Faida za Maharage

klorokwini

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
8,648
5,139
Baada ya kufanya resechi wiki 2 mfululizo mimi na ex wangu bila waifu kujua, tumegundua kumbe hata maharage pia yana faida (hii ni habari njema kwa walalahoi), nitazitaja faida kwa kiswahili.

NB: hii sredi yangu naomba isiwe sababu ya kupandishwa bei ya maharage nchini.

Faida za maharage

1) Maharage yanasaidia kumlinda mtu kutokana na safura (anaemia) kwavile yana Iron nyingi (hii ni Iron ya mineral sio chuma cha kuulia mwizi)

2) Maharage yana fibre nyingi kwahiyo yanasaidia kwenye shuhuli ya maliwatoni iwe bila kutoka jasho (inasaidia kuondosha constipation)

3) Maharage yanajenga misuli, ndo maana jamaa wa uswahilini ni tabu sana kuwaibia wake zao.

4)Inapunguza kolesterol (kitambi si sifa wajameni)

5) Pia inasadikiwa kulinda na kutibu sukari.

Ujumbe: kanunueni maharage haraka haraka kabla hayajapotea sokoni.

Nimemaliza,
hakuna masuali wala mkopo.
 
hivi kuna mbongo asiependa wali na maharage?
sidhani aisee

Mbona mimi najua wengi hawapendi, atleast nnaowafahamu mimi.Wakisikia maharage wanaywea, ukitaka kuwafurahisha wakarangizie nyama au samaki.
 
Dr Kloro,asante sana. Umesahau faida kuu, ni chanzo cha protini ambayo hujenga mwili(suala #3). Ila maharagwe ya soya pekee ndo 1st class protein sawa na nyama.
 
Mbona mimi najua wengi hawapendi, atleast nnaowafahamu mimi.Wakisikia maharage wanaywea, ukitaka kuwafurahisha wakarangizie nyama au samaki.

umeona RR alivyouliza hapo juu?
tupo wengi mno wa wali na maharage...
mimi nyama sipendi kabisa....

by the way mnayajua maharage meupe makubwa makubwa hivi?????acha mchezo hayo
 
Dr Kloro,asante sana. Umesahau faida kuu, ni chanzo cha protini ambayo hujenga mwili(suala #3). Ila maharagwe ya soya pekee ndo 1st class protein sawa na nyama.
Senksi nurse wangu, Hapo kwenye protein pia wanasemaga inasaidia nywele kuwa strong, yaani maharage nimeyafanyia research ya nguvu kuliko research ya kutafta mchumba.
 
umeona RR alivyouliza hapo juu?
tupo wengi mno wa wali na maharage...
mimi nyama sipendi kabisa....

by the way mnayajua maharage meupe makubwa makubwa hivi?????acha mchezo hayo

Mimi mwenyewe napenda vyakula vingi na maharage isipokua ugali, labda kuwe na mboga za majani pembeni.Ila asilimia karibu tisini ya ndugu na marafiki zangu hawapendi kabisa.
 
Lol! Hapo kwenye nywele ndo unamsifia lizzy wako kisirisiri eeh? Faida nyingine ya maharagwe mi naogopa kuitaja banaa!
Senksi nurse wangu, Hapo kwenye protein pia wanasemaga inasaidia nywele kuwa strong, yaani harage nimelifanyia research ya nguvu kuliko research ya kutafta mchumba.
 
Lol! Hapo kwenye nywele ndo unamsifia lizzy wako kisirisiri eeh? Faida nyingine ya maharagwe mi naogopa kuitaja banaa!

Kama itapandisha mzuka usiitaje, azawaizi lipuka tu bana, au ni ile ya gesi asilia?
 
Mimi mwenyewe napenda vyakula vingi na maharage isipokua ugali, labda kuwe na mboga za majani pembeni.Ila asilimia karibu tisini ya ndugu na marafiki zangu hawapendi kabisa.

ha haaa umenikumbusha gazeti letu la udaku....'supestar lizzy asema yeye hali ugali na maharage lol
mwanaume anaemtaka ajiandae kwa ma burgers na ma pizza lol
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom