saikolojia ya binadamu inahitaji Wenza wa maisha, kila mtu anahitaji familia yake binafsi, Mume/mke na watoto.

Akili na hisia za binadamu kipindi hiki inahitaji ukaribu na watu wa nje zaidi(mke au mume) kuliko ndugu WA damu moja.

Mtu yeyote aliyekatika umri huu akikosa au akizuia ukaribu au urafiki au Wenza au mahusiano basi atasababisha UPWEKE "LONELINESS" na UNYOGOFU " Depression" ndio huzuni ya Moyo, uchungu, sonona n.k.

Ikiwa mtu atafanikiwa kujenga ukaribu au mahusiano katika kipindi hiki basi kutazuka kitu kina "UPENDO" (LOVE) Akishindwa basi ndio hivyo tunapata Upweke na Unyogofu.

7. GENERATIVITY Vs STAGNATION "UZALISHAJI Dhidi ya KUKOSA TIJA"VILIO" (Age 40-65)
Kipindi hiki Mtu anakuwa Mtu mzima, ambaye anahitaji kuacha Alama njema katika jamii yake, Kwa kukuza watoto na kuwalea katika njia nzuri. Shauku ya kushiriki katika shughuli za kijamii huongezeka, Kipindi hiki Mtu atahitaji afanye kila analoweza kulinda familia yake na jamii yake.

Kwa ambaye ataenda kinyume na hivyo atajiona Hana tija ndani ya jamii na hii itampelekea kuwa na vilio ndani Kwa ndani. Hii hutokea zaidi Kwa wanaume zaidi, mwanaume katika umri huu Kama haoni Mchango wake ndani ya familia yake au jamii yake huugulia ndani Kwa ndani na wengine huishia kupata magonjwa na kufa kabisa. Wanawake sio Sana kutokana na kuwa Wao hawana Wajibu mkubwa katika kujenga jamii au familia Kama Mwanaume.

8. EGO INTEGRITY Vs Despair " UADILIFU AU UKAMILIFU BINAFSI dhidi Ya KUKATA TAMAA(Age 65)
Hiki ni kipindi cha ambacho mtu haangalii tena mbele isipokuwa anaangalia alipotoka, kipindi hiki Mtu hujivunia mambo mazuri aliyokwisha kuyafanya katika maisha yake, hujazwa na Hekima na busara, pia huongozwa zaidi na Busara na maadili.

Pia ni kipindi cha Kukata tamaa kwa kuangalia siku za mbele zilizobaki kuwa zimeisha, lakini ni kipindi cha majuto Kwa kuangalia makosa yote uliyoyafanya katika maisha yako.

Ni wajibu wetu Kama wazazi kuhakikisha tunaelewa hatua za ukuaji na maendeleo yetu na yawatoto wetu kusudi kuepusha madhara yanayoweza kutukia huko mbeleni.

Shughuli zetu za uzalishaji na majukumu yetu ya kimaisha tujitahidi yasiathiri malezi ya watoto wetu.
Kwa wale ambao watoto wao wanalelewa na Wasaidizi wa kazi za ndani "Housemaid" tunapaswa kuwa Makini katika kuchagua Aina ya Maids wa Kulea watoto wetu.

Pia shule tunazopeleka watoto wetu, iwe Daycare au shule za msingi au sekondari tuhakikishe kuwa zina usalama wa kutosha wa kimalezi kuwakuza watoto wetu.

Makanisa na misikiti pia tunapowapeleka watoto tuhakikishe Waalimu, maimamu, ostadhi na Wachungaji wanaowafundisha watoto wetu wanavigezo vyote vya kimaadili na kielimu.

Kufikia hapo Taikon Sina la ziada!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Kahama, shinyanga.
 
Kweli asee Niko stage namba sita toka nipate mwali Basi nimewatenga ndugu zangu.huu NI upumbavu kuanzia Sasa nitakuwa nikiwapigia Simu mama zangu wadogo na ndugu zangu Mara tatu kila week lengo la kwanza NI kuwatoa ktk hali ya upweke maana wao wako above 40..naanza sasa.mke mwenyewe ananizingua TU hana jipya kazi kuninyenga TU..ubarikiwe mtoa maada
 
Kweli asee Niko stage namba sita toka nipate mwali Basi nimewatenga ndugu zangu.huu NI upumbavu kuanzia Sasa nitakuwa nikiwapigia Simu mama zangu wadogo na ndugu zangu Mara tatu kila week lengo la kwanza NI kuwatoa ktk hali ya upweke maana wao wako above 40..naanza sasa.mke mwenyewe ananizingua TU hana jipya kazi kuninyenga TU..ubarikiwe mtoa maada
[/QUOTE


Shukrani Sana Mkuu!

Wazazi wanahitaji ukaribu wetu na kuwaondolea upweke wao, majuto Yao n.k
 
Mzee wangu yupo kwenye 40-60 na kwa kuwa wote ni wanaume basi najitahidi kuwa naye karibu sana namsaidia vitu vidogo vidogo kujenga ukaribu zaidi. Kupitia hivyo naona anazidi kuwa na furaha sana na pia nafaidi hekima kubwa nilioikosa wakati nikiwa shule.

Nilivofikisha miaka 15 ndio nikawa beneti nae sana. Likizo ilikuwa inatumika kukaa nae sana katika uzalishaji .

Nilivokuwa mkoa wa mbali sana chuoni basi utakuta kakupigia afu haongei kitu basi najua huyu mzee kanimiss basi tunaanza kupiga mazungumzo. Yeah😂. Watoto wa kiume shindeni pamoja na wazee wenu haya shauri yenu. Sio kila muda na kinamama tu.

I love you mzee.
 
Vipindi vya mwanzo wa makuzi ya mtoto kabla hajafika 18 ndio vya muhimu zaidi, vinajenga afya ya akili na mwili wa mtoto.
 
Mzee wangu yupo kwenye 40-60 na kwa kuwa wote ni wanaume basi najitahidi kuwa naye karibu sana namsaidia vitu vidogo vidogo kujenga ukaribu zaidi. Kupitia hivyo naona anazidi kuwa na furaha sana na pia nafaidi hekima kubwa nilioikosa wakati nikiwa shule.
Nilivofikisha miaka 15 ndio nikawa beneti nae sana. Likizo ilikuwa inatumika kukaa nae sana katika uzalishaji . Nilivokuwa mkoa wa mbali sana chuoni basi utakuta kakupigia afu haongei kitu basi najua huyu mzee kanimiss basi tunaanza kupiga mazungumzo. Yeah😂. Watoto wa kiume shindeni pamoja na wazee wenu haya shauri yenu. Sio kila muda na kinamama tu.
I love you mzee.


Wamama usiposhinda nao wanaweza kukuloga😂😂😂
 
Mzee wangu yupo kwenye 40-60 na kwa kuwa wote ni wanaume basi najitahidi kuwa naye karibu sana namsaidia vitu vidogo vidogo kujenga ukaribu zaidi. Kupitia hivyo naona anazidi kuwa na furaha sana na pia nafaidi hekima kubwa nilioikosa wakati nikiwa shule.
Nilivofikisha miaka 15 ndio nikawa beneti nae sana. Likizo ilikuwa inatumika kukaa nae sana katika uzalishaji . Nilivokuwa mkoa wa mbali sana chuoni basi utakuta kakupigia afu haongei kitu basi najua huyu mzee kanimiss basi tunaanza kupiga mazungumzo. Yeah. Watoto wa kiume shindeni pamoja na wazee wenu haya shauri yenu. Sio kila muda na kinamama tu.
I love you mzee.
big up Sana mkuu.nime kukubali!!

hawa ndg zetu ,KE,NI wabinafsi Sana na huwa wanatugombanisha na kutufitinisha na watt wetu Sana .
 
Back
Top Bottom